Wizara ya elimu wekeni somo la uzalendo

Wizara ya elimu wekeni somo la uzalendo

jina baya

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2014
Posts
573
Reaction score
381
Wakuu habari,

Limekuwepo tatizo kubwa sana katika nchi yetu la viongozi wakubwa kabisa katika ngazi mbalimbali kukutwa na kashfa za ajabu za rushwa au kushiriki katika matukio yasiyo na maadili.

Tatizo hili limeonekana sugu kabisa tena na linahusisha hadi wasomi wakubwa waliosoma kati ya vyuo bora hapa Africa kwa kipindi hicho ambacho ni UDSM

Nimejaribu kukaa chini na kulinganisha na taifa moja.
Katika taifa hilo, wanafunzi wa vyuo vikuu wanawekewa bidhaa mbalimbali kwenye korido za vyuo vyao na wanapohitaji huduma hujihudumia wenyewe na kuacha pesa hapo. Kumbuka bidhaa hizo hazilindwi bali zikiisha zinaongezwa na mahesabu yanafanyika.

Pale ambapo bidhaa itaonekana imepungua na pesa haipo basi wanachuo hao hawapati ajira kabisa katika nchi hiyo.

Katika nchi yetu tunaweza kuanzisha somo la uzalendo na maadili ili kuwajenga watoto wetu katika maadili yanayofaa.
Mfano, somo likawepo kuanzia darasa la kwanza likawa na historia za mashujaa na matukio ya kizalendo waliyowahi kufanya zamani.
Hii itasaidia watoto kujifunza kuwa wazalendo na wenye maadili na mapenzi kwa nchi yao.
Somo hilo lisiwe na mtihani wowote.
 
Wewe mtoa mada unajua maana ya Uzalendo.

uzalendo nikupigana tafu nakutenda haki .

kama unaviwanja viwili ugawe kimoja .
 
uzalendo hafundishwi ni culture iliopo katika jamii inarithiwa. Mtu anapata huduma bora za afya, elimu bora, na anaona kodi yake inavyofanya kaz na hakuna aliyejuu ya sheria kusema yy ni bora zaidi kuliko wengine.
 
uzalendo kwa tanzania ni uongo wa kusadikika...viongozi kila siku wanatupigia kelele kuhusu uzalendo...lakin ukifanya uzalendo kwa vitendo hao hao viongozi wanakufanya adui na ikiwezekana wanaandaa mipango ya kukupoteza na ikiwezekana upotee mazima (ufe)....
 
Kila kitu kikiwekwa kama somo mbona watoto watachanganyikiwa. Mara tuwe na somo la Mazingira, amani, rushwa leo uzalendo kesho Umoja, keshokutwa mshikamano.
 
Nani atalifundisha hilo somo?

Umeshawahi kupewa ushauri wa kuimarisha ndoa na mtu aliyeoa mara tano anaacha?

Au muuza vitabu vya kupata utajiri ndani ya wiki mbili ambao anatembea nyumba kwa nyumba kuuza vitabu?
 
Ubongo wa watanzania walio wengi umejaa vitabu tu lakini zile akili zingine zinaitwa za kuzaliwa tayari zime evaporate kutokana na huu ujinga unaitwa utandawazi.

Na wasomi ni mizigo mizito kuliko hata majabari kwa sahivi, uvivu hadi kwenye masikio yao
 
Mbongo na wizi ni samaki na maji,unawakumbuka wale waliosoma vyuo vikuu enzi za nyerere na walisomeshwa bure ndo hao mafisadi nambari moja mfn
1.Lowassa
2 .j.k
3.sitta
4.chenge
5.kabudi,
6.mahiga
Hawa ndo wanaiharibu nchi kwa kushirikiana na akina Livingstone Lusinde,msukuma,mbowe(mazuzu)
 
Wakuu habari,

Limekuwepo tatizo kubwa sana katika nchi yetu la viongozi wakubwa kabisa katika ngazi mbalimbali kukutwa na kashfa za ajabu za rushwa au kushiriki katika matukio yasiyo na maadili.

Tatizo hili limeonekana sugu kabisa tena na linahusisha hadi wasomi wakubwa waliosoma kati ya vyuo bora hapa Africa kwa kipindi hicho ambacho ni UDSM

Nimejaribu kukaa chini na kulinganisha na taifa moja.
Katika taifa hilo, wanafunzi wa vyuo vikuu wanawekewa bidhaa mbalimbali kwenye korido za vyuo vyao na wanapohitaji huduma hujihudumia wenyewe na kuacha pesa hapo. Kumbuka bidhaa hizo hazilindwi bali zikiisha zinaongezwa na mahesabu yanafanyika.

Pale ambapo bidhaa itaonekana imepungua na pesa haipo basi wanachuo hao hawapati ajira kabisa katika nchi hiyo.

Katika nchi yetu tunaweza kuanzisha somo la uzalendo na maadili ili kuwajenga watoto wetu katika maadili yanayofaa.
Mfano, somo likawepo kuanzia darasa la kwanza likawa na historia za mashujaa na matukio ya kizalendo waliyowahi kufanya zamani.
Hii itasaidia watoto kujifunza kuwa wazalendo na wenye maadili na mapenzi kwa nchi yao.
Somo hilo lisiwe na mtihani wowote.
akili ndogo hufikiri kidogo uzalendo hauji kea kujifinza bali ni imani ambayo ina pa kuanzia
 
Uzalendo haufundishwi darasani, uzalendo ni matokeo ya matendo yanayofanywa na serikali kwa wananchi wake.

Tafakari upya, mbona hamna so la udugu ila watu wanakuwa na ndugu mbalimbali.
 
uzalendo hafundishwi ni culture iliopo katika jamii inarithiwa. Mtu anapata huduma bora za afya, elimu bora, na anaona kodi yake inavyofanya kaz na hakuna aliyejuu ya sheria kusema yy ni bora zaidi kuliko wengine.
Nimetoa mfano wa kanchi flani ambako tulikopi BRN vyuoni wanavyofanya.. Je pale inasaidia nini? Hatuwezi kufanya hivyo na sisi?
 
Nani atalifundisha hilo somo?

Umeshawahi kupewa ushauri wa kuimarisha ndoa na mtu aliyeoa mara tano anaacha?

Au muuza vitabu vya kupata utajiri ndani ya wiki mbili ambao anatembea nyumba kwa nyumba kuuza vitabu?
[emoji41][emoji41][emoji41]
 
Somo LA uzalendo ni muhimu sana na pia lazima nchi kama inchi ikae na iweke Sera za kiinchi kuliko kichama
 
Uzalendo haufundishwi darasani, uzalendo ni matokeo ya matendo yanayofanywa na serikali kwa wananchi wake.

Tafakari upya, mbona hamna so la udugu ila watu wanakuwa na ndugu mbalimbali.
Serikali inaongozwa na hao waliokulia katika mazingira yasiyohamasisha wawe wazalendo ndo maana wapo viongozi wanaokula rushwa bila aibu kabisa
 
Uzalendo hauji kwa kufundishwa shuleni. Ni matokea ya maisha ndani ya familia na jamii, maisha ya imani na ustaarabu wa kujali. Kama wazazi wako hawakuwa na uzalendo huwezi kuwa nao ukifika shule. Kama viongozi wa kiimani hawana mfano unaoenenda na mafundisho yao hwawezi kuwa chanzo cha uzalendo. Na kama utamaduni wa nchi ni wa kutojali wengine hakuna chemichemi ya uzalendo. Hata shuleni hutawapata waalimu wa uzalendo.
 
Uzalendo unaanzia pale panapokuwa na utu. Penye utu, kuna haki na kujali kila mtu na kila jambo.
Kwa Tz, Ubinafsi hasa wa walio na madaraka, ambao wamesomeshwa mambo ya Uzalendo enzi zao, ndio unalibomoa Taifa.
 
Back
Top Bottom