Kufuatia Tundu Lissu kushambuliwa Dodoma, wabunge waomba ulinzi binafsi, Serikali yasema haiwezekani kwa sasa

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Balozi Adadi Rajabu ameeleza masikitikao ya kamati ya Ulinzi na Usalama ya Bunge kufuatia kushambuliwa kwa risasi kwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu mwezi Septemba mwaka 2017 maeneo ya Bunge Dodoma na kuleta mshtuko mkubwa kwa wabunge na wananchi kiujumla

Kamati imependekeza kwa kuwa hakuna sheria wala kanuni inayoelekeza wabunge kupewa ulinzi katika makazi yao na hivyo kulifanya jukumu la ulinzi na usalama wa mbunge kuwa jukumu lake mwenyewe na kwa kuwa kazi ya mbunge katika kuisimamia serikali inagusa maslahi binafsi ya watu na makundi ambayo yanaweza kujenga chuki dhidi yao, hivyo sheria ya haki kinga na madaraka ya bunge irekebishwe ili kuweka sharti la wabunge kupewa ulinzi hususani katika makazi yao wanapokuwa katika majukumu ya kibunge mjini Dodoma na katika maeneo yao ya uwakilishi

Pia kuwekautaratibu wa kuweka namba maalumu za usajili wa magari ya wabunge kama MB Muheza, MB Viti Maalum Mbeya n.k

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amesema hoja ya wabunge kupewa ulinzi ni hoja ya msingi na serikali haiwezi kulipinga , lakini kuna miundombinu inatakiwa iwe imefanyika katika nchi ili uweze kufanya ulinzi kwa mbunge mmoja mmoja

Ametolea mfano Dodoma ambapo tayari walishakubaliana na kamati ya Ulinzi na Usalama ya Bunge kwamba maeneo wanakokaa wabungewataimarisha doria pindi ambapo wabunge wapo Dodoma

Na maeneo ambayo wabunge wanakaa kwa pamoja watawekia utaratibu wa askari kuwa katika maeneo hayo lakini utaratibu wa kuwa na ulinzi wa mbunge, mathalani katika kila jimbo ni jambo ambalo linahitaji miundombinu kwanza kabla ya kuweka utaratibu huo kwa kuwa askari watakuwa katika hatari ya kushambuliwa na hata kunyang'anywa silaha

Mwigulu amesema nchi ambazo mbunge anapewa ulinzi, mbunge anakaa kwenye makazi maalumu kama mkuu wa Wilaya ambapo inawezekana kupeleka ulinzi kwa kuwa ni eneo la serikali

Mtu akijipanga na akikudhamiria kukudhuru / kukumaliza hata uwe na Walinzi wangapi atafanikisha tu lengo lake. Wabunge Kazi yao ni Kutunga Sera za Kuijenga nchi na siyo kupoteza muda wa kuomba Ulinzi na hata Sera ya nchi hakuna mahala inaposema kwamba Wabunge wanatakiwa wapewe Ulinzi ila kuna ngazi fulani za Watu ( VIP's ) ambao hupata hiyo fursa.

Ni ' Hoja ' ya Kipuuzi mno kutoka kwa Wabunge waliotaka na nashukuru ombi lao limekataliwa. Kwanza wengi wana ' Hirizi ' zao ambazo siku zote zinawalinda kutong'oka ' madarakani ' sasa wanashindwaje kurudi huko kwa hao Waganga wao na kuzifanyia tu ' updating ' au ' adjustment ' kidogo hizo ' Hirizi ' ili ziweze pia kuwalinda / kuwakinga na Maadui?
 
Mkuu Genta sipingi mtazamo wako, lakini huwa tunaona wakuu wa wilaya wanapewa ulinzi, ni kipi special toka kwao mpaka wapewe huo ulinzi? Sioni kama ni jambo la lazima sana wabunge kupewa ulinzi, lakini inakuwaje wakuu wa wilaya wanapewa wakati hawana lolote la maana katika jamii?
 
Mkuu wa Wilaya ni muwakilishi rasmi wa Serikali na shuguli zake zote wakati Mbunge ni muwakilishi tu wa Jimbo fulani ambalo lipo ndani ya Wilaya / Himaya husika ya huyo huyo Kiongozi wa Serikali ( Mkuu wa Wilaya )

Wala huhitaji akili kubwa kuweza kujua ya kwamba kuna tofauti kubwa sana ya Kiutendaji na Kiunyeti baina ya Mbunge na Mkuu wa Wilaya ambaye ana dhamana kubwa sana na Serikali yake ya Wilaya ambayo inawajibika katika Serikali Kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wape Elimu hii na Wenzako pia ili mbadilike pia Kimtizamo na Kifikra.

Kila la kheri.
 
Nakubaliana na maelezo yako. Ila kwa haya yanayotendwa na wakuu wa wilaya sioni jipya zaidi ya kuhakikisha ccm inabakia madarakani. Inshort maelezo yako hayajakata kiu yangu kwanini mkuu wa wilaya apewe ulinzi wakati anachofanya ni kazi za mazoea, na cheo hicho kinapewa upewa ulinzi kutokana na mfumo tuliorithi kwa wakoloni na wala sio tija ya cheo chenyewe. Labda urudi upya na hoja zaidi za kiushawishi kwa kuainisha hatari ya kiuasalama ambayo inamtofautisha sana na mbunge kiusalama. Nataraji hoja zinazoingia akilini na sio hizi hoja za kwamba huo ndio utaratibu ( business as usual)
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mtu akijipanga na akikudhamiria kukudhuru / kukumaliza hata uwe na Walinzi wangapi atafanikisha tu lengo lake. Wabunge Kazi yao ni Kutunga Sera za Kuijenga nchi na siyo kupoteza muda wa kuomba Ulinzi na hata Sera ya nchi hakuna mahala inaposema kwamba Wabunge wanatakiwa wapewe Ulinzi ila kuna ngazi fulani za Watu ( VIP's ) ambao hupata hiyo fursa.

Ni ' Hoja ' ya Kipuuzi mno kutoka kwa Wabunge waliotaka na nashukuru ombi lao limekataliwa. Kwanza wengi wana ' Hirizi ' zao ambazo siku zote zinawalinda kutong'oka ' madarakani ' sasa wanashindwaje kurudi huko kwa hao Waganga wao na kuzifanyia tu ' updating ' au ' adjustment ' kidogo hizo ' Hirizi ' ili ziweze pia kuwalinda / kuwakinga na Maadui?

Hao wabunge na mwenyekiti wao ni wapuuzi badala ya kufanya kazi waliyoomba ya kuibana serikali kwa niaba ya wapiga kura wao wanaomba walindwe against what? Ulinzi sio dawa. Wabunge watende haki na kutumia muda mwingi kuwasemea wanyonge huo ndio ulinzi mzuri but when they wish to squander tax payers money hakuna Askari anayeweza kuwalinda. Kushambuliwa kwa Tundu Lisu was a special case and they say it was carried out by security details attached to Daudi Bashite ! Hilo eneo la area there was security but they went into hiding and provided daylight for the attempted assassination of the learned MP ! Rajabu Adadi a seasoned cop Ex - DCI knows that na kwamba hiyo sanaa ya kutamka ulinzi it’s just trying to wash dirty linen in public. Matokeo ya kamati iliyokuwa ichunguze hayo mauaji iliishia wapi that is the million dollar question that remain unanswered ! Marufuku kuwapatia wabunge ulinzi labda wakatwe mishahara yao walipie hao Police wa CCM au from private security companies ! Narudia ni marufuku kutumia hata senti hamsini za walipa kodi kuwalinda they can go to hell!
 
ccm oyeeeeee
 
Zidumu fikra za mwenyekiti
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mkuu Genta sipingi mtazamo wako, lakini huwa tunaona wakuu wa wilaya wanapewa ulinzi, ni kipi special toka kwao mpaka wapewe huo ulinzi? Sioni kama ni jambo la lazima sana wabunge kupewa ulinzi, lakini inakuwaje wakuu wa wilaya wanapewa wakati hawana lolote la maana katika jamii?
Kwa nini unasema wakuu wa wilaya hawana lolote ktk jamii wakati mkuu wa wilaya ni mlinzi wa AMANI na ni M/kiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani? ktk jukumu la ulinzi wa amani ambalo ni moja ya majukumu ya msingi ya mkuu wa wilaya, District Commanding Officer yaani (OCD) na makamanda wengine wa vyombo na Idara za usalama hapo wilayani huwajibika chini ya mkuu wa wilaya hivyo automatically mkuu wa wilaya ni Afande no.1 hapo wilayani.
 
Ningetoa wito kwa viongozi wa serikali na vyombo vya dola. Wawalinde viongozi wote wa CHADEMA, hii itapunguza mauaji yanayoendelea kwa sasa. Na pia itatoa picha elekezi kwa jumuia ya kimataifa kwamba serikali inajali raia wake.
 
Hahaha unafurahisha, ni sawa kuwaambia marekani wawalinde ISIS, wakati ndio adui zao.
 
Ni kweli, lakini uadui wa ISIS na marekani ni tofauti na hapa, hawa raia wanaouliwa anaweza kuwa leo CHADEMA kesho mtaji kwa CCM. Ama leo CCM kesho mtaji kwa CHADEMA. Hapa naposema wawalinde raia walio ndani ya CHADEMA ambao ni soft target.
 
Hahaha mbona kule mbugani kuna askari wa TANAPA wanalinda wanyama halafu serikali inagawa vitalu kuwawinda hao wanyama.
Huu ndio ustaarabu wetu, kuua kutishia wananchi eti wakiogopwa ndio wanaita amani.
 
Mbunge aliyeshambuliwa alikuwa kwenye makazi yenye ulinzi na wasio na ulinzi hawajawahi kushambuliwa.
Hoja ya kuwapatia ulinzi haina nguvu hapo, kamati ingekuwa makini au siyo biased, wangeomba kuunda kamati teule kuchunguza jambo hilo ili lijulikane chanzo na watekelezaji na mbinu za kuzuia lisitokee tena kwa mbunge.
 
Ni kweli, lakini uadui wa ISIS na marekani ni tofauti na hapa, hawa raia wanaouliwa anaweza kuwa leo CHADEMA kesho mtaji kwa CCM. Ama leo CCM kesho mtaji kwa CHADEMA. Hapa naposema wawalinde raia walio ndani ya CHADEMA ambao ni soft target.
Hahaha hapa hawataki kupingwa, kanakwamba wao ni miungu. Kuua chadema ndiyo primary goal yao, itachekesha waki deviate goal yao waanze kuwalinda.
 
Back
Top Bottom