Wizara, kiwanda vyawaka moto Dar

Mgoyangi

Senior Member
Feb 6, 2008
184
9
Usikuwa kuamkia leo, katika matukio mawili tofauti lakini ambayo yanaonekana kutokea kwa wakati mmoja, Jengo la Wizara ya Mali Asili na Utalii na Kiwanda cha Bakheresa vimewaka moto.

Katika jengo la Wizara hiyo Nyaraka katika ofisi ya Katibu Mkuu zimeteketea kwa moto huo ambao hata hivyo haijafahamika ulitokana na nini, ingawaje sababu rahisi tutakayoambiwa baada ya siku mbili tatu ni funika kombe mwanaharamu apite - hitilafu ya umeme.

Pia jengo la Kiwanda cha Bakheresa nacho kimeungua na moto ulianzia katika stoo ya chakula.

Mioto hii, ilizimwa majira ya saa nane usiku, kwa mujibu wa habari za hivi punde kutoka Star TV.

Hasara na vyanzo bado havijafahamika.
 
Last edited by a moderator:
Kuna nyaraka nyingine zina dhamani kama pesa kama kunahistoria ya nyaraka muhimu kuungua itabidi wawe wanaweka kwenye ma safe.La sivyo tutakuwa hatu waelewi kwa chanja ya nyani kula indi bichi.
 
We Hujawa hi kisikia watu wanaunguza Ofisi fulani ili waweze kuunguza Nyaraka ili kupoteza Ushahidi
 
Huu ni aina ya ufisadi; wanaunguza nyaraka ili kuficha madudu yao, si juzii tu hawa makatibu wakuu wamebadilishwa akiwemo wa wizara iliyoungua!! Hapo lipo jambo sio bure.
 
Back
Top Bottom