Wivu umeniponza

We jamaa ni fala sana ..utakufa masikini endekeza wanawake walioachwa na wanaume wenzako..unafikiri kwa nn mwenzako alimuacha na watoto...huyo ni malaya mpenda pesa...acha ufala tafuta mwanamke achana na kahaba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wadau wa JF jukwaa lililosheheni wajuvi wa mambo,

Niende kwenye mada,

Nina mpenzi wangu ambae hadi leo kaniacha ni miaka miwili na miezi sita sasa, tangu tufahamiane nilimpenda Bi dada huyu kwa mapenzi ya dhati, alikua akiishi kwao lakini nikamuwezesha kupanga chumba na kumfungulia biashara iliyokuwa na mtaji wa tsh 4.5m ili aweze kuendesha maisha yake na wanae alioachwa nao, niliweza kulipia chumba kwa mwaka.

Kila kodi ilipokwisha bili ya umeme na maji nilipia, chumba cha biashara pia kila kodi ilipokwisha nilihudumia, matibabu kwa mpenzi wangu na wanawe pale walipougua niliweza, kumpa fedha kwa ajili ya fanicha za ndani kwa kadiri ya mahitaji ya msingi bila kujali nilikua radhi kumgawia yeye nusu ya kipato changu ili akidhi mahitaji yake lakini wivu wangu kwake umeniponza.

Bidada huwa anapokasirika hachagui neno la kuniambia hata ikiwa yeye ndiye mkosaji anakasirika, hii inapelekea mimi kujishusha na kumuomba yeye radhi yaishe japo kosa ni la kwake, amekua hapendi kuulizwa maswali japo huwa namuuliza kwa upole na nia ni kulipa afya penzi letu, moja ya maswali yangu asiyo yapenda huwa napenda kila Mara kujua yuko wapi na anafanya nini nikiwa na wasiwasi nikitaka kujiridhisha hapo atanijibu kama huniamini achana na mimi mi najiamini na sio malaya, ni majibu ambayo ukweli huyatoa kwa ukali.

Hali ambayo imekua ikinisikitisha, kisa sasa cha kuachwa ni kodi ya nyumba imekwisha ya huu mwaka, nami hali yangu kiuchumi sio nzuri nikamuomba anivumilie nimtafutie lakini hakunielewa amepunguza mawasiliano kama ilivyokua kawaida yetu kupigiana simu Mara nne kwa siku kwani siishi nae huwa nikitaka kwenda kwake ni hadi nimpe taarifa.

Ndugu zake asilimia kubwa wananifahamu kuwa mi ndio namlea ndugu yao lakini Jana usiku nilimpigia simu baada ya kuwa nzima kupita bila mawasiliano nikiwa kuna mtu kanitonya kuwa bidada kakaa baa na mtu anakunywa bia mi kumpigia nikamsalimia nikamuuliza yuko wapi, akanidanganya nikakwambia vuka barabara tuonane akaniambia sawa, dk chache akanipigia mbona sikuoni nikakwambia sipo pale lakini kuna mtu akaniambia umekaa na mtu baa akaniuliza ninani sikumtaja akasema nikimjua atanitambua.

Kwani kukaa na mtu wa kiume ndio nikalale nae mimi najitambua nikakwambia naomba kukutana nawe, akaniambia kwa hasira hutanikuta wala sikuhitaji huna msaada kwangu wewe ukipigiwa simu na mtu unapaniki na kunihisi kama polisi, mimi sitaki huo ujinga na kama unadhani mimi ni malaya basi kuanzia leo futa namba yangu na usinitafute tena aniache na maisha yangu.Tangu nikuombe kodi umekuana visavisa kata mawasiliano na mimi.

Wana JF mimi sikumjibu lolote zaidi ya kusema asante, bidada nampenda sana uchumi wangu umeyumba lakini kwa maneno alionitamkia nimebaki njia panda biashara yake niliompa mtaji umekata.

Naomba ushauri wenu kwani nahisi kuchanganyikiwa jinsi nilivompenda lakini wivu wangu kwake umeniponza, nifanyeje wana JF nisaidie ushauri.
Kwa maelezo yako inaonesha hajawahi kukupenda
 
Asanteni wote mliotumia muda wenu kuniambia lolote,nimeyapokea yote na nilichozingatia na kukifanyia kazi ni kuwa na maisha mengine mapya bila yeye niwashukuru tena wana jf wote ushauri wenu umeniponya na penzi la mateso.
 
Asante kwa ushauri wako maisha yangu yanaenda hata bila yeye sasa nimejua niishije na viumbe hawa ninapokutana nao
 
Hapo tatizo siyo wivu wako...

Tatizo ni huyo aliyekuwa mwanamke wako, yupo na wewe ki-maslahi asilimi 100, unalijua hilo na unaliona lakini unajifanya mahaba niue...

Utavuna ulichopanda... She is not your type... Humuwezi na uchumi wako mdogo...


Cc: mahondaw
 
Kwa mtazamo wangu kulikuwa hakuna haja ya kufungua uzi kuomba ushauri labda kichwa cha khabari kingekuwa fundisho au somo ulilolipata maana rangi zote kakuonyesha weye ulitakiwa uchukue hamsini zako coz alipenda kipato na si mtu wa kukumbuka fadhila
 
Acha nae huyo, ni mbwa koko,, jipange upya kwa maisha mengine, huyo anaonesha hana mpango na ww, alipenda pochi kuliko mpenzi, hahahah
 
Jamani kuna watu wana bahati wanazipiga teke! Wenzie wanatafuta wa kumpa 2000 hawampati!! Upele humpata msi kucha!
 
Tatizo moja umeingia kwenye penzi lake mzima mzima badala ya kukaa mguu ndani mguu nje..unaona sasa, umelipia kooote huko umekwama amekuacha...Hawa viumbe hawaelewekagi mzee mwenzangu ni kuishi nao kwa akili tu...

Unaweza ukaanza maisha mapya lakini kama utakuwa tayari kumpotezea, kwanza demu yenyewe inaonesha hana Real Love na ana sponsor mwingine..


Pole sana Mzee Baba
 
Ningemjua huyo mwanamke ningempa mbata kama mwanamke mwenzie wenzie tunaangaika kusali,kufunga,kuomba,Mungu atupe mume bora linampata yeye anachezea aiseeee Jamani Huyu mwanamke ni pepo bwana Mimi mwanaume anifungulie tu biashara aiseeee ata akitaka nimbebe mgongoni nambeba tu Mungu amlaani uyu Dada

Sent using Jamii Forums mobile app
Samahani, hili Tangazo umelipia??
 
Kwa mtazamo wangu kulikuwa hakuna haja ya kufungua uzi kuomba ushauri labda kichwa cha khabari kingekuwa fundisho au somo ulilolipata maana rangi zote kakuonyesha weye ulitakiwa uchukue hamsini zako coz alipenda kipato na si mtu wa kukumbuka fadhila
Kaka, mapenzi yanatabia mbaya sana asee unawezakua kipofu
 
Back
Top Bottom