Mtende
JF-Expert Member
- Sep 27, 2010
- 6,385
- 7,295
Heri ya mwaka mpya wanafamilia wa JF, naamini kila mmoja amemaliza mwaka salama pamoja na misukosuko mingi tuliyopitia, ni Mwaka mwingine tena tuombe heri kwa kila tunalofanya.
Moja kwa moja niende kwenye mada, imekua desturi kwangu na familia kila tunapopata nafasi tunapita mahospitali au vituo vya watoto yatima kuwafariji kwa chochote hata kidogo ikiwa ni kama sehemu ya sadaka.
Jana tulikwenda Ocean road kuwaona wagonjwa wa Cancer, kiukweli moyo wangu umevunjika sana, nimejikuta nina huzuni kubwa na simanzi lakini na woga pia kutokana na hali za wagonjwa, wengine wamekaa hospitali kwa zaidi ya miezi sita na familia zao zimewatelekeza hawana msaada wa namna yoyote na wapo katika hali ya ugonjwa na maumivu makubwa, akina mama na watoto wametelekezwa na hawana wa kuwapelekea japo mahitaji muhimu kama vile pads, pants,sabuni za kuogea, vocha nk
Wengine hospitali pamekua kama second home kwao na hawana hata mtu wa kwatia moyo wala kuwafariji japo kwa maneno mazuri ( nimesme tu MSHUKURU MUNGU HATA KWA AFYA ULIYONAYO)
Nilifarijika baada ya kuwaona akina mama wa kisomali, wahindi na jamii ya watu wa Asia wakitoa misaada kama vyakula, pads, nguo, sabuni za kuoga na niliambiwa kwamba hao akina mama kila siku asubuhi na jioni hufika kuwagawia wagonjwa chai/uji chakula cha mchana na cha jioni pia, ni kama wanapeana zamu, hawakauki pale hospitali
On the other side nilipata maswali mengi sana nilipowaza viongozi na waumini wa makanisa makubwa kama kwa Mwamposa, KKT, RC, akina Mwingira, Kakobe, Gwajima na sadaka zote wanazopokea wanashindwa japo kurudisha upendo kwa jamii yenye uhitaji, nilikutana na mchungaji mmoja underground alikua anawaombea wagonjwa akaniambia hata akina Mwamposa kabla hawajawa wakubwa walikua wanapita kuwaombea wagonjwa lakini sasa wanatembea na mabodigadi
nawapongeza sana Waislamu, wahindi wasomali kwa upendo wao juu ya wale wagonjwa, Wakristo tujifunze jambo, tusiishie tu kupeleka sadaka zetu kwa wachungaji wachumia tumbo, tuwakumbuke na hawa wenye uhitaji, nayo ni sadaka kuvwa Mbele za Mungu
Mwisho, niseme nimejifunza jambo kubwa sana, kuna watu wanateseka na magonjwa ya kila aina, wamekata tamaa na hawana matumaini ya kuendelea kuishi, sisi ambao ni wazima tunatembea na kucheka na tunafuhia na familia zeti, hebu kila tunapopata nafasi tupite hospitali mbalimbali kuwafariji wagonjwa kwa chochote, hasa wale waliotelekezwa na familia zao na hawana msaada wowote, hata kama huna pesa au chochote cha kuwapa, neno lako la faraja linaweza kumpa uponyaji wa nafsi na tumaini jipya la kuishi na pengine tabasamu kwenye uso wake.
Mungu awabariki na kuwapa afya njema.