MD25 usiwe mzushi, Dr Mtasiwa hakuwa mtu wa kumtegemea Luhanjo kwa sababu ya kuwa kabila moja au kutoka mkoa mmoja.
Kama unaugomvi naye useme. Kama umekurupuka basi waulize waliosoma naye au kufanyakazi naye toka akiwa Jiji watakueleza.
MAT walitoa maelezo tosha ni kwanini walimsimamisha Dr Mtasiwa uanachama kwa mwaka 1.
FYI, Dr Mtasiwa ni mhehe wa Iringa vijijini na Luhanjo ni mbena wa Njombe-Lupembe.
Mama Nyoni anahusika kwa asilimia mia moja, kwasababu yeye ndiye mtendaji mkuu wa wizara na idara zote ziko chini, hakuna pesa inayotoka bila idhini yake, hakuna mradi unaofanyika bila kupitia kwake, barua zote lazima zielekezwe kwake, nafikiri umetanguliza ushabiki kuliko uhalisia KAJIPANGE UPYA, kuchagua kumtetea huyo mama ni sawa na Kubeba mzigo wa "KINYESI".
Haya hembu kanusha madudu zaidi ya 30 haya hapa aliyoyafanya!! Halafu tuje kwa waatumishi wengine
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/221725-ufisadi-wa-blandina-nyoni-huu-hapa.html
MTM, nakubaliana nawe kuwa MoHSW kuna matatizo mengi mno. Hayo uliyataja ni baadhi tu. Kuna watu kwasababu ya kukusa sifa wamejitengenezea gamba. Members wa hilo gamba wanamlinda bosi wao hali wao wakila kupitia huyo gamba mkuu.
Unaweza kufikiria kuwa jambo hili kufumbiwa macho mf pesa inatumwa toka Hazina kupitia Wizarani kwenda Rukwa kwa ajili ya mradi wa macho. Ikifika huko inakatwa kama 30-40% na kurudishwa kwenye akaunti binafsi ya mheshimiwa fulani wa wizarani. Yeye atajua watakavyo gawana na wenzake. Mchezo huo unafanywa sana katika vertical projects/programmes.
Kwa ufupi, ikitokea scandal Wizara ya Afya mara nyingi wadogo hutolewa kafara na wakubwa kupeta.
Mama Nyon alikuwa anasukumiza mikono ya vipofu kila vipofu wanapotaka kumega tonge wakati huo huo vipofu wanamsikia nyam nyam nyam zake anapokula. Manung'uniko yakaanza. Kipofu aliyependwa aliruhusiwa kula.
Rudia tena.kusoma............wapi nimemtetea mama Nyoni..........?..........................Yeye ana mabaya yake narudia tena..............lakaini kama alivyosema MTM .............na tuitumie hii nafasi kumwomba Mh. Rais , asiishie hapo tu maadam kaaamua kulivalia njuga hili swala ....afagie na hizi takataka zilizoji ficha upenuni mwa nyumba asiishie na zile kule uwanjani zinazoonekana na kila mtu!
Luhanjo Iringa ?, Nyoni Iringa/Songea? Dr Mtasiwa Iringa?
Hivi Dr Mtasiwa alimaliza Intern lini? alitibia wapi na wapi or alifikaje fikaje pale na kuukwaa u CM-D??
Umeiweka mwakeMTM, nakubaliana nawe kuwa MoHSW kuna matatizo mengi mno. Hayo uliyataja ni baadhi tu. Kuna watu kwasababu ya kukusa sifa wamejitengenezea gamba. Members wa hilo gamba wanamlinda bosi wao hali wao wakila kupitia huyo gamba mkuu.
Unaweza kufikiria kuwa jambo hili kufumbiwa macho mf pesa inatumwa toka Hazina kupitia Wizarani kwenda Rukwa kwa ajili ya mradi wa macho. Ikifika huko inakatwa kama 30-40% na kurudishwa kwenye akaunti binafsi ya mheshimiwa fulani wa wizarani. Yeye atajua watakavyo gawana na wenzake. Mchezo huo unafanywa sana katika vertical projects/programmes.
Kwa ufupi, ikitokea scandal Wizara ya Afya mara nyingi wadogo hutolewa kafara na wakubwa kupeta.
Mama Nyon alikuwa anasukumiza mikono ya vipofu kila vipofu wanapotaka kumega tonge wakati huo huo vipofu wanamsikia nyam nyam nyam zake anapokula. Manung'uniko yakaanza. Kipofu aliyependwa aliruhusiwa kula.
We Asprin unataka niliwe nyama mbichi hapa eh! Zaidi ya makoti meupe na kile kijichuma wakivaacho Madk sina lolote nlijualo.
Huhitaji digrii kusoma mawazo yako, ni wazi umekelekwa na kushughulikiwa kwa huyo mama na hii inakuweka kwenye kundi la utetezi zaidi. Nafikiri wewe ndo ungepitia upya post yako, naposema unataka kutofautiana na wengine kuhusu mama nyoni na kuelekeza lawama kwa watendaji wengi ukidai ukionyesha wazi kuwa kilichofanyika ni baadhi ya watendaji wake kutumia udhaifu wa mgomo huu kummaliza. Samahani pengine sijui kiswahili vizuri ila nahisi hii kama kauli ya utetezi..:A S-confused1:
Bahati mbaya siwezi zuia kutafsiriwa visivyo..........na hii post yako imeonesha hilo.........umepatia nimekerwa na kitu kimmoja...........Blandina nyoni ni papa miongoni mwa mapapa wengine.........nimekerwa kwa kutoona hao wengine kutoshughulikiwa kwenye hili.........
Usiwe na matumaini makubwa na huyo rais, yeye aliwekwa madarakani na wanamtandao ambao kwa sasa ndio wanaoiongoza serikali, na kwahiyo utatuzi wa MoH utategemea nani member wa mtandao ili alindwe na nani sio member ili atoswe, natusubiri tuone.Rudia tena.kusoma............wapi nimemtetea mama Nyoni..........?..........................Yeye ana mabaya yake narudia tena..............lakaini kama alivyosema MTM .............na tuitumie hii nafasi kumwomba Mh. Rais , asiishie hapo tu maadam kaaamua kulivalia njuga hili swala ....afagie na hizi takataka zilizoji
ficha upenuni mwa nyumba asiishie na zile kule uwanjani zinazoonekana na kila mtu!
Usiwe na matumaini makubwa na huyo rais, yeye aliwekwa madarakani na wanamtandao ambao kwa sasa ndio wanaoiongoza serikali, na kwahiyo utatuzi wa MoH utategemea nani member wa mtandao ili alindwe na nani sio member ili atoswe, natusubiri tuone.
Tuanze na kujiuliza Blandina amehamia lini MoHSW na matatizo ya madaktari yameanza lini?
Utakua umetumwa wewe mbayuwayu!
Kwani ni nani alitaka huyo bi kidude nyoni atoke hapo wizarani? Madaktari au hao watumishi wa kwenye hizo idara?
Mwambie ajiandae kupanda karandinga yeye na mhehe mwenzake Dr Mtasiwa.
Si walikuwa wanamtegemea Godfather wao Luanjo, now inakula kwao sasa.