kabwekasoma
JF-Expert Member
- Jul 24, 2016
- 260
- 153
Kwa heshima na taadhima naomba kushauri suala la elimu kwa nia njema maana yake inaenda kuwa chakavu na mbaya kutokana na upungufu mkubwa wa rasilimali watu (waalimu) katika shule nyiingi ukianzia shule ya Msingi mpaka Sekondari.
Hali ni mbaya mashuleni kuanzia shule ya msingi kwani kuna baaadhi ya shule za msingi zina wanafunzi 800 lakini walimu waliopo hawazidi 9.Tunajua kuwa serikali inatumia pesa nyingi katika kugharamia elimu bure ili watoto wetu wapate elimu na mwitikio wa wazazi umekuwa mkubwa kwa wazazi kuwapeleka watoto mashuleni hivyo kufanya idadi ya wanafunzi kuwa kubwa.
Elimu yetu inachangamoto kubwa sana lakini kwa hili la waalimu Serikali ilitupie macho kwani kwa shule za msingi ni balaaa kubwa na ikumbukwe msingi mzuri wa elimu unajengwa kuanzia chini labda kama Serikali itakuwa imeamua kuwakusanya vijana pamoja mashuleni iliwapige soga na kisha kurudi nyumbani.
Ukija upande wa Sekondari huko ndo balaa zaidi kwani shule unaweza ukakuta haina mwalimu wa hesabu wala fizikia shuleni nzima Serikali imejitahidi kuajiri waalimu lakini mara nyingi inakuwa walimu 2000 ambapo kiwastanii kwa shule zilizopo Tanzania hata mwalimu mmoja mmoja hatoshi. Ubora wa elimu haupimwi kwa matokeo unapimwa kwa skills and competence ya mwanafunzi alionao kichwani.
Nashauri serikali iajiri walimu kwa shule za msingi Tanzania angalau walimu wa3 kila shule ya msingi na upande walimu wasayansi kwa shule za sekondari angalau wa5 kwa kila Shule Sekondari, TAMISEMI na Wizara ya Elimu najua ujumbe wangu utawafikia