Wizara ya Afya tuondoleeni uchafu huu kwenye mabaa

toa mifano ya maeneooo...SIDHANI KA NI WIZARA bali watendajii wale wanaoitwa "MABWANA AFYAAA."..huenda wamejisahauuuu..Zipo sehemu mingiii ukifika maji ya kunawa yamotooo, msalani kusafiii, wahudumu wamevaa vizuri, nk...naweza kukutajia maeneo machacheee......ila ni jambo muhimiuuuu
... mifano nimetoa kwenye post yangu. Pia kuna mdau hapo juu katoa mfano pia. Kuhusu kwamba sio kazi ya wizara kimsingi post yangu ilisomeka "Idara za Afya ..." nashangaa mods wamerekebisha title ikasomeka wizara. Anyway, vyovyote iwavyo wizara nayo ni mdau muhimu.
 
Kwa wasiojuwa: tumieni dawa ya mswaki kusafisha mikono mkiwa baa. Colgate inasafisha sanaaa na kuondoa shombo yoteee Kuliko hizo sabuni zilizochakachuliwa.
 
Karaha za Dunia ya tatu hizo! Poleni ndugu zangu!
Kingine kinachotia kinyaa hasa kwenye migahawa ni ile sehemu ya kunawia mikono halafu chini wametega ndoo ya kuyakinga yale maji machafu yanayotiririka. Unakuta ile ndoo iko wazi halafu maji machafu yaliyopo hayamwagwi kwa wakati,inachefua sana.
 
Kwa wasiojuwa: tumieni dawa ya mswaki kusafisha mikono mkiwa baa. Colgate inasafisha sanaaa na kuondoa shombo yoteee Kuliko hizo sabuni zilizochakachuliwa.
... somo zuri japo ugumu ni kutembea na colgate kila uendapo baa au mgahawani!
 
Wadau;

Kuna upumbavu mmoja ni kama umeshazoeleka hususan kwenye mabaa. Kanuni za afya zinawataka wenye mabaa na migahawa kuwa na sink au chombo cha maji safi na sabuni kwa ajili ya wateja kunawa kabla na baada ya kula au baada ya kwenda haja.

Kutokana na utaratibu huo, mabaa mengi huweka ndoo za maji "safi" somewhere kwa ajili ya wateja kujinawia na kwa kawaida ndoo hizi zenye mfuniko huwa na koki so mteja anafungulia na kujinawia zake. Pamoja na ndoo, baa nyingi huwa na vyombo vingine kama mabirika, majagi, mabakuli, na vyombo (chupa za plastiki zilizotobolewa mifuniko) vya sabuni za maji kwa ajili ya wahudumu kumhudumia mteja pale alipo badala ya mteja kufuata ndoo.

Imekuwa desturi, wahudumu wakishamnawisha mteja, chombo cha sabuni hutupwa mle mle kwenye bakuli la maji machafu waliyokwisha nawia wateja. Pia birika au jagi la maji "safi" huwekwa humo humo ndani ya bakuli. Ikumbukwe chombo cha sabuni kina tundu hivyo ni rahisi uchafu walionawa wateja kuingia kwenye chombo cha sabuni!

Upumbavu zaidi ni kwamba maji "safi" yakiisha kwenye jagi au birika, jagi au birika hilo hilo ambalo limo ndani ya bakuli lenye maji machafu waliyoanawaia wateja husukumizwa ndani ya ndoo ya maji "safi" na kujazwa maji mengine! Ndoo moja inaweza kusukumizwa mabirika au majagi mengi yaliyonawisha wateja wengi na wenye uchafu wa kila aina!

Kwa wazoefu wa kupata huduma kwenye mabaa iwe huduma za vinywaji au vyakula hawatakuwa wageni na utaratibu a.k.a upumbavu huu ambao umerasimishwa huku mamlaka husika zikiwa zimelala! Hii kitu ni hatari sana kwa afya za wananchi! Kwa kutolea mfano, mlioko Dodoma nendeni kwenye zile baa maarufu kwa kuku na nyama choma mtakutana na ujinga huu halafu wahusika hawana hata wasiwasi! Mambo ni hayo hayo kwenye mabaa na maeneo mengine yanayotoa huduma za vinywaji na vyakula!

Upumbavu mwingine, wahudumu wengi kama sio wote hawana desturi ya kunawa wanapotoka maliwatoni. Akikurupuka huko huyooo kaunta kumbebea mteja kinywaji, glass, na tishu! Ukimshtukia jibu ni rahisi tu "nimenawa mle chooni" wakati inaeleweka chooni kwenyewe maji hamna na hata yangekuwepo usafi mle ndani ni mdogo mno!

Mamlaka husika amkeni na timizeni wajibu wenu!

Neno ' Upumbavu / Upopoma ' umelitumia sana katika Maelezo yako lakini katika Kusoma Kwako haya Malalamiko nami pia nimegundua ya kwamba huenda ' Upumbavu / Upopoma ' zaidi ukawa upande wako Wewe Mlalamikaji kwani hakuna aliyekulazimisha uende katika hizo Baa au hayo maeneo kwani kama kweli unataka Baa zenye Ustaarabu mbona zipo nyingi tu? Na ningekuona una Akili kama baada ya Kugundua kuwa hizo Baa hazina Usafi unaoutaka Wewe basi ungekuwa una Utaratibu wako wa kila unapotaka kwenda huko Baa basi unamwambia Mkeo awe anakuchemshia Maji ya Moto kisha anakuwekea katika Ndoo yako pamoja na Sabuni yako ya Kunawia na unakuwa unaibeba hiyo Ndoo katika Bichwa lako hilo Kubwa lenye ' Upumbavu / Upopoma ' mwingi na ukiwa hapo Baa basi unajinawisha tu mwenyewe kuliko kuwasambua Wahudumu wa Watu na kukimbilia Mitandaoni kulalamika wakati hata Wewe unaweza pia Kuchukua hatua ya kuwa Msafi uwapo katika Baa.
 
Duh! Sawa.
 
... duh! Hatari sana. Tena ikishafika usiku mnene ni balaa tupu! Tunalishwa mauchafu ya ajabu sana.
Mkuu katika mambo ya hygiene kwenye hizi Bara na hotel zetu ni Mungu tu anajua. Kuna vipengele vingi sana ambavyo hata akija mgeni kutoka nchi zilizoendelea anashangaa. Huwa najiuliza kwanini vyooni huwa wanaweka gudulia moja kuuubwa lwenye maji na kichoteo, eti ya maji ya kutawazia? Huu ni uchafu wa hali ya juu. Au wauza nyama eg kitimoto wanatumia visu/mapanga kukata nyama mbichi halafu inapoiva wanaikatakata tena kwa kutumia visu/mapanga yale yale bila kuosha. Na mikono ndiyo kabisaa hawaoshi. Kuna jamaa mmoja alifariki kwa kuambukizwa minyoo ya kiti moto kwenye ubongo dr akasema mara nyingi inatokana na wakataji kutozingatia usafi.
 
Wadau;

Kuna upumbavu mmoja ni kama umeshazoeleka hususan kwenye mabaa. Kanuni za afya zinawataka wenye mabaa na migahawa kuwa na sink au chombo cha maji safi na sabuni kwa ajili ya wateja kunawa kabla na baada ya kula au baada ya kwenda haja.

Kutokana na utaratibu huo, mabaa mengi huweka ndoo za maji "safi" somewhere kwa ajili ya wateja kujinawia na kwa kawaida ndoo hizi zenye mfuniko huwa na koki so mteja anafungulia na kujinawia zake. Pamoja na ndoo, baa nyingi huwa na vyombo vingine kama mabirika, majagi, mabakuli, na vyombo (chupa za plastiki zilizotobolewa mifuniko) vya sabuni za maji kwa ajili ya wahudumu kumhudumia mteja pale alipo badala ya mteja kufuata ndoo.

Imekuwa desturi, wahudumu wakishamnawisha mteja, chombo cha sabuni hutupwa mle mle kwenye bakuli la maji machafu waliyokwisha nawia wateja. Pia birika au jagi la maji "safi" huwekwa humo humo ndani ya bakuli. Ikumbukwe chombo cha sabuni kina tundu hivyo ni rahisi uchafu walionawa wateja kuingia kwenye chombo cha sabuni!

Upumbavu zaidi ni kwamba maji "safi" yakiisha kwenye jagi au birika, jagi au birika hilo hilo ambalo limo ndani ya bakuli lenye maji machafu waliyoanawaia wateja husukumizwa ndani ya ndoo ya maji "safi" na kujazwa maji mengine! Ndoo moja inaweza kusukumizwa mabirika au majagi mengi yaliyonawisha wateja wengi na wenye uchafu wa kila aina!

Kwa wazoefu wa kupata huduma kwenye mabaa iwe huduma za vinywaji au vyakula hawatakuwa wageni na utaratibu a.k.a upumbavu huu ambao umerasimishwa huku mamlaka husika zikiwa zimelala! Hii kitu ni hatari sana kwa afya za wananchi! Kwa kutolea mfano, mlioko Dodoma nendeni kwenye zile baa maarufu kwa kuku na nyama choma mtakutana na ujinga huu halafu wahusika hawana hata wasiwasi! Mambo ni hayo hayo kwenye mabaa na maeneo mengine yanayotoa huduma za vinywaji na vyakula!

Upumbavu mwingine, wahudumu wengi kama sio wote hawana desturi ya kunawa wanapotoka maliwatoni. Akikurupuka huko huyooo kaunta kumbebea mteja kinywaji, glass, na tishu! Ukimshtukia jibu ni rahisi tu "nimenawa mle chooni" wakati inaeleweka chooni kwenyewe maji hamna na hata yangekuwepo usafi mle ndani ni mdogo mno!

Mamlaka husika amkeni na timizeni wajibu wenu!
we kula kwa baba na mama yako..... bar ni pa kunywa pombe na acha kulalamika kifala.
 
Back
Top Bottom