Wizara ya Afya...SHAME ON YOU! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wizara ya Afya...SHAME ON YOU!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Masikini_Jeuri, Feb 11, 2012.

 1. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #1
  Feb 11, 2012
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Nitakwenda kinyume na wengi..............mtiriiriko wa yaliyojiri hivi karibuni katika Wizara hii pamoja na mgomo wa Madaktari...........ni matokeo ya uozo na mbinu chafu zilizokuwa zikiendelea wizarani hapo kwa muda mrefu.............!

  Blandina Nyoni ana mapungufu yake lakini pia kwa sehemu kubwa watumishi wa wizari hii hasa hapo makao makuu mnabeba nusu ya lawama za mabaya ambayo yamepelekea matatizo lukuki kwenye wizara hii nyeti.

  Simtetei Mama Nyoni lakini niseme ukweli kuwa hapa ametumika (si kama kondoo wa kafar kwa sababu naye ana makosa yake kama pia kwenye hili) tofauti na Dr Mtasiwa ambaye mie namuona kama ni kondoo wa kafara kwenye hili..............watumishi wa makao makuu hasa wale kwenye maidara nani aisyejua mmekuwa mkiwanyanyasa madaktari wetu hasa wanapodai haki zao msingi kwa miongo mingi tu hata kabla ya mama Nyoni kuwepo hapo?

  Nani asiyejua kuwa ninyi mmemkuwa kikwazo kwa kuwanyima na kuwaibia stahiki zao? Nani asiyejua kuwa mmesabisha hadi baadhi ya madaktari bingwa kuondoka serikalini na hata wengine kuikimbia nchi na kwenda kufanya kazi nje kwa dhuluma zenu? Nani asiyejua mmekua mkitoa nafasi za masomo kwa upendeleo na hata wakati mwingine kwa rushwa ilhali ninyi hasa msiokuwa madaktari mmekuwa mkijipa nafasi na malipo mbalimbali bila hata ya aibu? Nani asiyejua kua ninyi ndio haswa chanzo cha madaktari wetu kuichukia wizara yao wenyewe, wizara iliyopaswa kuangalia mambo yao na hatimaye kugoma? kero nyingi za madaktari zilipaswa kutatuliwa na nyie.....hebu tuambieni mlichukua hatua gani zilizokuwa chini ya uwezo wenu?

  Msibaki kumtupia kila lawama Blandina Nyoni................na hili nalisema alipokuja hapo alizima mbinu zenu chafu za kuiiibia serikali na umma semeni na hilo pia..........pamoja na mbaya yake lakini aliweza kuwadhibiti na hivyo niko sahihi nikisema mmelitumia hili tatizo kuhakikisha mnmaliza .......sawa nyie wenyewe wasafi...............

  Blandina Nyoni hakuwa anawaslinaina na kila Daktari moja kwa moja ni nyie hapo makao makuu kupitia idara zenu...........kama ni kusimamishwa kazi.............wote mnastahili mpigwe chini kabisa................muondoke kwenye himaya mlizojijengea hapo wizarani.................

  Wanafiki wakubwa..................kama ni kushangilia kuondolewa Blandina Nyoni washangilie madaktari lakini sio ninyi hapo wizarani.....
   
 2. k

  kalakata Member

  #2
  Feb 11, 2012
  Joined: Dec 1, 2011
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Eeh hayo nayo kumbe yapo nyuma ya pazia! Kwel hii wizara ni muhimu iangaliwe kwa jicho la pili tusiishie kwahayo tu aliyoapiza waziri mkuu
   
 3. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #3
  Feb 11, 2012
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Duh! Tuhuma nzito hizo M_J. Ngoja nao waje wajitetee!
   
 4. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #4
  Feb 11, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Utakua umetumwa wewe mbayuwayu!
  Kwani ni nani alitaka huyo bi kidude nyoni atoke hapo wizarani? Madaktari au hao watumishi wa kwenye hizo idara?
  Mwambie ajiandae kupanda karandinga yeye na mhehe mwenzake Dr Mtasiwa.
  Si walikuwa wanamtegemea Godfather wao Luanjo, now inakula kwao sasa.
   
 5. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #5
  Feb 11, 2012
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,951
  Likes Received: 23,830
  Trophy Points: 280
  Habari za asubuhi?
  We uko wizara ya Afya, hebu tuambie hizi tuhuma ni za kweli?
   
 6. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #6
  Feb 11, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Siyo wao tu serikali ya jk na jk mwenyewe hawana aibu mbele ya wananchi
   
 7. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #7
  Feb 11, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Kuna ukweli mkubwa hapo kwa m_j.... Lakini mama nyoni alikua papa wapo
   
 8. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #8
  Feb 11, 2012
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Na waje nitawapa na vielelezo!

  MD25.......kwanza acha kukashifu kwa kuwaita watu majina..........huko ni kuishiwa sera; so watendaji wote waliopo serikalini wenye asili ya Iringa wamekuwa hapo kwa sababu ya Luhanjo?...........bahati nzuri umelitumia hili neno "Mbayuwayu"............linakufaa sana!
   
 9. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #9
  Feb 11, 2012
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  MD25 usiwe mzushi, Dr Mtasiwa hakuwa mtu wa kumtegemea Luhanjo kwa sababu ya kuwa kabila moja au kutoka mkoa mmoja.

  Kama unaugomvi naye useme. Kama umekurupuka basi waulize waliosoma naye au kufanyakazi naye toka akiwa Jiji watakueleza.

  MAT walitoa maelezo tosha ni kwanini walimsimamisha Dr Mtasiwa uanachama kwa mwaka 1.

  FYI, Dr Mtasiwa ni mhehe wa Iringa vijijini na Luhanjo ni mbena wa Njombe-Lupembe.
   
 10. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #10
  Feb 11, 2012
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Maskini Jeuri, wewe unaonyesha kuwa kibaraka wa Mama Nyoni. Huna ushahidi wa tuhuma zako. Ni kweli MoHSW kuna madudu ya miaka mingi lakini si kama unavyoeleza.

  Wewe unaeleza kwasababu umenyang'anywa kitumbua ama unayempenda kanyang'anywa kitumbua. Acha hizo. Utaumbuka.
   
 11. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #11
  Feb 11, 2012
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  We Asprin unataka niliwe nyama mbichi hapa eh! Zaidi ya makoti meupe na kile kijichuma wakivaacho Madk sina lolote nlijualo.
   
 12. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #12
  Feb 11, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  mNYAMAHODZO... LABDA TUWE MODERATE KIDOGO TU (INGAWA MIMI MWENYEWE NI EXTREMIST WHEN IT COMES TO HEALTH PROFESSIONALS RIGHTS)...
  1. Tuna matatizo pale wizarani kuanzia scholarships, kupotea kwa files, postings na abuse of power ya wakuu wa baadhi ya idara
  2. tuna shida kubwa sana finance na procurement
  3. Ila Mama Nyoni crossed all the borders beyond repair
  4. Hivi mnakumbuka murders zilizotembea pale? kashfa ya vitendanishi?, expiries?, songombingo za ARV regimes?, kasheshe za vocha za neti, ukosefu wa dawa za TB, hali ya diagnostics nk?

  Lets use this opportunity kusafisha wizara na hata wale wanharibifu waliobaki basi wajirekebishe au nao waondoke
   
 13. kaburungu

  kaburungu JF-Expert Member

  #13
  Feb 11, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 1,601
  Likes Received: 2,458
  Trophy Points: 280
  Hivi huwa mnakuwa wapi kuelezea tuhuma na utendaji mbovu wa wizara mpaka maji yanafika shingoni? Nauliza mko wapi, yaani mpaka nyoni na matasiwa wasimamishwe ndipo tuhuma wizarani zifumuliwe. Huu ni unafiki na kamwe unafiki huwa haujengi..
   
 14. Dotto Athumani

  Dotto Athumani Senior Member

  #14
  Feb 11, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 106
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mama Nyoni anahusika kwa asilimia mia moja, kwasababu yeye ndiye mtendaji mkuu wa wizara na idara zote ziko chini, hakuna pesa inayotoka bila idhini yake, hakuna mradi unaofanyika bila kupitia kwake, barua zote lazima zielekezwe kwake, nafikiri umetanguliza ushabiki kuliko uhalisia KAJIPANGE UPYA, kuchagua kumtetea huyo mama ni sawa na Kubeba mzigo wa "KINYESI".
   
 15. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #15
  Feb 11, 2012
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,922
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
 16. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #16
  Feb 11, 2012
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Hommie!

  Unatumia kipimo gani kushusha ukubwa wa tatizo hili tokea enzi?.............wacha kutuletea hadithi za dhambi ndogo ndogo na kubwa kubwa .....................DHAMBI NI DHAMBI...............huo udogo wauona weye lakini waweza kuwa mkubwa sana kwa aliyetendewa.................hebu fikiria kwa mfano Baba yangu alikataliwa nafasi ya masomo enzi zile zalate Dr. chiduo.............piga picha ya athari zake kwa taaluma yake, kwa watanzania na kwake binafsi!

  Nimeathirika na hili kama watz wengine
  Rudia tena maandishi yangu...........simsafishi Mama Nyoni.................lakini mnapaswa wote mmugane naye kwenye hili fagio!
   
 17. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #17
  Feb 11, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  iwe isiwe, Mama Nyoni was a super mole in the ministry, ni kansa mbaya sana
   
 18. Mtafiti1

  Mtafiti1 JF-Expert Member

  #18
  Feb 11, 2012
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 264
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  umeona eeehhh?
  wengine wameona bora kutopractice na kuingia fani nyingine!
   
 19. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #19
  Feb 11, 2012
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Maskini jeuri unaonekana ni maskini wa mawazo. Kumtetea Blandina Nyoni inakubidi uazime akili za mwenda wazimu. Lakini kwa mtu mwenye akili zako huwezi. Amewa victimize watendaji wengi kwa ajili ya kujisafishia ufisadi. Tunasubiri tume ianze kazi ndiyo tumamwage ushahidi. Blandina lazima akanyee debe segerea
   
 20. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #20
  Feb 11, 2012
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  MTM, nakubaliana nawe kuwa MoHSW kuna matatizo mengi mno. Hayo uliyataja ni baadhi tu. Kuna watu kwasababu ya kukusa sifa wamejitengenezea gamba. Members wa hilo gamba wanamlinda bosi wao hali wao wakila kupitia huyo gamba mkuu.

  Unaweza kufikiria kuwa jambo hili kufumbiwa macho mf pesa inatumwa toka Hazina kupitia Wizarani kwenda Rukwa kwa ajili ya mradi wa macho. Ikifika huko inakatwa kama 30-40% na kurudishwa kwenye akaunti binafsi ya mheshimiwa fulani wa wizarani. Yeye atajua watakavyo gawana na wenzake. Mchezo huo unafanywa sana katika vertical projects/programmes.

  Kwa ufupi, ikitokea scandal Wizara ya Afya mara nyingi wadogo hutolewa kafara na wakubwa kupeta.

  Mama Nyon alikuwa anasukumiza mikono ya vipofu kila vipofu wanapotaka kumega tonge wakati huo huo vipofu wanamsikia nyam nyam nyam zake anapokula. Manung'uniko yakaanza. Kipofu aliyependwa aliruhusiwa kula.
   
Loading...