Zorrander wewe ni muumini wa kumcheat mkeo?
nauliza kwa kuwa inasemekana wale walio na wivu wa kupindukia kwa wenzi wao mara nyingi wao ni waumini wa cheating tena ile extreme cheating na kwa hiyo wanahisi kama wanavyocheat na wenzi wao wanacheat hivyo hivyo na hivyo kuwa over defensive kwa mawivu,kama wewe ni muumini mzuri wa cheating basi uache kwani unavyoumia wewe kwa wivu huo ndivyo mkeo atakavyokuja kuumia ukimcheat na pia wivu ukizidi si mzuri kwani unasababisha kutoaminiana na pia kukosa raha kwa mtu mwenye kuonewa wivu kupindukia japo wivu wa kadri ni mzuri kwa wapendanao.
ikiwa wewe si muumini wa cheating ila umejikuta tu una wivu uliopitiliza jaribu haya:
1.jiulize nini kinakufanya uwe na wivu kiasi hicho kwa mkeo?amewahi kukuonyesha tabia fulani za kiusaliti?kama ndiyo labda ukae naye chini umweleze au kumuuliza tabia hizo zilimaanisha nini kwa wakati huo,yeye ndo mwenye majibu yote na kama hujawahi kuona nini kinakufanya uhisi kusalitiwa mara zote kiasi cha kuwa na wivu ulioptitliza?
2.ameweza kuelewa hisia zako akaacha fb, hayuko tena watts up,atajisikiaje akijua kuwa licha ya juhudi zote hizo bado humuamini na huwezi kumuachia uhuru wa kiasi?ataendelea kuvumilia sikuzote na kukupenda sikuzote akiwa na hisia kuwa humuamini na wala huwezi kumwacha huru walau kidogo?
3.ana mazoea yasiyofaa na wanaume wengine kama wafanyakazi wenzie au hata majirani au marafiki zako wa kiume?kama hapana nini kinakufanya uwe na wivu wa kiasi hiko?
4.umewahi kumkuta kwenye pozi tata akiwa na mwanaume mwingine?kama hapana kwa nini unakuwa na wivu kiasi hicho?kama ndiyo kwa nini usifanye utafiti wako ukajua ukweli kuliko kukaa ukijiumiza?
wansema NO LOVE WITHOUT JEOULOUS ni kweli lakini uwe ule wa kadri,mkeo anavumila kwa sasa lakini ukiendelea hivyo atakuchoka na ataanza kufanya mambo bila kujali ikiwa unaumia au la na hapo nadhani utaumia hata zaidi,kwa hiyo jitahidi tu hasa kama hujawahi kuona dalili zozote za usaliti kutoka kwa mkeo,jiaminishe tu kuwa ni wa kwako sikuzote na ndo maana akaamua kuwa na wewe,after all elewa kuwa wivu wala sio kinga ya wewe kutosalitiwa kama uliyenaye ni msaliti hata bila wivu anakusaliti tu,kaa chini ufikirie mkuu naamini utaweza,all the best.