Wizara Mambo ya Nje: Tutawaondoa Watanzania waliopo China iwapo Wataalamu wa Serikali ya China watashauri hivyo

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,438
3,333
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro amesema kuwa Serikali haiwezi kuchukua jukumu la kuwaondoa Watanzania walioko nchini China kwa kusikiliza ushauri wa mitandaoni, bali itawaondoa endapo wataalamu kutoka Serikali ya China watashauri hivyo.

Dkt. Ndumbaro ameyabainisha hayo baada ya kuonekana video fupi inayoonesha Watanzania waishio nchini China, wakiomba kurejeshwa nyumbani kutokana na hali ya maambukizi na vifo vinavyotokana na Virusi vya Corona kuongezeka kila uchwao nchini humo.

"Huu ni ugonjwa na hili ni suala la kitabibu hivyo ni vizuri kupata ushauri wa kitabibu, kwamba imefika wakati sasa hawa lazima waondolewe, sasa hivi tunasikia ushauri wa mitandaoni hapana. Tukae na wataalamu wa Serikali ya China na waseme sasa hapa ni lazima kuwaondoa" amesema Dkt. Damas Ndumbaro.

Unaweza pia kusoma; Hali ya usalama kwa wanafunzi/ Watanzania waishio Wuhan nchini Uchina ipo matatani, waiomba Serikali iwarudishe nchini
 
Jamani wabaki uko adi itakapotatuliwa, sipati picha watakapoleta maambukizi uku na hatuna uwezo wa kujenga hospitali ya kuwahudumia...
 
Huyo aliyetoa ushauri mtandaoni nani kuwa warudi?,wabakie hukohuko wasije tuletea tabu kwa kariakoo yetu tunavyoijua tutaisha,tunawapenda ila wabakie huko kwanza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanzania haina wataalam hadi tusubiri waChina? Na pia, sisi si ndio inabidi tuwaombe ushauri, au tunasubiri watupe from nowhere?
 
Looh, hatarrrrrr!!!
20200212_101850.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Walitakiwa warudishwe mapema tu kabla mambo hayajafika hapa.
Kwasasa ni kutoana kafara tu
 
Ukisikia hawa watu wanavyoongea unaweza ukahisi ni watu wenye uwezo fulani wa kiuchumi kumbe ni takataka tu
 
Jamani wabaki uko adi itakapotatuliwa, sipati picha watakapoleta maambukizi uku na hatuna uwezo wa kujenga hospitali ya kuwahudumia...
Kama tunajenga SGR kwa pesa za ndani tutashindwa vipi kujenga hospital ya ku deal na corona virus
 
Ukisikia hawa watu wanavyoongea unaweza ukahisi ni watu wenye uwezo fulani wa kiuchumi kumbe ni takataka tu
Naibu Waziri hili Jambo unaonyesha unataniana nalo au unalichukulia kisiasa zaidi.ilitakiwa hadi muda huu uwe umekwisha wasiluana na hao wataalamu wa kitabibu wa kichinaujue hatuaza kuchukuliwa hata Kama waliopo wuhani ni watanzania wawili bado ni watanzania wenzetu.
Pili tunasikia hata baloziwa Tanzania nchini china hayuko china alikwisha ondoka huko siku nyingi hivyo watanzania hawajui waongelee wapi Wala waende wapi ndiyo sababu wanatumia mitandao ya kijamii kumpeleka ujumbe .
Tatu, nchi ya Ghana umetuma fedha kuwasaidia waghana waliojifungia ndani kujilinda kuugua,he ukiwa Naibu waziri wa Mambo yanje umeshindwa kuishsuri serikali hata itume Dola 100 tu kuwasaidia wanafunzi hao kupata mlo wa siku?
Mwisho,tambua kuwa akija mtanzania mmoja mgonjwa kutoka china hapa nchini ataambukiza watanzania 55 million ,dawa hatuna,kinga hatuijui,wataalamu hatuna Bora kuwasaidia hao wachache wakiwa huko china ,wakija Tanzania wakiwa wagonjwa kitakuwa Kiama kwa nchi nzima.
 
Tulichogundua ni kwamba,Naibu Waziri wa mambo ya nje,hajui,Hana data za idadi ya wanafunzi wa kitanzania waliopo Wuhan, Hana idadi ya wanafunzi wa kitanzania wanaosoma china,hajui huko china wanaoma vyuo gani hivyo hata serikali ikimwambia Sasa walioko china wakaondolewe hajui atawakuta wapi na wangapi.hadakama nu watanzania kuwachangia wanafunzi hao hajui wako wapi,wako wangapi na wapelekewe akina Nani huo msaada na kiasi gani.
ni muhimu serikali kupata takwimu hizo. Mwisho ninashauri waziri kuitembelea china kwenda kuwaona na kuwasikiliza hao wanafunzi wa kitanzania walioko huko na kuiangalia namna ya kuwasaidia au kuwaokoa.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro amesema kuwa Serikali haiwezi kuchukua jukumu la kuwaondoa Watanzania walioko nchini China kwa kusikiliza ushauri wa mitandaoni, bali itawaondoa endapo wataalamu kutoka Serikali ya China watashauri hivyo.

Dkt. Ndumbaro ameyabainisha hayo baada ya kuonekana video fupi inayoonesha Watanzania waishio nchini China, wakiomba kurejeshwa nyumbani kutokana na hali ya maambukizi na vifo vinavyotokana na Virusi vya Corona kuongezeka kila uchwao nchini humo.

"Huu ni ugonjwa na hili ni suala la kitabibu hivyo ni vizuri kupata ushauri wa kitabibu, kwamba imefika wakati sasa hawa lazima waondolewe, sasa hivi tunasikia ushauri wa mitandaoni hapana. Tukae na wataalamu wa Serikali ya China na waseme sasa hapa ni lazima kuwaondoa" amesema Dkt. Damas Ndumbaro.

Unaweza pia kusoma; Hali ya usalama kwa wanafunzi/ Watanzania waishio Wuhan nchini Uchina ipo matatani, waiomba Serikali iwarudishe nchini
 
Mimi na ndugu China anasoma ila sikubaliani kabisa tena kabisa kuwrudisha ni bora wapewe hata jengo LA ubarozi huko wakae serikali iwahudumie, tusiwaige wenzetu wa ulaya wanaowarudisha ndugu zao sana uchumi mzuri ,wataalam na vifaa vya kisasa ,sisi marelia tu kila siku tunkufa ikija corona wallah tutakufa kama kuku serikli kaza hapo hapo hakuna kurudi MTU hapa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naibu Waziri hili Jambo unaonyesha unataniana nalo au unalichukulia kisiasa zaidi.ilitakiwa hadi muda huu uwe umekwisha wasiluana na hao wataalamu wa kitabibu wa kichinaujue hatuaza kuchukuliwa hata Kama waliopo wuhani ni watanzania wawili bado ni watanzania wenzetu.
Pili tunasikia hata baloziwa Tanzania nchini china hayuko china alikwisha ondoka huko siku nyingi hivyo watanzania hawajui waongelee wapi Wala waende wapi ndiyo sababu wanatumia mitandao ya kijamii kumpeleka ujumbe .
Tatu, nchi ya Ghana umetuma fedha kuwasaidia waghana waliojifungia ndani kujilinda kuugua,he ukiwa Naibu waziri wa Mambo yanje umeshindwa kuishsuri serikali hata itume Dola 100 tu kuwasaidia wanafunzi hao kupata mlo wa siku?
Mwisho,tambua kuwa akija mtanzania mmoja mgonjwa kutoka china hapa nchini ataambukiza watanzania 55 million ,dawa hatuna,kinga hatuijui,wataalamu hatuna Bora kuwasaidia hao wachache wakiwa huko china ,wakija Tanzania wakiwa wagonjwa kitakuwa Kiama kwa nchi nzima.
NW hamnazo
 
Huyo aliyetoa ushauri mtandaoni nani kuwa warudi?,wabakie hukohuko wasije tuletea tabu kwa kariakoo yetu tunavyoijua tutaisha,tunawapenda ila wabakie huko kwanza.

Sent using Jamii Forums mobile app
Muelezee huyo,mzee anasema tu, mtandao asiudharau ! mitandaoni kuuna vyoote! yaani;
1.Negative,
2.Neutral na
3.Postive,

Aulizie au atizame picha ya Tunisia, Libya, Area 52 nk atajua mitandaoni siyo!

Kwa muktadha huo chochote utakacho amua wewe kama kiongozi Tayari Makundi kwa Makundi yamesha amua kimtandao! na kujadili kwa mapana, na marefu. Bado utaufuata tu uamuzi wa mitandaoni, cha muhimu na yeye ajiunge .

Mfano ukiwaleta home ni ushauri wa mitandaoni tu, ukiwaacha ni ushauri wa mitandaoni pia, kama relis alivo shauri. hapa bora anyamaze tu kama Jiwe!

kwanza waje kufanya nini, Dege la free, chakula na dawa za bure hatuna, njooni mfe!... au wanazuga tu hawataki kuja bana, Waswahili?!!! yaani China ile nayoijua ya MAO TSE TUNG utoke?? kurudi Bongo?.au mko mazogoroni?
China kwenye AC inayonyunyiza nchi nzima kimya kimya, na Lami za ukoka mpaka mlangoni? misosi bure kambini?

So uje hapo naniliu Gongo la Mboto!! tena ya Magufuli kweli??? mtachakaaa! mpaka mlie poo! wasizuge hao wanaomba kimoyomoyo tu, kaugonjwa hako kaendelee kuua, kupunguza idadi, waweza pata kazi na kuziba mapengo ya marehemu!

Bora watakao baki DSM kidogo, lkn wanafunzi wanao toka mikoani? mfano Mtwara- kuree Mahurunga kwa Father Edfoncy tena bila cheti mnafurahia nini kule? mnajinafikisha Home is best?

wachina wanajua kwenu dhiki! mkijishebedua sana watawarudisha kwenu, na hamrudi tena wanachukua wanafunzi wapya! dawa ni nyie pigeni kimya wawasahau!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom