Wizara ya Elimu katika marekebisho ya mtaala mpya wa elimu ya msingi Irudishe usomaji wa hadithi katika masomo ya Lugha

Agrey998

JF-Expert Member
Jul 8, 2019
398
518
Wengi wetu katika Elimu yetu ya msingi katika masomo ya lugha tulisoma hadithi mbalimbali zilizotusaidia kukuza uwezo wetu wa kusoma na kuandika kwa wakati ule, hadithi kama Juma na Uledi, punda wa Dobi, Gulio, Hawafu mwenye Nguvu zilikua maarufu sana kipindi kile na ilivutia watoto wengi kupenda kujifunza kusoma ili kuweza kufurahia hadithi hizo.

Hii ilisababisha hata kukuza uwezo wa watoto kujifunza kusoma kwa haraka zaidi na ilikua ni ngumu kukuta mtoto katika darasa la nne hajui kusoma.

Lakini kwa sasa idadi ya watoto wanaoenda shule lakini wana uwezo mdogo wa kusoma ni mkubwa tofauti na zamani na pia wengine huchelewa sana kujua kusoma, Fasihi andishi katika hatua za awali za shule ya msingi ilikua na msaada mkubwa sana, ningependa kuwasilisha kwa kusema ni vema wizara ya elimu ikatizama upya Mtaala iliyobadilisha na kuurudisha ule wa awali au kuja na njia nyingine ambayo ni sahihi zaidi ya ile ya usomaji wa vitabu.

Nawasilisha

Sent from my SHV43 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom