Wivu unanimaliza!

Mkuu tatizo dogo sana hilo, hata mimi nilikuwa nalo lakini baadaye liliisha, cha msingi fanya hivi.

Kipindi akiwa anatoka na marafiki zake, paka pilipili machoni itakusaidia kutokufikiria mabaya juu yake na badala yake utakuwa busy kusikilizia utamu jichoni, maumivu yakiisha atakuwa kasharudi.

NB: Maumivu ya macho hayauwi, ila ya moyo yatakuua.
 
Wivu kwa umpendae ni jambo la kawaida,bt usizidi kipimo....insecurity is not attractive at all.....atavumilia lakin mwishoe atachoka,so badilika,ur the man,MWANAUME KUJIAMINI.
 
Ha ha ha huyo nouma
 
Yani hii thread lazima nimuoneshe mwafulani, maake na yeye kwa wivu nahisi stroke itampata soon

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Wivu nlikuwa nao ila baada ya kutendwa sijali tena. No wivu anymore.
 
How old are you labda tuanzie hapo??
 
hahah huu wivu au ugonjwa. Wewe tafuta demu mwingine wivu utapungua wenyewe tu. Ila acha kuendekeza uzinzi.
 
pole mkuu, mi naona kwanza kwa mapenz ya sasa utaja kufa kabla ya wakati, hebu fikir cku moja ukigundua ana m2, hebu ishi nae kwa uhuru kwamba cc ni binadam any thing my happen,
 
Aisee mtu anampigia simu mtu wako usiku halafu unataka ujifunze kuzivumilia simu za kutakiana usiku mwema?

Mwe.......!
 
Yani hii thread lazima nimuoneshe mwafulani, maake na yeye kwa wivu nahisi stroke itampata soon

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

Me naona huyo mwafulani wako hana wivu kama mwafudenge wangu.
Yani imefika mahali naachika jioni narejewa asubuhi kisa wivu.......nakonda!
 
pole mkuu, mi naona kwanza kwa mapenz ya sasa utaja kufa kabla ya wakati, hebu fikir cku moja ukigundua ana m2, hebu ishi nae kwa uhuru kwamba cc ni binadam any thing my happen,

Thanks mkuu kwa ushauri ntaufanyia kazi
 
Me naona huyo mwafulani wako hana wivu kama mwafudenge wangu.
Yani imefika mahali naachika jioni narejewa asubuhi kisa wivu.......nakonda!

Aisee kumbe tuko wengi wenye haya matatizo?? Ila mbona hamtupi uzoefu wenu!! Mnatumia juhudi gani kuwasaidia?? Au mmeridhika na hiyo hali??? Au kuna siku mnahisi mtawachoka na kuwakimbia??!!
 
Wivu unaondoa raha ya mapenzi wivu unaondoa uaminifu wivu unajenga woga wivu unajenga heshima fake!!! Wivu ni sumu kwenye mapenz...

Mimi niliwahi kuwa na wivu ila baada ya michakato ya hapa na pale ule moyo ukafa sijui ulienda wapi...nilifikia kipindi mtu akikohoa me silali shabaaash....
Ushauri wangu ni hivi....
1. Punguza kuwaza mabaya we chukulia kila kitu in a positive way na onyesha kutojali sana mfano mtu kachelewa kurudi home from ofisi jaribu siku moja ku assume kuwa labda ni sababu ya foleni na si kaenda kwa flani...
Au mfano katoka na marafiki jaribu kutombugudhi mpaka arudi na wala usiulize sana we weka mawazo yako + tu usiwaze mabaya.....
2. Kuwa busy mkuu inaelekea muda mwingi upo unawaza mapenzi jiweke busy na kazi jiweke busy na mambo ya msingi hata kwa kujisomea....
3. Usimnyime haki zake za msingi kama kuwa na marafiki maana machoni mwako inawezekana anakuridhisha ila nyuma ya pazia libeneke linanyweka...hebu fikiria kwa nini alipokea simu ile mbele yako then alivyoona umemind akapiga simu kutoa onyo?? Unajua yule mtu alikuelewa vipi??

Anyway chaji imeisha ntaendelea
 
Aisee kumbe tuko wengi wenye haya matatizo?? Ila mbona hamtupi uzoefu wenu!! Mnatumia juhudi gani kuwasaidia?? Au mmeridhika na hiyo hali??? Au kuna siku mnahisi mtawachoka na kuwakimbia??!!

Sina cha kufanya, nimemuelewesha nimechoka, angekuwa just boyfriend ningekuwa nshaondoka, ila ni mchumba wangu so kuachana ni process...!
Ila inakera, sina uhuru, nalazimika kuwa muongo ili mambo yaende, kwa kifupi sina raha....imagine mtu ana password zangu kuanzia ya email, fb, atm card, anakagua phonebook mpaka call logs achilia mbali sms......Inachoshaaa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…