Wizara ya afya yatoa tangazo la nafasi za masomo kwa mwaka wa masomo 2013/2014 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wizara ya afya yatoa tangazo la nafasi za masomo kwa mwaka wa masomo 2013/2014

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Access Denied, Mar 10, 2013.

 1. Access Denied

  Access Denied JF-Expert Member

  #1
  Mar 10, 2013
  Joined: Aug 10, 2012
  Messages: 627
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Tangazo la kozi za Afya - 2013JAMHURI YA MUUNGANO YA TANZANIAWIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMIIMAOMBI YA NAFASI ZA MAFUNZO MWAKA WA MASOMO 2013/14Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii anakaribisha maombi ya kujiunga na kozi mbalimbali zinazotolewa na Wizara ya Afya kwa mwaka wa masomo 2013/2014.1. Kozi zinazotangazwa ni:A. Kozi za ngazi ya Stashahada:(i) Afisa Afya ya Mazingira (Assistant Health Officer)(ii) Fiziotherapia (Physiotherapy)(iii) Fundi Sanifu Meno (Dental Laboratory Technologist)(iv) Mteknolojia Maabara (Laboratory Technician- off Campus)-Watajitegemea Malazi(v) Optometria (Optometry)(vi) Tabibu (Clinical Officer)(vii) Tabibu Meno (Dental Therapist)(viii) Uuguzi Daraja ‘’A’’ (Diploma in Nursing)B. Kozi za ngazi ya Cheti(i) Fundi Sanifu Maabara Msaidizi (Laboratory Assistants)(ii) Mtunza kumbukumbu za Afya (Health Record Technicians)(iii)Tabibu Msaidizi (Clinical Assistants)(iv) Uuguzi Daraja ‘’B’’ (Certificate in Nursing)C. Mafunzo ya Tabibu kwa njia ya masafa (Distance Learning) kwa wale waliohitimu mafunzo ya Tabibu Msaidizi mwaka 2009.2. Muda wa Mafunzo:(i) Miaka mitatu kwa kozi za Stashahada(ii) Miaka miwili kwa kozi za Ngazi ya cheti3. Sifa za Muombaji:Waombaji watarajali (Pre-service):(i) Awe raia wa Tanzania(ii) Awe amemaliza kidato cha nne au sita kati ya mwaka 2008 na kuendelea(iii)Ufaulu wa kidato cha nne uwe wa kiwango kisichopungua alama ya ‘C’, katika masomo ya Biologia na Kemia , na alama ‘D’ kwa somo la Fizikia kwa kozi za Stashahada . Alama hizi zipatikane katika kikao kimoja tu cha mitihani.(iv) Cheti chake cha kidato cha nne, kionyeshe ufaulu usiopungua point 28 kwa kozi za cheti. Aidha ni lazima awe na ufaulu usiopungua (minimum) alama ‘D’, kwa masomo ya Biologia, Kemia na Fizikia. Alama hizi zipatikane katika kikao kimoja tu cha mtihani.(v) Kwa wale waliomaliza kidato cha sita na wanaohitaji kujiunga na mafunzo ya stashahada, wawe na alama isiyopungua ‘E’, kwa masomo ya Biologia, Kemia na Fizikia. Ufaulu huu uwe umepatikana katika kikao kimoja tu cha mtihani.(vi) Kufaulu somo la Kiingereza na Hisabati ni sifa ya nyongeza.Tangazo la kozi za Afya - 2013 Page 2Waombaji wa Mafunzo ya Masafa (Distance learning:A. Wanaotakiwa kujiunga na Bridging course kabla ya kuendelea na masomo ya NTA 6 (Clinical Officer)i. Awe amemaliza kidato cha nne na kupata ufaulu wa angalau alama “D” katika masomo manneii. Awe na cheti cha kuhitimu mafunzo ya waganga wasaidizi vijijini mwaka 1999 na kurudi nyuma.B. Tabibu wasaidizi (NTA 5) Wanaotakiwa kuendelea na masomo ya NTA 6 (Clinical Officer)i. Awe amemaliza kidato cha nne na kupata ufaulu wa angalau alama “D” katika masomo manne.ii. Awe na cheti cha kuhitimu mafunzo ya Tabibu wasaidizi (NTA 5) mwaka 2009.4. Utaratibu wa kutuma maombi:(i) Fomu za maombi zitapatikana kwa wakuu wa kanda za mafunzo zilizoainishwa hapo chini (rejea kipengele Na. viii) chini, Waganga Wakuu wa wilaya na wakuu wa vyuo vya afya vilivyo chini ya Wizara.(ii) Waombaji wote watalipia fomu kwa sh. 15, 000/=. Risiti halisi ya Benki kwa ajili ya malipo haya, itawasilishwa pamoja na fomu za maombi. Kiasi hiki cha fedha hakitarejeshwa (Non refundable).(iii)Malipo yaingizwe kwenye akaunti ,‘Health Service fund’, Account No. 0111-030-12059 NBC – CORPORATE BRANCH.(iv) Maombi yatakayopokelewa na kufanyiwa kazi, ni yale yatakayoambatanishwa na risiti halisi ya malipo ya Benki, inayoonyesha kiwango cha malipo kilichotajwa hapo juu.(v) Maombi ambayo hayataambatanishwa na hati ya malipo ya Benki(Pay in Slip) na kivuli cha cheti cha Baraza la Mitihani cha kuhitimu Elimu ya Sekondari, hayatafanyiwa kazi.(vi) Maombi yote yatapokelewa kupititia kanda za mafunzo baada ya malipo kufanyika kwenye akaunti iliyotajwa hapo juu.(vii) Fomu za maombi zijazwe na zitumwe kwa katibu mkuu, wizara ya afya na ustawi wa jamii,kupitia anwani za wakuu wa kanda kulingana na eneo muombaji alipo.(viii) Anwani za Wakuu wa Kanda ni kama zilivyoainishwa hapa chini:-a) Mratibu wa Kanda ya Mashariki (Mikoa ya Morogoro na Pwani) - Chuo cha Mafunzo ya Afya ya Jamii – S.L.P. 1060, Morogoro.b) Mratibu wa Kanda ya Magharibi (Mikoa ya Kigoma na Tabora) – Chuo cha Tabibu Wasaidizi, S.L.P. 458, Kigomac) Mratibu wa Kanda ya Kusini (Mikoa ya Lindi na Mtwara)– Chuo cha Tabibu, S.L.P. 86, Mtwara.d) Mratibu wa Kanda ya Kaskazini (Mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro na Tanga)– Chuo cha CEDHA, S.L.P.1162, Arusha..e) Mratibu wa Kanda ya Nyanda za Juu kusini Magharibi (Mikoa ya Rukwa na Mbeya) – Chuo cha Madaktari Waasaidizi, S.L.P. 1142, Mbeya.f) Mratibu wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (Mikoa ya Ruvuma na Iringa)– Chuo cha Afya ya Jamii, S.L.P. 235, Iringa.g) Mratibu wa Kanda ya Kati (Mikoa ya Singida na Dodoma) – Chuo cha Uuguzi Mirembe, S.L.P. 595, Dodoma.h) Mratibu wa Kanda ya Ziwa (Mikoa ya Mwanza, Mara, Kagera na Shinyanga) – Chuo cha Madaktari Wasaidizi, S.L.P. 11351, Mwanza.i) Mkurugenzi wa Taasisi za Sayansi Shiriki za Afya Muhimbili, S.L.P 65005, Dar-es-salaam.j) Mkuu wa Chuo cha Madaktari Wasaidizi-Tanga, S.L.P 5030, Tanga.k) Mkuu wa Chuo cha Tabibu-Kibaha, S.L.P 30282, Kibaha5. Utaratibu wa kutoa taarifa kwa waliochaguliwa:a) Wizara itakuwa na wajibu wa kuwataarifu wale wote watakaofanikiwa kuchaguliwa kujiunga na kozi mbalimbali kupitia magazeti, ‘website’ ya Wizara na mbao za matangazo Wizarani na Kanda za Mafunzo.b) Taarifa hizo zitatumwa pia kwenye kanda za mafunzo kama zilivyoainishwa hapo juu.6. Muda wa mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 30 Aprili, 2013.7. Muhula wa masomo unatarajiwa kuanza tarehe 1 Oktoba, 2013.Imetolewa na:Katibu Mkuu,Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,S.L.P. 9083,Dar es Salaam.
   
 2. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #2
  Mar 10, 2013
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,093
  Likes Received: 529
  Trophy Points: 280
  Hivi siku hizi kusoma kozi za afya lazima usome physics? Hata nursing na maabara? Maana kuna watu waliacha physics form two ila wana ufaulu mzuri wa cbg na maths na advance hawakufanya vizuri. Sijaona ulazima wa kuzuia watu waliofaulu bios na chem wasisome nursing, maabara na health officers labda clinical officer, dental, radiotherapy. Au ndo yale ya documents ambazo zinaandikwa tu bila kufanyiwa kazi?
   
 3. S

  Sheko JF-Expert Member

  #3
  Mar 11, 2013
  Joined: Mar 9, 2013
  Messages: 284
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
   
 4. BLESS MIHILA

  BLESS MIHILA JF-Expert Member

  #4
  Mar 12, 2013
  Joined: Dec 22, 2012
  Messages: 305
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 45
  Tunashukuru kwa taarifa kwenye familia
   
 5. Ben40

  Ben40 Senior Member

  #5
  Mar 13, 2013
  Joined: Apr 18, 2012
  Messages: 191
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Wadau vyuo vp ni vzuri kwa ngazi ya cheti medical lab.?
   
 6. S

  Sheko JF-Expert Member

  #6
  Mar 14, 2013
  Joined: Mar 9, 2013
  Messages: 284
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi jamani namboni kuuliza mimi nimemaliza kidato cha 4 mwaka jana na hapo vigezo vyote ninavyo vya kujiunga na hivyo vyuo sababu nimepata BIO C,CHEM C na PHYS D. Hasa nikianza na ngazi ya cheti itanikost miaka mingapi hadi kufikia university naombeni mnijuze wakuu
   
 7. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #7
  Mar 14, 2013
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,319
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Nimeshindwa kusoma
   
 8. B

  BGG Senior Member

  #8
  Mar 16, 2013
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 136
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  unasoma miaka mitatu na unapata NTA Level 6 ambayo nikigezo cha wewe kuingia chuo kikuu moja kwa moja
   
 9. S

  Sheko JF-Expert Member

  #9
  Mar 16, 2013
  Joined: Mar 9, 2013
  Messages: 284
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  asante sana mkuu kwa kunijuza.ila hapo ina maana kwamba diploma nasoma mwaka mmoja sababu certificate nasoma miaka miwilli naomba kujuzwa na hapo wakuu?
   
 10. Ben40

  Ben40 Senior Member

  #10
  Mar 16, 2013
  Joined: Apr 18, 2012
  Messages: 191
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Ndiyo dipl. ni mwaka 1.
   
 11. E

  Erick minde New Member

  #11
  Mar 18, 2013
  Joined: Mar 17, 2013
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  za asubuhii??vipi mimi nina c ya biology na nina pointi 29 ntapata nafasi??
   
 12. 3MMANUEL

  3MMANUEL Member

  #12
  Mar 25, 2013
  Joined: Nov 7, 2012
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jamani nina
  CHEM-C,
  BIOS-C
  MATH-D
  PHYS-D
  KWENYE TANGAZO HAPO JUU KUNA SHARTI MOJA LINANIBANA KU-APPLY KWASABABU WAMESEMA MWOMBAJI AWE AMEMALIZA KIDATO CHA NNE 2008 NA KUENDELEA NA MIMI NIMEMALIZA 2006 NAOMBA USHAURI NIJARIBU KUTUMA MAOMBI AU SIWEZI KUPATA NAFASI KABISA?
   
 13. R

  RAMA BINRAMA New Member

  #13
  Mar 26, 2013
  Joined: Jan 16, 2013
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mm naombeni msaada wa namna gani nitaweza kupata shule ya advance mkoa wa tanga EGM plz naombeni msaada. mda unazidi kwenda kwani sifahamu shule yoyote.
   
 14. THE GREAT CAMP

  THE GREAT CAMP JF-Expert Member

  #14
  Mar 26, 2013
  Joined: Jun 29, 2012
  Messages: 767
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  apply utapata
   
 15. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #15
  Mar 26, 2013
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 29,284
  Likes Received: 8,454
  Trophy Points: 280
  Hapa nimeona maruweruwe...
   
 16. CompaQ

  CompaQ JF-Expert Member

  #16
  Mar 26, 2013
  Joined: Dec 31, 2012
  Messages: 276
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 45
  acha uongo umeambiwa hiyo Diploma ni ya CBE?
  Hakuna kitu kama hicho!
  Ukiamua kwenda kusoma Diploma ni miaka mitatu!
  Ngazi ya certificate ni Miaka 2
  hata ukianza ngazi ya cheti ambayo ni miaka miwili kisha ukaamua kuendeleza diploma utasoma tena miaka mitatu!
   
 17. C

  Cambri Senior Member

  #17
  Mar 26, 2013
  Joined: Nov 9, 2012
  Messages: 142
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Unaweza kupata
   
 18. A

  Arteta_21 Member

  #18
  Mar 26, 2013
  Joined: Feb 25, 2013
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakuu kama una F ya math halafu PHY-D CHEM-C BIO-C na ENG-D halafu nika apply diploma in clinical officer naweza kuchaguliwa?
   
 19. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #19
  Mar 26, 2013
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,356
  Likes Received: 1,929
  Trophy Points: 280
  Hakuna chuo kizuri wala kibaya. Ni akili yako, bidii binafsi na utakavyojiuza sokoni. Ila kuna vyuo vya kifahari (prestigious)
   
 20. Kabodot

  Kabodot Member

  #20
  Apr 5, 2013
  Joined: Oct 8, 2012
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Kama niko kanda ya kati nikatuma kanda ya ziwa nivibaya?
   
Loading...