Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,014
- 144,372
Kupitia akaunti ya twitter ya Tundu Lissu,nimeona video (bila shaka ni huko Kawe, Dar-es-salaam) inayoonyesha rundo la kura zinazidaiwa kuwa ni feki huku Polisi wakishirikishwa kuzitambua/ kushuhudia karatasi hizo za kura ambazo zimepigiwa kura mgombea wa CCM.
Video hii ni tofauti na ile inayoonyesha wananchi wakichoma moto kura walizozikamata.
Ukiacha huko Kawe, kuna video nyingine mtandaoni(twitter), inaonyesha wananchi(mkoani Kigoma) wakivamia kituo cha kupigia kura baada ya kubaini uwepo wa kura feki kwenye mfuko huku mwenye mfuko akigoma kuutoa /kukaguliwa na kusababisha vurugu kituoni hapo.
Kwakuwa hali hii inaripotiwa katika maeneo mengi nchini, ni wazi Tume ya Uchaguzi imeshindwa kutimiza wajibu wake na hivyo inapaswa kujiuzulu yote kuanzia mwenyekiti, mkurugenzi na watendaji wengine wote waliohusika kusimamia huu uchaguzi unless watuthibitishie kuwa madai haya ni ya uongo.
Mwisho, uchaguzi huu wote ufutwe iwapo tuhuma/ madai haya yathibitika kuwa ni ya kweli.