mlinzi mlalafofofo
JF-Expert Member
- Apr 20, 2008
- 279
- 551
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amewataka Watanzania kuzingatia mtindo bora wa maisha ikiwemo kufanya mazoezi na kwamba wasifanye mzaha na ushauri unaotolewa na wataalamu wa Afya akiwemo Dkt. Janabi, kwani hata zikijengwa hospitali 100 kama Saifee bila kubadili mtindo wa maisha hazitatosha.
Ummy, ameyasema hayo eo Februari 18, 2024, kwenye uzinduzi wa Hospitali ya Saifee, iliyopo Jijini Dar es Salaam, iliyozinduliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa.
“Hata kama tutajenga hospitali 100 kama hizi za Saifee tusipobadili mtindo wetu wa maisha hospitali hazitatosha tusifanye mzaha na ushauri tunaopata kutoka kwa wataalamu wa Afya akiwemo Dkt. Janabi.” Alisema Waziri Ummy.
Sosi: Itv insta