kbm
JF-Expert Member
- Oct 5, 2012
- 5,224
- 1,686
Mwanamke mmoja na watoto wake
wawili, wameokolewa na wasamaria
wema baada ya kufungiwa na
mumewe kwenye nyumba bila
huduma muhimu kwa miaka mitatu
mfululizo kwa sababu ya wivu.
Tukio hilo limetokea kijiji cha Longuo
wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro.
Mwanamke huyo, Janeth Barama
kutoka kijiji cha Ilula mkoani Iringa,
alisema mumewe Arcado Massawe ni
mlevi wa gongo na bangi.
Alisema kipindi chote walichokuwa
kifungoni walikuwa wakijisaidia ndani
huku akiwaletea chakula kidogo mara
chache kwa wiki.
Alidai kuwa sababu ya kufungiwa
ndani ni wivu wa kimapenzi kwa hofu
kuwa atafanya mapenzi na wanaume
wengine.
Huku akibubujikwa na machozi,
alisema mume wake huondoka kila
siku saa 11 alfajiri na kurudi saa 9
usiku akiwa amelewa chakari na
humpiga bila sababu.
Alioomba serikali imchukulie hatua
kali mumewe kwa kuwa akiachiwa
anaweza kuwaua.
Alisema mume wake anafanya kazi ya
ulinzi katika nyumba hiyo ambayo
mmiliki wake anaishi jijini Dar es
Salaam.
Hata hivyo, alisema bosi wa mumewe
hana taarifa za vitendo vya kinyama
anavyofanyiwa na mfanyakazi wake.
Aliendelea kusimulia kuwa mtoto
wake wa pili, Zuena Massawe (1.2),
alijifungua akiwa amefungiwa ndani
ya nyumba hiyo na kwa muda wote
uzazi wake hakuwahi kupelekwa
kliniki lakini anamshukuru Mungu
mtoto yuko salama.
Watoto hao, Zuena na kaka yake,
Obama Massawe (3.5), wameathirika
kiafya kutokana na kuwa na
utapiamlo.
Alisema hii ni mara ya pili kwa
mumewe kumfungia kwenye nyumba
kwani mara ya kwanza wakati
anafanya kazi kwa bosi mwingine
alimfungia kwa miezi sita na bosi
alipogundua alimfukuza kazi.
Mwenyekiti wa kijiji hicho, Gerson
Mambo alisema, jana ndiyo
waligundua kuwa ndani ya nyumba
hiyo wanaishi binadamu baada ya
mwanamke huyo kupiga mayowe ya
kuomba msaada.
Alisema alitoa taarifa kwa afisa
mtendaji wa kijiji ambaye alipiga
simu polisi na kuvunja mlango.
Baadhi ya majirani wameviomba
vyombo vya dola vimsaidie
mwanamke huyo apate haki zake za
kimsingi na watoto wake na
kumrejesha kijijini Ilula kwa wazazi
wake.
Akizungumza na gazeti hili kwa njia
ya simu, Kamanda wa polisi mkoani
Kilimanjaro, Robert Boaz alisema,
mtuhumiwa ametiwa mbaroni na
anatarajiwa kufikishwa mahakamani
ili sheria ichukue mkondo wake.
Aliwapongeza wananchi kwa kutoa
taarifa kituo cha polisi na kumwokoa
mwanamke huyo ambaye angeweza
kupoteza maisha na watoto wake.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
wawili, wameokolewa na wasamaria
wema baada ya kufungiwa na
mumewe kwenye nyumba bila
huduma muhimu kwa miaka mitatu
mfululizo kwa sababu ya wivu.
Tukio hilo limetokea kijiji cha Longuo
wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro.
Mwanamke huyo, Janeth Barama
kutoka kijiji cha Ilula mkoani Iringa,
alisema mumewe Arcado Massawe ni
mlevi wa gongo na bangi.
Alisema kipindi chote walichokuwa
kifungoni walikuwa wakijisaidia ndani
huku akiwaletea chakula kidogo mara
chache kwa wiki.
Alidai kuwa sababu ya kufungiwa
ndani ni wivu wa kimapenzi kwa hofu
kuwa atafanya mapenzi na wanaume
wengine.
Huku akibubujikwa na machozi,
alisema mume wake huondoka kila
siku saa 11 alfajiri na kurudi saa 9
usiku akiwa amelewa chakari na
humpiga bila sababu.
Alioomba serikali imchukulie hatua
kali mumewe kwa kuwa akiachiwa
anaweza kuwaua.
Alisema mume wake anafanya kazi ya
ulinzi katika nyumba hiyo ambayo
mmiliki wake anaishi jijini Dar es
Salaam.
Hata hivyo, alisema bosi wa mumewe
hana taarifa za vitendo vya kinyama
anavyofanyiwa na mfanyakazi wake.
Aliendelea kusimulia kuwa mtoto
wake wa pili, Zuena Massawe (1.2),
alijifungua akiwa amefungiwa ndani
ya nyumba hiyo na kwa muda wote
uzazi wake hakuwahi kupelekwa
kliniki lakini anamshukuru Mungu
mtoto yuko salama.
Watoto hao, Zuena na kaka yake,
Obama Massawe (3.5), wameathirika
kiafya kutokana na kuwa na
utapiamlo.
Alisema hii ni mara ya pili kwa
mumewe kumfungia kwenye nyumba
kwani mara ya kwanza wakati
anafanya kazi kwa bosi mwingine
alimfungia kwa miezi sita na bosi
alipogundua alimfukuza kazi.
Mwenyekiti wa kijiji hicho, Gerson
Mambo alisema, jana ndiyo
waligundua kuwa ndani ya nyumba
hiyo wanaishi binadamu baada ya
mwanamke huyo kupiga mayowe ya
kuomba msaada.
Alisema alitoa taarifa kwa afisa
mtendaji wa kijiji ambaye alipiga
simu polisi na kuvunja mlango.
Baadhi ya majirani wameviomba
vyombo vya dola vimsaidie
mwanamke huyo apate haki zake za
kimsingi na watoto wake na
kumrejesha kijijini Ilula kwa wazazi
wake.
Akizungumza na gazeti hili kwa njia
ya simu, Kamanda wa polisi mkoani
Kilimanjaro, Robert Boaz alisema,
mtuhumiwa ametiwa mbaroni na
anatarajiwa kufikishwa mahakamani
ili sheria ichukue mkondo wake.
Aliwapongeza wananchi kwa kutoa
taarifa kituo cha polisi na kumwokoa
mwanamke huyo ambaye angeweza
kupoteza maisha na watoto wake.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI