Wizara ya Afya tuondoleeni uchafu huu kwenye mabaa

dudus

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2011
Posts
24,856
Reaction score
56,841
Wadau;

Kuna tabia moja ni kama umeshazoeleka hususan kwenye mabaa. Kanuni za afya zinawataka wenye mabaa na migahawa kuwa na sink au chombo cha maji safi na sabuni kwa ajili ya wateja kunawa kabla na baada ya kula au baada ya kwenda haja.

Kutokana na utaratibu huo, mabaa mengi huweka ndoo za maji "safi" somewhere kwa ajili ya wateja kujinawia na kwa kawaida ndoo hizi zenye mfuniko huwa na koki so mteja anafungulia na kujinawia zake. Pamoja na ndoo, baa nyingi huwa na vyombo vingine kama mabirika, majagi, mabakuli, na vyombo (chupa za plastiki zilizotobolewa mifuniko) vya sabuni za maji kwa ajili ya wahudumu kumhudumia mteja pale alipo badala ya mteja kufuata ndoo.

Imekuwa desturi, wahudumu wakishamnawisha mteja, chombo cha sabuni hutupwa mle mle kwenye bakuli la maji machafu waliyokwisha nawia wateja. Pia birika au jagi la maji "safi" huwekwa humo humo ndani ya bakuli. Ikumbukwe chombo cha sabuni kina tundu hivyo ni rahisi uchafu walionawa wateja kuingia kwenye chombo cha sabuni!

Tabia zaidi ni kwamba maji "safi" yakiisha kwenye jagi au birika, jagi au birika hilo hilo ambalo limo ndani ya bakuli lenye maji machafu waliyoanawaia wateja husukumizwa ndani ya ndoo ya maji "safi" na kujazwa maji mengine! Ndoo moja inaweza kusukumizwa mabirika au majagi mengi yaliyonawisha wateja wengi na wenye uchafu wa kila aina!

Kwa wazoefu wa kupata huduma kwenye mabaa iwe huduma za vinywaji au vyakula hawatakuwa wageni na utaratibu huu ambao umerasimishwa huku mamlaka husika zikiwa zimelala! Hii kitu ni hatari sana kwa afya za wananchi! Kwa kutolea mfano, mlioko Dodoma nendeni kwenye zile baa maarufu kwa kuku na nyama choma mtakutana na tabia hii halafu wahusika hawana hata wasiwasi! Mambo ni hayo hayo kwenye mabaa na maeneo mengine yanayotoa huduma za vinywaji na vyakula!

Tabia nyingine, wahudumu wengi kama sio wote hawana desturi ya kunawa wanapotoka maliwatoni. Akikurupuka huko huyooo kaunta kumbebea mteja kinywaji, glass, na tishu! Ukimshtukia jibu ni rahisi tu "nimenawa mle chooni" wakati inaeleweka chooni kwenyewe maji hamna na hata yangekuwepo usafi mle ndani ni mdogo mno!

Mamlaka husika amkeni na timizeni wajibu wenu!
 
Wadau;

Kuna upumbavu mmoja ni kama umeshazoeleka hususan kwenye mabaa. Kanuni za afya zinawataka wenye mabaa na migahawa kuwa na sink au chombo cha maji safi na sabuni kwa ajili ya wateja kunawa kabla na baada ya kula au baada ya kwenda haja.

Kutokana na utaratibu huo, mabaa mengi huweka ndoo za maji "safi" somewhere kwa ajili ya wateja kujinawia na kwa kawaida ndoo hizi zenye mfuniko huwa na koki so mteja anafungulia na kujinawia zake. Pamoja na ndoo, baa nyingi huwa na vyombo vingine kama mabirika, majagi, mabakuli, na vyombo (chupa za plastiki zilizotobolewa mifuniko) vya sabuni za maji kwa ajili ya wahudumu kumhudumia mteja pale alipo badala ya mteja kufuata ndoo.

Imekuwa desturi, wahudumu wakishamnawisha mteja, chombo cha sabuni kibatupwa mle mle kwenye bakuli la maji machafu waliyokwisha nawia wateja. Pia birika au jagi la maji "safi" huwekwa humo humo ndani ya bakuli. Ikumbukwe chombo cha sabuni kina tundu hivyo ni rahisi uchafu walionawa wateja kuingia kwenye chombo cha sabuni!

Upumbavu zaidi ni kwamba maji "safi" yakiisha kwenye jagi au birika, jagi au birika hilo hilo ambalo limo ndani ya bakuli lenye maji machafu waliyoanawaia wateja husukumizwa ndani ya ndoo ya maji "safi" na kujazwa maji mengine! Ndoo moja inaweza kusukumizwa mabirika au majagi mengi yaliyonawisha wateja wengi na wenye uchafu wa kila aina!

Kwa wazoefu wa kupata huduma kwenye mabaa iwe za vinywaji au vyakula hawatakuwa wageni na utaratibu aka upumbavu huu ambao umerasimishwa huku mamlaka husika zikiwa zimelala! Hii kitu ni hatari sana kwa afya za wananchi! Jamani mamlaka husika amkeni na timizeni wajibu wenu! Kwa kutolea mfano, mlioko Dodoma nendeni kwenye zile baa maarufu kwa kuku na nyama choma mtakutana na ujinga huu halafu wahusika hawana hata wasiwasi!
Kingine kinachotia kinyaa hasa kwenye migahawa ni ile sehemu ya kunawia mikono halafu chini wametega ndoo ya kuyakinga yale maji machafu yanayotiririka. Unakuta ile ndoo iko wazi halafu maji machafu yaliyopo hayamwagwi kwa wakati,inachefua sana.
 
... halafu wanaojiita mabibi na mabwana afya wapo tu wanakula mishahara! Mamlaka husika zinatakiwa kutoa taratibu na miongozo na kufuatilia. Otherwise, tunalishwa uchafu sana kwenye migahawa na mabaa uswahilini huko.
 
Kingine kinachotia kinyaa hasa kwenye migahawa ni ile sehemu ya kunawia mikono halafu chini wametega ndoo ya kuyakinga yale maji machafu yanayotiririka. Unakuta ile ndoo iko wazi halafu maji machafu yaliyopo hayamwagwi kwa wakati,inachefua sana.
Ukimchunguza BATA.........
 
Wadau;

Kuna upumbavu mmoja ni kama umeshazoeleka hususan kwenye mabaa. Kanuni za afya zinawataka wenye mabaa na migahawa kuwa na sink au chombo cha maji safi na sabuni kwa ajili ya wateja kunawa kabla na baada ya kula au baada ya kwenda haja.

Kutokana na utaratibu huo, mabaa mengi huweka ndoo za maji "safi" somewhere kwa ajili ya wateja kujinawia na kwa kawaida ndoo hizi zenye mfuniko huwa na koki so mteja anafungulia na kujinawia zake. Pamoja na ndoo, baa nyingi huwa na vyombo vingine kama mabirika, majagi, mabakuli, na vyombo (chupa za plastiki zilizotobolewa mifuniko) vya sabuni za maji kwa ajili ya wahudumu kumhudumia mteja pale alipo badala ya mteja kufuata ndoo.

Imekuwa desturi, wahudumu wakishamnawisha mteja, chombo cha sabuni hutupwa mle mle kwenye bakuli la maji machafu waliyokwisha nawia wateja. Pia birika au jagi la maji "safi" huwekwa humo humo ndani ya bakuli. Ikumbukwe chombo cha sabuni kina tundu hivyo ni rahisi uchafu walionawa wateja kuingia kwenye chombo cha sabuni!

Upumbavu zaidi ni kwamba maji "safi" yakiisha kwenye jagi au birika, jagi au birika hilo hilo ambalo limo ndani ya bakuli lenye maji machafu waliyoanawaia wateja husukumizwa ndani ya ndoo ya maji "safi" na kujazwa maji mengine! Ndoo moja inaweza kusukumizwa mabirika au majagi mengi yaliyonawisha wateja wengi na wenye uchafu wa kila aina!

Kwa wazoefu wa kupata huduma kwenye mabaa iwe huduma za vinywaji au vyakula hawatakuwa wageni na utaratibu a.k.a upumbavu huu ambao umerasimishwa huku mamlaka husika zikiwa zimelala! Hii kitu ni hatari sana kwa afya za wananchi! Kwa kutolea mfano, mlioko Dodoma nendeni kwenye zile baa maarufu kwa kuku na nyama choma mtakutana na ujinga huu halafu wahusika hawana hata wasiwasi! Mambo ni hayo hayo kwenye mabaa na maeneo mengine yanayotoa huduma za vinywaji na vyakula!

Upumbavu mwingine, wahudumu wengi kama sio wote hawana desturi ya kunawa wanapotoka maliwatoni. Akikurupuka huko huyooo kaunta kumbebea mteja kinywaji, glass, tishu! Ukimshtukia jibu ni rahisi tu "nimenawa mle chooni" wakati inaeleweka chooni kwenyewe maji hamna na hata yangekuwepo usafi mle ndani ni mdogo mno!

Mamlaka husika amkeni na timizeni wajibu wenu!
Angalizo muhimu sana,hasa kipindi hiki cha mvua zenye upepo wa kisulisuli.
 
Wadau;

Kuna upumbavu mmoja ni kama umeshazoeleka hususan kwenye mabaa. Kanuni za afya zinawataka wenye mabaa na migahawa kuwa na sink au chombo cha maji safi na sabuni kwa ajili ya wateja kunawa kabla na baada ya kula au baada ya kwenda haja.

Kutokana na utaratibu huo, mabaa mengi huweka ndoo za maji "safi" somewhere kwa ajili ya wateja kujinawia na kwa kawaida ndoo hizi zenye mfuniko huwa na koki so mteja anafungulia na kujinawia zake. Pamoja na ndoo, baa nyingi huwa na vyombo vingine kama mabirika, majagi, mabakuli, na vyombo (chupa za plastiki zilizotobolewa mifuniko) vya sabuni za maji kwa ajili ya wahudumu kumhudumia mteja pale alipo badala ya mteja kufuata ndoo.

Imekuwa desturi, wahudumu wakishamnawisha mteja, chombo cha sabuni hutupwa mle mle kwenye bakuli la maji machafu waliyokwisha nawia wateja. Pia birika au jagi la maji "safi" huwekwa humo humo ndani ya bakuli. Ikumbukwe chombo cha sabuni kina tundu hivyo ni rahisi uchafu walionawa wateja kuingia kwenye chombo cha sabuni!

Upumbavu zaidi ni kwamba maji "safi" yakiisha kwenye jagi au birika, jagi au birika hilo hilo ambalo limo ndani ya bakuli lenye maji machafu waliyoanawaia wateja husukumizwa ndani ya ndoo ya maji "safi" na kujazwa maji mengine! Ndoo moja inaweza kusukumizwa mabirika au majagi mengi yaliyonawisha wateja wengi na wenye uchafu wa kila aina!

Kwa wazoefu wa kupata huduma kwenye mabaa iwe huduma za vinywaji au vyakula hawatakuwa wageni na utaratibu a.k.a upumbavu huu ambao umerasimishwa huku mamlaka husika zikiwa zimelala! Hii kitu ni hatari sana kwa afya za wananchi! Kwa kutolea mfano, mlioko Dodoma nendeni kwenye zile baa maarufu kwa kuku na nyama choma mtakutana na ujinga huu halafu wahusika hawana hata wasiwasi! Mambo ni hayo hayo kwenye mabaa na maeneo mengine yanayotoa huduma za vinywaji na vyakula!

Upumbavu mwingine, wahudumu wengi kama sio wote hawana desturi ya kunawa wanapotoka maliwatoni. Akikurupuka huko huyooo kaunta kumbebea mteja kinywaji, glass, na tishu! Ukimshtukia jibu ni rahisi tu "nimenawa mle chooni" wakati inaeleweka chooni kwenyewe maji hamna na hata yangekuwepo usafi mle ndani ni mdogo mno!

Mamlaka husika amkeni na timizeni wajibu wenu!
Waeleshe tuu, ikiwezekana pia nenda na kikombe chako unanywea ukishiba unaweka kwenye begi la laptop. Unaondoka.
 
Wale wanaoweka visabuni vya unga juu ya mfuniko. Mtu anagusa ananawa,,katok kupuu anagusa ananawa, unakuja kula unagusa
... bora vile vya unga kuliko za vipande. The best ni za maji ndani ya chupa japo handling yake ndio kama hivyo chupa muda wote iko ndani ya bakuli la maji machafu waliyonawia wateja.
 
Waeleshe tuu, ikiwezekana pia nenda na kikombe chako unanywea ukishiba unaweka kwenye begi la laptop. Unaondoka.
... kiongozi sometimes ni vigumu kutembea na kikombe au chombo binafsi kila mahali. La msingi ni kanuni za afya kuzingatiwa na mamlaka husika kufuatilia na kutoa adhabu kwa wahusika kukomesha huu ujinga. Mteja anapolipa hela yake ahakikishiwe usalama wa afya yake.
 
Wadau;

Kuna upumbavu mmoja ni kama umeshazoeleka hususan kwenye mabaa. Kanuni za afya zinawataka wenye mabaa na migahawa kuwa na sink au chombo cha maji safi na sabuni kwa ajili ya wateja kunawa kabla na baada ya kula au baada ya kwenda haja.

Kutokana na utaratibu huo, mabaa mengi huweka ndoo za maji "safi" somewhere kwa ajili ya wateja kujinawia na kwa kawaida ndoo hizi zenye mfuniko huwa na koki so mteja anafungulia na kujinawia zake. Pamoja na ndoo, baa nyingi huwa na vyombo vingine kama mabirika, majagi, mabakuli, na vyombo (chupa za plastiki zilizotobolewa mifuniko) vya sabuni za maji kwa ajili ya wahudumu kumhudumia mteja pale alipo badala ya mteja kufuata ndoo.

Imekuwa desturi, wahudumu wakishamnawisha mteja, chombo cha sabuni hutupwa mle mle kwenye bakuli la maji machafu waliyokwisha nawia wateja. Pia birika au jagi la maji "safi" huwekwa humo humo ndani ya bakuli. Ikumbukwe chombo cha sabuni kina tundu hivyo ni rahisi uchafu walionawa wateja kuingia kwenye chombo cha sabuni!

Upumbavu zaidi ni kwamba maji "safi" yakiisha kwenye jagi au birika, jagi au birika hilo hilo ambalo limo ndani ya bakuli lenye maji machafu waliyoanawaia wateja husukumizwa ndani ya ndoo ya maji "safi" na kujazwa maji mengine! Ndoo moja inaweza kusukumizwa mabirika au majagi mengi yaliyonawisha wateja wengi na wenye uchafu wa kila aina!

Kwa wazoefu wa kupata huduma kwenye mabaa iwe huduma za vinywaji au vyakula hawatakuwa wageni na utaratibu a.k.a upumbavu huu ambao umerasimishwa huku mamlaka husika zikiwa zimelala! Hii kitu ni hatari sana kwa afya za wananchi! Kwa kutolea mfano, mlioko Dodoma nendeni kwenye zile baa maarufu kwa kuku na nyama choma mtakutana na ujinga huu halafu wahusika hawana hata wasiwasi! Mambo ni hayo hayo kwenye mabaa na maeneo mengine yanayotoa huduma za vinywaji na vyakula!

Upumbavu mwingine, wahudumu wengi kama sio wote hawana desturi ya kunawa wanapotoka maliwatoni. Akikurupuka huko huyooo kaunta kumbebea mteja kinywaji, glass, na tishu! Ukimshtukia jibu ni rahisi tu "nimenawa mle chooni" wakati inaeleweka chooni kwenyewe maji hamna na hata yangekuwepo usafi mle ndani ni mdogo mno!

Mamlaka husika amkeni na timizeni wajibu wenu!

Kona Baa na Hongera Bar pale Sinza, huwa unakuta mhudumu katoka KUBADILI PEDI hanawi mikono, anakuletea tissue, ama anakupa bia yako na kuifuta futa, unaona vidamu kwenye kucha zake.

Nashauri watu wanyweee majumbani mwao na waume zao.
 
toa mifano ya maeneooo...SIDHANI KA NI WIZARA bali watendajii wale wanaoitwa "MABWANA AFYAAA."..huenda wamejisahauuuu..Zipo sehemu mingiii ukifika maji ya kunawa yamotooo, msalani kusafiii, wahudumu wamevaa vizuri, nk...naweza kukutajia maeneo machacheee......ila ni jambo muhimiuuuu
 
Kona Baa na Hongera Bar pale Sinza, huwa unakuta mhudumu katoka KUBADILI PEDI hanawi mikono, anakuletea tissue, ama anakupa bia yako na kuifuta futa, unaona vidamu kwenye kucha zake.

Nashauri watu wanyweee majumbani mwao na waume zao.
... duh! Hatari sana. Tena ikishafika usiku mnene ni balaa tupu! Tunalishwa mauchafu ya ajabu sana.
 
Back
Top Bottom