Wizara ya Afya Tanzania
Official Account
- Oct 1, 2020
- 58
- 124
- Thread starter
- #61
Salaam Ntwale.Kwanini NHIF wanaendelea kuondoa baadhi ya DAWA? Shida ni nini ?
Tunashukuru sana kwa swali lako. Tunaomba utambue kuwa hakuna dawa iliyoondolewa katika huduma ya NHIF katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya katika ngazi zote. Niwaombe tu, ikitokea wewe au mwanachama yeyote amepata au kukutana na changamoto yoyote juu ya huduma zitolewazo na NHIF tunaomba sana awasiliane nasi tuweze kumsaidia.
Tafadhali sana, utupigie tu kwa namba 0800110063. Tumeboresha Afya Nchini, na kazi inaendelea kuwasogezea zaidi huduma wananchi karibu na maeneo yao wanayoishi.
Aksante.