Wito Kwa wana JamiiForums kuhusu ukosoaji wa Rais Magufuli


Ni sahihi unachokisema. Ila ni vizuri tujifunze kukosowa kwa staha siku zote na kwa watu wote na siyo kwa Rais tu.
 
Nadhani kumfananisha Rais na Baba kwenye familia sio sahihi. Baba hapatikani kwa kura bali kwa bidii zake kwa Mama
Ziko aina nyingi za kupiga kura sio lazima kwa karatasi na pia aina nyingi za ballot box hivyo hata zile pia ni kura! .

Paskali
 
Mkuu Msemaji Ukweli, ni kweli kifungu hicho ni Kinga ya rais kutokushitakiwa mahakamani, ila kinga hiyo inahusu rais kutokushitakiwa mahakamani katika utekelezaji wa majukumu ya kirais tuu na sio kila kitu.

Mfano Ben alipofanya biashara akiwa Ikulu, kufanya biashara Ikulu sii miongoni mwa majukumu ya kirais akiwa Ikulu hivyo anashitakika kwa kosa la abuse of office, na kutokushitakiwa ni kwa heshima tuu ya kumstahi aachwe apumzike kwa amani.

Au JK alipoyasamehe yale majizi ya EPA, hakuna kifungu chochote cha katiba yetu kinachompa rais mamlaka ya kuzuia sheria isichukue mkondo wake. Yaani jitu ni lijizi la malí ya umma, limekamatwa red handed, badala ya sheria kuachwa ichukue mkondo wake, majizi yale yalisamehewa!.

Kwa mujibu wa katiba, mwenye mamlaka ya kufungua mashitaka au kutofungua ni DPP na sio rais. Mamlaka ya rais ni kumsamehe mfungwa yoyote baada ya kuhukumiwa na sio kuzuia majizi yasishitakiwe, hivyo JK anashitakika ile kinga ya kutokushitakiwa haimhusu ila kwa heshima ameachwa apumzike kwa amani kama Ben, hivyo hata aliyepo ni kweli hata afanye madudu gani ikiwemo uvunjaji wa katiba, hatafanywa chochote, ataachwa apumzike tuu kwa amani.

Usikute hizi ni miongoni mwa sababu zinazopelekea bao la mkono au zisipotosha zitatosheshwa.

Paskali
 
Mimi nakubaliana na mleta uzi ingawa kuna mahali napata shida sana. "Constructive criticism" ni ya namna gani kwa common sense ya kawaida? Mimi nafikiri watu waseme mawazo yao mbadala. Na wayaseme vizuri kabisa, hata kama watasema hawakubaliani kabisa na mawazo ya mtu mwingine. Bado sioni tatizo liko wapi. Tuondokane na hii tabia ya kupenda kukubaliana kwa kila kitu kama penguins. Kuna dhana ya diversity inasema, kila mtu ana utofauti wa namna yake na wa kipekee. Hata wachangiaji wa Jf tuna mawazo mseto yenye kuakisi diversity zetu. Mtu asiyependa kusikia mawazo tofauti au asiyependa kukosolewa hajawahi kuishi katika sayari hii bado, ni mtu aliyejifungia kwenye box lake linaloitwa "illusion".
 
Mkuu ,TL Marandu, hili ni angalizo tuu!.

Paskali
 

Aanze kubomoa nyumba za serikali alizouza,arudishe hela za samaki Na meli mbovu arudishe hela zetu tutamuona anafanya la maana,yeye anagusa walikokosea wenzake tu Bali alikoboronga yeye anatutisha eti ataehoji MV DSM anahoji kifaru cha jeshi!!!!???huku ni kulipiza visasi maana ya kwake ni mengi Na hayaguswi Na ukijaribu wataku Ben SAA 8
 
Pascal issue ya kukosoa JPm itabadilika pale atakapobadili lugha yake against Wapinzani wake Wa kisiasa.Pale atakapojua Uchaguzi umekwisha na Tanzania ni yetu sote.

Pale Wanachama wa CCM watakapojua miiko ya sheria na haki za RAIA kwamba hakuna aliye juu ya Sheria.

Matusi, Majigambo,udhalilishaji,ubaguzi,vitisho na visasi lazima vikemewe siyo wakati wake.

Tumepata Rais ambaye anaabudu na kuheshimu visasi,chuki na ubaguzi. Anayoyasema.mdomo ni si anayoyatenda.Yuko tofauti na Makamu wake a jitahidi kubadili ka amasivyo ameligawa Taifa na limegawanyika aone matendo yake kwamba ni maovu asikimbilie niombeeni.

Tutaliombea Taifa lakini si MTU mwenye Chuki, visasi na ubaguzi. Na katika marais atachukiwa na wengi sana.
 

Siyo hivyo tu aache chuki,visasi na ubaguzi havijengi Bali vinabomoa Taifa.
 
Huu uzi sikuwahi kuuona kabla. In a way nashukuru sikuwa nimeuona !
Ila pia kama huyu ni yule yule Mayala sasa naelewa kwa nn ktk ule mkutano na waandishi wa habari yaliulizwa maswali ya kitoto !
Tatizo sugu kwa ss wa TZ ni unafiki !! Na utatumaliza milele na milele. Sasa sijui ni ukanjanja au, tuanze kufundishana siasa 101 ?

Zama hizi sio zama za ujima, people have to speak up their mind, na siyo mambo ya kupewa ubwabwa na kofia na kushangilia kila kitu !! Mikataba mliingia, mkaitetea kwa mbwembwe na kushangilia kwa kura za ndiyoooooo then leo mjifanye mna uchungu eti wazalendo ?

Mnasema tuwaombee kwa mungu kila siku huku nyuma mnakula rambirambi za watoto, na kutoa lugha chafu kwa waathirika wa tetemeko !!

 
Uzi wa kijinga kabisa kupostiwa na MTU anaejiita GT hapa jamii forum, vyovyote iwavyo binadamu hapangiwi namna ya kufikiri,kutoa maoni n.k


Kuweni wema mtaona tu mambo yanabadirka yenyewe
 
amtoe na bashite ,
 
Utumwa ni Utumwa Tuu, hata wa Fikra nao ni Utumwa.
 
Mwenye kuhitaji kuheshimiwa anapaswa kuanza kujiheshimu mwenyewe na kuwaheshimu wale wanaomzunguka nk. Zile kauli za bukoba na moshi zilikupendeza wewe? Uvunjaji wa dhahiri wa katiba kuhusu mikutano ya vyama vya siasa wewe unaridhika nao? Hebu tufike mahali kijiko tukiijua kijiko tu
 
Mkuu upo sahihi...ila post hii ilitolewa kipindi kile cha kujipendekeza kupata UKUU wa mikoa na wilaya.
sahivi huyu Pasco mwenyewe anamnyea mukulu ipasavyo...maana hatamani tena kupata hata ujumbe wa 10 houses
 
Utumwa ni Utumwa Tuu, hata wa Fikra nao ni Utumwa.
Naunga mkono hoja, tena Mwalimu Nyerere alitufundisha, hakuna umasikini mbaya kama umasikini wa fikra. Ila pia heshima ni kitu cha bure. Katika vitabu vyote vya dini tunafundishwa utii wa mamlaka halali. Na katika mila zote na desturi zote za Kiafrika tunafundishwa kuwaheshimu wakubwa. Na katika familia zetu tunafundishwa kuwaheshimu wazazi, waheshimu baba na mama upate miaka mingi na heri duniani. Rais wa nchi ni kiongozi wako, ni mkubwa kwako na ni kama baba wa familia ya Watanzania, hivyo pamoja na yote, anastahili heshima. Hivyo mimi katika hili la heshima, nakiri kuwa mtumwa!.

P.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…