Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,445
- 3,403
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro amesema kuwa Serikali haiwezi kuchukua jukumu la kuwaondoa Watanzania walioko nchini China kwa kusikiliza ushauri wa mitandaoni, bali itawaondoa endapo wataalamu kutoka Serikali ya China watashauri hivyo.
Dkt. Ndumbaro ameyabainisha hayo baada ya kuonekana video fupi inayoonesha Watanzania waishio nchini China, wakiomba kurejeshwa nyumbani kutokana na hali ya maambukizi na vifo vinavyotokana na Virusi vya Corona kuongezeka kila uchwao nchini humo.
"Huu ni ugonjwa na hili ni suala la kitabibu hivyo ni vizuri kupata ushauri wa kitabibu, kwamba imefika wakati sasa hawa lazima waondolewe, sasa hivi tunasikia ushauri wa mitandaoni hapana. Tukae na wataalamu wa Serikali ya China na waseme sasa hapa ni lazima kuwaondoa" amesema Dkt. Damas Ndumbaro.
Unaweza pia kusoma; Hali ya usalama kwa wanafunzi/ Watanzania waishio Wuhan nchini Uchina ipo matatani, waiomba Serikali iwarudishe nchini