Wito Kwa wana JamiiForums kuhusu ukosoaji wa Rais Magufuli

Paskali, nakubaliana na wewe, na si kwa RAISI pekee, hata binadamu mwingine yeyote anapokoselewa, akosolewe kwa heshima... HATA BIBLIA INATUHIMIZA kuonyana kwa upendo.....

Lakini hulka ya binadamu ni kulipa kisasi pale anapohisi kafanyiwa kitu fulani kibaya, na haswa mbele ya hadhara....

Kinachompa unafu mmoja kati ya hao wanaohisi kuonewa hadharani, ni YEYE KUWA NA MADARAKA KIKATIBA kuliko mwingine....

Na huyo anayehisi anaonewa, akihisi anaonewa na mwenye madaraka na huku akijua hawezi kumfanya kitu, BAADHI au yote kati yafuatayo yanaweza kutokea

1. Kujibiwa hovyo ila ndani ya mipaka ya sheria
2. Kukosolewa kwa namna inayoudhi huku hakuna sheria iliyovunjwa
3. Kutafutwa makosa yako popote yalipojifisha na kutajwa hadharani
4. Watu kutafuta PUBLIC SYMPATHY popote penye upenyo, na kwa sababu wanaokuzunguka wote wanahisi kuonewa, basi ataipata, na mwisho mtawala utalazimika kutumia authorities ulizonazo kama POLISI, TRA, MAHAKAMA etc kumtuliza mtu huyo..

BINAFSI NADHANI,
ILI UKOSOLEWE KWA STAHA, MWENYE MADARAKA ANATAKIWA AKOSOE WATU KWA STAHA....
KAULI KAMA
1. Hawa ndo vichaa tunaohangaika nao....
2. Hamna mia mbili pigeni mbizi
3. Hata ikibidi kula nyasi lazima ndege ya raisi inunuliwe
4. Kinyesi kiwe lami...
5. Watanzania ni malofa..
6. Acheni wivu wa kike (hili liliombewa msamaha....

KAULI KAMA HIZI AU ZINAZIOFANANA NA HIZO, USITEGEMEE WANAOTOLEWA WAKIPATA MWANYA WA KUKUKOSOA WATAKUKOSOA KWA STAHA....

Jiulize tu, hao wanaitwa wachochezi... WHY HAWAFUNGWI PINDI WAPELEKWAPO MAHAKAMANI? Jibu ni kwamba wanatumia lugha mbovu lakini zilizopo ndani ya mipaka ya sheria...

MY CONCLUSION NI KWAMBA, WATAWALA WAKIWA NA LUGHA ZA STAHA, HATA WANANCHI WATAKUWA HIVYO.... KWA HIYO ILI STAHA YA KUKOSOLEWA IPATIKANE, INATAKIWA IANZIE KWA WATAWALA.....

Kwa wale walio na akili zilizo sawa, ulipokuwa mdogo na ukawa unahimizwa kuosha vyombo na mama kila siku huoshi... ULIJISIKIAJE SIKU BABA YAKO ALIPOAMUA KUOSHA VYOMBO ULIVYOLIA CHAKULA WEWE?

tutafakari, tuchukue hatua..
Mkuu thanks for this, very objective, michango kama hii ndio inalisaidia taifa, naamini humu huwa anapitaga, na akikuta mchango kama huu, na kuusoma, amini usiamini, mtu anabadilika!. Kiukweli hata mtu uwe na kichwa kigumu kama nini, kuna hoja ukikutana nazo, lazima zinakuingia tuu, hapa umejenga hoja, heshima lazima itoke kwa mkubwa kwenda kwa mdogo, ili heshima hiyo ikurudie!.

Paskali
 
I think it is wrong, and unfortunate to call President Mshamba, mlimbukeni au dinosaur. By all means criticizes his ideas and his policies, when you think he got it wrong. But don't make it personal.

I like Tony Blair, and Barack Obama when they were on opposition they were always criticizing ideas and policies. Jeremy Cobyrn is doing the same today. The always attack the ball instead of attacking the man. That is how you gain genuine momentum and ability to win election especially in great country like Tanzania.

You can influence majority of decent Tanzanians using decent language. Unaweza kufurahisha genge kutumia matusi and kejeri, but you'll never win any election using this strategy.

Majority of Tanzanians are still good, decent people who like other Tanzanians to use decent language. They are put off by anybody who always resort to Matusi and kejeri.
Mkuu Charles, naunga mkono hoja, hili ninilizungumza katika uzi huu.

P.
 
Wanabodi,
Huu ni wito tuu kwa wana jf kuhusu ukosoaji wa Rais wa nchi, Mhe. Dr. John Pombe Joseph Magufuli,
kama kuna mahali rais kama binadamu amekosea, au amefanya ndivyo sivyo, tupaseme kwa unyenyekevu kwa lugha ya heshima na staha, kisha tuweke na ushauri wa the right thing to do, hivyo ukosoaji kwa rais, ufanyike constructively kwa nia njema ya kujenga na sio kubomoa, yaani tufanye "a constructive criticism" hivyo ukosoaji huu utakuwa na nia ya kumsaidia rais wetu kuwa rais bora zaidi na kulisaidia taifa kusonga mbele na sio kurudi nyuma kwa sababu kwa mujibu wa katiba yetu, rais hawezi kukosea ndio maana hawezi kushitakiwa. Rais ana sehemu mbili, rais ni presidential institution hivyo hawezi kufanya kosa lolote ni perfect na kila kauli yake ni sharia, inafuatiwa na utekelezaji tuu, lakini hiyo institution inashikiliwa na mtu anayeitwa John Pombe Joseph Magufuli, huyu ni binadamu, he is a human anaweza kukosea.

Nakiri kupandisha uzi huu kutokana na mchango wa mwana jf huyu

Rais wa nchi ni kama baba wa familia, anahitaji kuheshimiwa.

Hata ikitokea baba mwenye nyumba au baba nyumbani amekosea jambo fulani, anakosolewa kwa heshima kiutu uzima kwa kutumia lugha ya heshima na staha na sio lugha za dharau, kebehi, machukizo au matukano! .

Hata akidanganya haitwi muongo anaitwa hayuko sahihi sana, au ameshauriwa vibaya kwa sababu rais wa nchi hawezi kudanganya, wala hawezi kusema uongo!.

Hata akichelewa kwenye shughuli haambiwi kachelewa maana mkubwa hachelewi bali anakuwa bado hajawasili kutokana na kutingwa na shughuli muhimu, na asipotokea kabisa ni kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu!.

Simaanishi rais Magufuli yeye ni malaika hivyo hawezi kukosea au kufanya makosa, no!, rais Magufuli naye ni binaadamu tuu kama sisi binaadamu wengine wote, na siku zote sisi binaadamu ni viumbe dhaifu, hivyo rais Magufuli naye ana madhaifu yake ikiwemo kuonekana kama ni mtu wa kupenda misifa kupindukia, anapoongea kuna wakati anaonekana kama ni msema hovyo au kama anapayuka, au anaropoka, na katika kufanya maamuzi, kuna wakati anaonekana kama anatenda kwa pupa au papara na baadhi ya maamuzi yake, kuonekana kama ni maamuzi ya chuki au kukurupuka ila kwa vile yeye ndie kiongozi wetu Mkuu, kuna mambo ambayo hatupaswi kuyasema hivyo yalivyo, hata kama ni kweli, ikiwemo kumuita rais ni muongo hata kama ni kweli sometimes anaweza kusema kitu cha uongo hatupaswi kusema rais ni muongo bali rais alikuwa hajashauriwa vizuri au alikuwa ana joke tuu, au anazungumza kwa utani tuu, yaani rais anatania au rais ameteleza tuu ulimi!.

Mfano rais alipohimiza kufyatua tuu watoto kisa atasomesha bure. Tamko hili lilikwenda kinyume cha uzazi wa mpango, hapa rais kiukweli aliropoka na kuteleza ulimi, lakini haiwezi kusemwa kuwa rais karopoka, bali rais alikuwa anatania tuu watani zake, wazaramo!. Siku alipotamka hivyo, hata mimi nilishitushwa na tamko lile ( Rais Kusitisha Uzazi wa Mpango Kwa"Fyatueni Watoto wa Kutosha",Ni Yake au ni ya Wale Wazee wa..?!.)
Lakini baada ya siku mbili tatu, Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu aliibuka na kulitolea ufafanuzi wa kina tamko lile kuwa lilikuwa sii kweli bali rais alikuwa akiwatania tuu watani zake Wazaramo!.

Mfano kwenye hoja ya udikiteta, ni kweli rais Magufuli ni dikiteta fulani hivi, lakini hivyo ndivyo alivyo, na sio kwamba anajifanyisha, ila pia, kwa Tanzania hapa tulipofika, seriously tulihitaji sana mtu mwenye sifa, silika na haiba za udikiteta ndio anaweza kuinyoosha hii nchi ilivyopinda, siku nyingi tumekuwa tukilaani u pole wa Kikwete hadi kumuita "dhaifu" hivyo tumekuwa tukisali kumuomba Mungu atupe kiongozi imara, shupavu, thabiti, ambaye sio mtu wa mchezo mchezo, na kweli hatimaye Mungu akaisikia sala yetu ametupatia Magufuli ambaye ni dikiteta kweli ila sio dikteta mbaya kama Hitler, huyu ni dikiteta mzuri " a benevolent dictator", hivyo badala ya watu kuulaumu huu udikiteta wa rais Magufuli, tunapashwa kumshukuru Mungu kutupatia Magufuli.
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba!

Watu walipoitwa Vila.za, hatukunyamaza, tulitoa ushauri humu.
Wito kwa Baba Jesca: Watendee Haki Kina Jesca Wote Ili Nao Wapate Bahati Kama Jesca!.

Hata alipozungumzia mishahara ya peponi, pia tulitoa ushauri humu
Rais hana mamlaka ya kupunguza mshahara wa mtumishi yeyote

Hata majumbani mwetu hasa majumba ya Kiafrika na Kiswahili, baba ambaye ni mkuu na kichwa cha nyumba, kuna mara kibao anakosea hasa sisi mababa wa Kiafrika tunaofuata mila zetu za kiasili za Kiafrika na mambo yetu yalee ya Uafrika wetu, na pia sio malaika hivyo tuna madhaifu mengi tuu ambayo wamama huyajua huyaona, huyavumilia lakini hawayasemi hadharani.

Kuna namna ya ukosoaji wa heshima na staha wenye lengo la kujenga, a constructive criticism ambao hufanywa in good faith na kuna ukoasoaji wa udhalilishaji wenye lengo la kubomoa ambao hufanywa in bad faith, ridiculously au kumdhalilisha, mkosolewa kwa nia ya kumjengea chuki, achukiwe, kumshushia hadhi na heshima ili aonekane ni mtu wa hovyo, etc huu sio ukosoaji mzuri hata kama ni kweli amekosea, yaani japo is the truth but the motive behind is ill motive.

Simaanishi sasa ndio wote kazi yetu iwe ni moja tuu, kumhusu rais wetu, iwe ni kumuimbia tuu nyimbo za sifa na mapambio, no !, tumkosoe rais Magufuli kwa heshima na kwa kutumia lugha ta staha kwa nia njema kabisa kwa lengo la kumrekebisha na kumsaidia na sio kumdhalilisha.

Tanzania ni yetu sote, sio Tanzania ya Magufuli pekee, na japo CCM ndio chama tawala, haimaanishi Tanzania ni ya CCM, Tanzania sio ya CCM pekee, ni Tanzania ya wote, hivyo we all have a role to play and a responsibility of duty of care kujenga nchi yetu na sio kuibomoa na kumjenga rais wetu na sio kumbomoa regardless tunampenda, hatupendi, tulimchagua, hatukumchagua, kama wazalendo wa nchi hii ni lazima kuijenga nchi yetu na kumsaidia rais wetu as a responsibility and a duty of care, kama inavyotokea kuwepo kwa mtoto mwenye ulemavu katika familia, hakuna anayependa ulemavu, lakini imetokea, lazima tumpende and we have a duty of care kumsupport, kumsaidia na kupenda kwa dhati, vivyo hivyo ndivyo ilivyo kwa Magufuli, ndie rais wetu na hivyo alivyo ndio alivyo tumpende na kumpa kila aina ya ushirikiano ili aweze.

Kuna watu katika kumbonda rais Magufuli, kila siku kazi yao wao ni kuponda tuu, hata akifanya mazuri vipi, wao wataponda tuu, kubeza, kukosoa kila kitu na kumbomoa tuu na wengine humsifia Nyerere, yaani kumtumia wasifu wa Nyerere as a reference, ila kiukweli ukimwangalia rais Magufuli kwa jicho la karibu, yuko kama Nyerere kwa karibu kila kitu
Magufuli Kama Nyerere:Ni Mtu wa Watu, Hapapasi, Hamung'unyi, Ni Kazi Tuu, Ila Pia,Sio Kama Nyerere!.

Katika kujenga nchi the motive iwe ni kujenga kila kitu ikiwemo kujenga watu akiwemo rais anahitaji kuendelea kujengwa na sio kubomolewa tuu.

Japo nafahamu katika kujenga, kuna sehemu inaweza ikakubidi ubomoe kwanza ndipo ujenge, ubomoaji huo hufanyika kwa makini sana ili usibomoe kusiko husika na kila ubomoaji huo ukifanyika hufuatiwa na ujenzi papo kwa papo! .

Nitapenda kuiona jf ya hivyo, wale waashi mahiri wa jf ambao kazi yao ni kubomoa tuu, wapewe jukumu la kujenga pia sio kila siku wao ni kubomoa tuu, mwisho watapewa sifa ya kuitwa wabomoaji tuu ili hali tuna wajenzi imara na mahiri humu tena waliopitia kozi za uanagenzi kwa wale mahiri kabisa.

Wana jf tuwe wakweli kumhusu rais Magufuli toka ndani ya nafsi zetu sio kwa kuvaa miwani yenye kuona upande mmoja tuu wa mabaya tuu, mapungufu tuu na makosa pekee, bali kama kuna mema pia tuyaone, kama kuna mazuri pia tuyaangazie na kuyasema as encouragement kwa rais wetu mpendwa Mhe Dr John Pombe Joseph Magufuli.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali
Rejea kuhusu ukosoaji. Zifuatazo hapa chini ni baadhi tuu za mada zangu za ukosoaji.

Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria! .
JF Modes, Magufuli ni Rais Wetu, Asiabudiwe, Asiogopwe, Bali Aheshimiwe!.
Katazo la Rais Kusafiri Nje ya Nchi bila Vibali: Je, Halikiuki Haki za Binaadamu?!..
Rais hana mamlaka ya kupunguza mshahara wa mtumishi yeyo
te
Rais Magufuli, Waliomchagua Wanajuta!, Wasiomchagua Wanamshangilia!. Akishika Chama, Watakoma

Magufuli, "Kama Unaona Kazi ya Urais ni Ngumu Kwako, Jiuzulu! ".

Je inawezekana huu ndio mwisho wa utumbuaji wa papara na kukurupuka?! Mkuu kutumbuliwa soon!
Tumekuchoka sasa na wewe, too much!
 
Magufuli si malaika ! ni binadamu kama wengine ! Anawaza,analala,anakula nk kama wengine tu ! Cha msingi tujaribu kumsoma kiongozi wetu kuwa nini ilikuwa dhamira yake kwenye jambo fulani ! Rais anaweza akawa na dhamira fulani njema juu ya jambo fulani lkn akateleza tu ktk namna kuliwasilisha kwa wahusika,Rais ni binadamu kama wengine tu jamani,Cha msingi ni sisi kujiongeza kwa kumuelewa rais wetu anataka nini na nini dhamira yake juu ya jambo fulani tutaishi kwa amani sana.
Basi ni vyema nae ajue kua wanaomkosoa nae ni binadam kama yeye. Labda ungesema kua yeye ni MUNGU basi ungeeleweka
 
Pole Lissu,Mungu atakuponya,Pole Lissu.

Leo nimemsikiliza Katibu mkuu wa Chadema Dr Vicent Mashinji akielezea hali ya Tundu Lissu,nimestuka sana kwamba mguu na mkono wa kushoto pamoja na nyonga zimevunjwa,mara ya kwanza nilipopata taarifa za Lissu Kupigwa Risasi,nilichagua kukaa kimya nisiseme wala kuandika kitu,niwasikilize zaidi wengine.

Baadae nilianza kuona picha na taarifa mbalimbali za jinsi Lissu alivyojeruhiwa,niliumia sana kuona binadamu mwenzangu alivyoumizwa,sikuwa na taarifa sahihi jinsi Lisu alivyoumizwa.

Kesho yake nikamuona Spika akitoa taarifa bungeni na kuueleza umma kuwa Lisu alimiminiwa Risasi 32,nilistuka sana,kwa nini Risasi 32 zimiminwe kwa mwanadamu?mtu ambaye si jambazi?inakuwaje Risasi zaidi ya 30 zimiminwe kwa Mwanasiasa na mwanasheria?.

Nilibaki natetemeka,nikikuomba Mungu anipe moyo wa kujifunza kwa wengine na nijue hasa kwa nini mwanasiasa na mwanasheria amiminiwe Risasi zaidi ya 30?kakosa nini?

Kwa nini najiuliza maswali mengi mpaka sasa na kubaki njia panda?

Binafsi nilimfahamu Lissu kabla hajaingia bungeni mara ya kwanza kukutana nae ilikuwa mwaka 2006,wakati huo Lissu alikuwa mpambanaji mkubwa na makampuni makubwa ya uwekezaji kwenye sekta ya madini nchini Tanzania!.

Nilikutana nae wakati huo nikiwa nimejikita zaidi kwenye uandishi wa habari za madini,tulijikuta wote tupo kwenye eneo moja,yeye akifanya kama mwanasheria na mimi nikifanya kama mwandishi wa habari.

Lissu aliniambia amekuwa na mapambano makubwa na kampuni la Barrick,alikuwa akipaza sauti kweli kweli kuhusu wizi unaofanywa na wawekezaji hawa,Lissu alikuwa ni miongoni mwa wanaharakati kutoka chama cha wanasheria wa mazingira waliopaza sauti kutaka uchunguzi ufanyike kuhusu tuhuma dhidi ya mgodi wa Bulyanhulu kuwa uliwafukia baadhi ya wachimbaji wadogo,kama sijakosea ilikuwa mwaka 1999.

Lissu aliniambia mapambano yake na Barrick yalimsababishia aishi maisha magumu yaliyojaa hofu,Serikali ilimpinga na kusema Lissu alikuwa anasema uongo na kuwagombanisha wawekezaji na wananchi.

Lisu akaniambi alilazimika kufanya mkutano na waandishi wa habari kuelezea tuhuma dhidi ya Barrick,mkutano ule aliufanya muda mfupi kabla hajaondoka kwenda masomoni Nchini Marekani,mkutano ule ulimsababishia ugomvi mkubwa na Serikali ya Awamu ya tatu,aliitwa majina mengi,kubwa lilikuwa mchochezi.

Lissu alipotoka kwenye masomo yake ya shahada ya pili,aliendelea na harakati zake za kupambana na wawekezaji kwenye sekta ya madini.

Lissu aliporudi alikuta kundi kubwa la wananchi wanaoshi pembezoni mwa migodi wakiwa kwenye vifungo baada ya kukutwa na makosa ya uvamizi kwenye migodi,Lissu aliamua kuanza mchakato wa kuwatetea na hata kukata rufaa kwa watu waliokuwa wamewekwa ndani kwa makosa ya kuvamia migodi,makumi kwa mamia ya watu walitetewa bure na kutoka jela kwa utetezi wa Lissu bila malipo,Lisu alipataza sauti kuwa uwekezaji umegeuka kuwa unyama nchini Tanzania.

Harakati zake zilimsababishia ugomvi na serikali pamoja na wawekezaji,mwaka 2011,Baadhi ya wakazi wa Nyamongo waliingia kwenye mgodi kusaka mabaki,wakapogwa Risasi na Polisi na watu wawili nakumbuka walifariki dunia.

Lissu akiwa kwanza ndiyo ameingia bungeni,alikwenda Nyamongo,aliitisha mikutano,familia na wanajamii ya nyamongo,ziligoma kuzika maiti zilizopigwa Risasi.

Lissu akiwa Nyamongo alikamatwa na kuwekwa ndani kwa makosa ya kuwachochea wananchi wawachukie wawekezaji,Lissu aliwekwa ndani akafikishwa mahakamani na baadae kuamriwa asikanyage Nyamongo kwani amekuwa anachochea chuki wananchi wa Tarime wawachukie Barrick,sidhani kama katazo hilo lilifutwa.

Mwaka 2006,jumuiya ya viongozi wa dini nchini hapa ni viongozi wa dini zote na madhehebu yote,nakumbuka mara mbili nilifuatana nao,kwa kushirikiana na Lissu ilizunguka migodi yote nchini kuwatetea wananchi waliokuwa wananyanyaswa na wawekezaji.

Nakumbuka kwenye tema hiyo alikuwemo Shehe Fereji,Askofu Munga,Askofu Mkuu Ruzoka na viongozi wengi,hawa walipaza sauti kuiambia serikai kuhusu wizi na unyama unaofanyika kwenye sekta ya madini nchini.

Mpaka leo nalikumbuka chozi la Aksofu Munga na Shehe Fereji walipofika kwenye mgodi wa RUSU huko Nzega mkoani Tabora baada ya kukuta wananchi wakiteseka na kuishi maisha ya simanzi na umasikini wa kutopea,kwa kila aliyepaza sauti aliitwa mchochezi ana wivu wa maendeleo.

Viongozi wa dini hawa walitafuta wataalam kutoka ndani na nje ili wafanye utafiti wa kisayansi kuhusu mchango wa sekta ya madini nchini.

Walikuwa ni Curtus na Tundu Lissu ndiyo waliozunguka migodi yote nchini na kutoka na ripoti ya kina kuhusu hali ya uwekezaji kwenye sekta ya madini.

Lissu na Curtus walikusanya ushahidi kutoka mgodini,serikalini na kwa wananchi wa kawaida,wakatoka na ripoti iliyoitwa
"THE GOLDEN OPPORTUNITY",ripoti hii waweza ipata mtandaoni,iliandikwa na Lisu huyu ambaye muda huu anateseka kitandani huko Nairobi.

Mwaka 2009,wakati huo nikifanya uchunguzi kuhusu ukweli wa sumu za mti Tigite huko Nyamongo,na hii ni baada ya baadhi ya wakazi wa Nyamongo kubabuka na wengine walipoteza maisha kutokana na kilie kilichodaiwa kuwa ni Sumu,nilipokuwa Nyamongo,kila familia niliyoitembelea,walikuwa wananiambia niwasaidie kumwambie Lissu aende kwani wanakufa na Sumu.

Watu wale walimuona Lisu ndiyo kimbilio lao,mwaka Huo huo,ili kuionesha ushahidi serikali kuwa mgodinwa Barrick umetiririsha sumu kwenye vyanzo vya maji huko Nyamongo,Lisu huyu anayeteseka huko Nairobi muda huu na chama cha wanasheria za mazingira walilazimika kuwasafirisha kwa ndege waathirika wa sumu za mto Tigite.

Lissu alimsafirisha mzee Mwikwabe ambaye mwili wake ulikuwa umebabuka na sumu za mto Tigite,ilikuwa ni usiku kupitia Channel Tena,Lissu akiwa na Mzee Mwikwabe,walijitikeza kwenye mjadala na Lissu akawa anaongea kwa ukali akiiambia Serikali,"Mnataka niwape ushahidi upi ili muamini kuwa huko Nyamongo kuna watu wanakufa kwa sumu zinazotiririshwa na mgodi"

Lisu hakusikilizwa,Mgodi ulikana,Serikali
ilikana,bunge liliunda kamati ,kama sikosei spika wa sasa wakati huo akiwa mwenyekiti wa kamati walikwenda Nyamongo ba baadae wakasema hakuna ushahidi kuwa zile ni sumu.

Nakumbuka siku kamati ilipokuwa Nyamongo,mimi na team yangu tulikuwa Nyamnongo,katika kijiji cha Kewanja,wananchi waliwaambia wabunge wa kamati ya mazingira kuwa kama wanadhani maji hayana sumu wanaguse ama kunywa,hakuna mbunge aliyegusa.

Ni Lissu na baadhi ya waandishi wa habari akiwemo Christopher Gamaina wakati huo akiwa na Gazeti la Mtanzania ndiyo waliosema kuna watu wameungua kwa sumu.

Lissu alisimama na kusema bila hofu kuwa wawekezaji hawa wanaliibia taifa,wanaua watu kwa bunduki na sumu zinazitirirka kwenye vyanzo vya maji,lakini akaitwa mwanaharakati anayetaka wagombanisha wawekezaji na wananchi.

Nakumbuka wakati tunachunguza ukweli wa sumu kwenye mto Tigite,moja ya nyaraka tulizotumia ni Ripoti za Lissu,nakumbuka kwenye makala za uchunguzi huko Geita,tulitumia mapendekezo ya ripoti Lisu na Curtus kuitaka serikali ifanye
mabadiliko ya kisera na kisheria ili watanzania wanufaike na madini,Ripoti ya Lisu ndiyo ilikuwa mwongozo wa nini tufanye?

Najiuliza,mbona Lissu amekuwa mpambanaji wa mali za umma,tangu ubarubaru wake leo anatesema kiasi hiki na hata kudhihakiwa na baadhi ya watu wakati huu akitesema huko Nairobi?

Muda,Ujasiri,kujitoa kwake kupambana na wawekezaji wa Lissu hautoshu wote tunuombee badala ya wengine kumdhihaki?,ni kweli kazi na upambanaji wa Lissu haujulikani?

Pole Lissu,Mungu anajua kazi za akili na mikono yako,naamini utapona Lissu,nayaona maumivu uliyonayo muda huu hapo hospitali,Naamini Utapona,naaamini Mungu anayaona maumivu na machozi.

Maneno toka kwa mashuhuda. Et huyu ndio amekua mpinga accacia kuliko Lissu
 
Wacha umbwa aitwe umbwa,kumuita paka haisadii.Kikwete alikuwa na stara na ndo mana alikosolewa kwa stara.Huyu wa sasa sio binadamu kabisa.Hana huruma,hana utu,hana hekima,hana kauli nzuri,hana heshima wala adabu kwa waliomtangulia,ana matusi,kebehi na jeuri.Sasa kama anatukana wenzie yeye ni nani hasa mpaka asitukanwe?.
 
ninyi mnaanzaje kumkosoa mh rais?wewe Pascal Mayalla umepoteza uzalendo, umeanza kuhongwa na majizi. wewe kama jina lako lilivyo kwa kisukuma ni njaa.wewe unaonekana njaa imekushika sana. unathubutu kumkosoa mheshima rais?tena unaishi kwenye nchi yake?unasema yeye ni bully? unajua rais naweza hata kukuhamisha nchi? unajua kuwa inaweza kuchunguzwa ukagundulika wewe si raia wa nchi hii? unalijua hilo? unajua kuwa hapo ulipo jenga inawezekana kabisa ni eneo la barabara? unapata wapi ujasili wa kumsema hivyo mheshimiwa mtukufu rais?nimeshtuka sana.

"kilichomkuta kibeku na ungo pia kitamkuta"
Mkuu Gu Dume, kwanza asante kwa angalizo hili, nimesema au nimeuliza?. Kumbe rais anaweza kukuhamisha nchi?!, akakupeleka wapi?, yaani wewe ni Mtanzania halafu rais akuhamishe?!, unless kama unamaanisha uhamisho kama ule wa Lissu?, huku ni kumsingizia, hakuna mtu yoyote hata rais, anaweza kukunyang'anya haki zako ya uraia!. Hili la kuchunguzwa na kugundulika mimi sii raia, pia linawezekana, kwa sababu tuna Watanzania wengi, tena wengine ni viongozi, tunawajua kuwa ni Watanzania wenzetu, lakini, kiukweli sii Watanzania!, japo mimi nimezaliwa familia ya Kisukuma, lakini nikichunguzwa ni kweli naweza kukutwa kuwa kumbe ni banyamulenge Fulani, ila nimepose tuu kama Msukuma!. Uchunguzi huu ufanywe kwa Watanzania wote wanaoomba uongozi wa kuchaguliwa!, kuanzia diwani, mbenge hadi..., na hili likifanyika, nakuhakikishia mtashangaa!.

Kuhusu kujenga, bahati nzuri sana, mimi sijajenga, naishi nyumba ya kupanga, upande mzima, pale kwa Mtogole.
Naomba kukuhakikishia mimi namuheshimu sana rais Magufuli, na bandiko hili ni uthibitisho wa hili.

Wanabodi,
Huu ni wito tuu kwa wana jf kuhusu ukosoaji wa Rais wa nchi, Mhe. Dr. John Pombe Joseph Magufuli,
kama kuna mahali rais kama binadamu amekosea, au amefanya ndivyo sivyo, tupaseme kwa unyenyekevu kwa lugha ya heshima na staha, kisha tuweke na ushauri wa the right thing to do, hivyo ukosoaji kwa rais, ufanyike constructively kwa nia njema ya kujenga na sio kubomoa, yaani tufanye "a constructive criticism" hivyo ukosoaji huu utakuwa na nia ya kumsaidia rais wetu kuwa rais bora zaidi na kulisaidia taifa kusonga mbele na sio kurudi nyuma kwa sababu kwa mujibu wa katiba yetu, rais hawezi kukosea ndio maana hawezi kushitakiwa. Rais ana sehemu mbili, rais ni presidential institution hivyo hawezi kufanya kosa lolote ni perfect na kila kauli yake ni sharia, inafuatiwa na utekelezaji tuu, lakini hiyo institution inashikiliwa na mtu anayeitwa John Pombe Joseph Magufuli, huyu ni binadamu, he is a human anaweza kukosea
Paskali
 
Pascal Mayalla usibishe inaweza kabisa ikaonekana wewe ni mtu wa kongo huko kivu katikati ya machafuko ya vita ya wenyewe kwa wenyewe. tena inaweza julikana babu yako ni kutoka sudani au hata syria na ikataikiwa upelekwe huko mpakani ukajitegemee. mbona wengi tu walishawah kuonekana si wazaliwa au si raia wa nchi hii. mimi nmekwambia kama ndugu yako. uchunguzi huwa haudanganyi hasa ukifanywa na serikali tukufu..unaweza kuta babu wa babu yako wa babu yake babu yake wa babu yake wa kipindi kile alikuwa ni mkimbizi na miaka hiyo ya 1120 hakuchukua uraia.so unarudishwa kwenu halafu ndo uombe uraia kwa kufuata process.

huko tandale kwa tumbo unapoishi usije msababishia mwenye nyumba matatizo. unajuaje hajajenga eneo la wazi?au kwenye mkondo wa bahari? au kwenye eneo la barabara? mi nakupa angalizo tu.kuuliza uliza huku angalia sana. maana mdomo uliponza kichwa. rais hakosei..allways he is right. inatakiwa tu uwe unashangilia anachofanya na kusema. yeye ni msema kweli na ni mpenzi wa mungu.. haya usije sema sikusema.

Mkuu Gu Dume, kwanza asante kwa angalizo hili, nimesema au nimeuliza?. Kumbe rais anaweza kukuhamisha nchi?!, akakupeleka wapi?, yaani wewe ni Mtanzania halafu rais akuhamishe?!, unless kama unamaanisha uhamisho kama ule wa Lissu?, huku ni kumsingizia, hakuna mtu yoyote hata rais, anaweza kukunyang'anya haki zako ya uraia!. Hili la kuchunguzwa na kugundulika mimi sii raia, pia linawezekana, kwa sababu tuna Watanzania wengi, tena wengine ni viongozi, tunawajua kuwa ni Watanzania wenzetu, lakini, kiukweli sii Watanzania!, japo mimi nimezaliwa familia ya Kisukuma, lakini nikichunguzwa ni kweli naweza kukutwa kuwa kumbe ni banyamulenge Fulani, ila nimepose tuu kama Msukuma!. Uchunguzi huu ufanywe kwa Watanzania wote wanaoomba uongozi wa kuchaguliwa!, kuanzia diwani, mbenge hadi..., na hili likifanyika, nakuhakikishia mtashangaa!.

Kuhusu kujenga, bahati nzuri sana, mimi sijajenga, naishi nyumba ya kupanga, upande mzima, pale kwa Mtogole.
Naomba kukuhakikishia mimi namuheshimu sana rais Magufuli, na bandiko hili ni uthibitisho wa hili.

Paskali
 
Habari hii ilichapishwa kwenye gazeti la RAI miaka michache iliyopita ikisomeka...

Huyu Ndiye Pombe Magufuli:

- Wasema nyumba 8,000 kauza kwa mkono wake mwenyewe
- Apuuza maonyo ya wataalamu- Mafaili ya Sundi na Musa aliyabeba kwapani

ALIYEKUWA Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, katika Serikali ya awamu ya tatu, aliteka madaraka na kuwa mwenyekiti wa zoezi la kuuza nyumba za serikali ambazo hadi sasa, zimeshauzwa 8,288 imefahamika.

Habari zilizopatikana ndani ya wakala wa Majengo ya Serikali (TBA), zimethibitishia Rai wiki hii kwamba Magufuli alihakikisha anashiriki kama Mwenyekiti katika zoezi zima la kuuza nyumba, ambalo kimsingi lilistahili kusimamiwa na Mtendaji Mkuu wa TBA.

Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vya habari ndani ya TBA, Magufuli alifanya kila aina ya ‘fujo’ katika zoezi la kuuza nyumba hizo, wakati mwingine akibatilisha maamuzi yaliyofanywa na Kamati ya TBA ya kuuza nyumba hizo, akiwapangia watu nyumba kwa utashi wake na wakati mwingine akiwakemea wale wote waliomshauri kinyume na matakwa.

Ni chini ya utaratibu huo, habari zinaeleza kwamba Magufuli, aliyabeba yeye mwenyewe mafaili ya ndugu zake; Musa Magufuli ambaye ni mdogo wake, na Sundi Malomo ambaye ni mzazi mwenzake na kuwalazimisha watendaji wa TBA wafuate matakwa yake katika kuwapatia nyumba ndugu zake hao.

Habari hizo zinaeleza kwamba awali Mtendaji Mkuu wa TBA alimshauri Magufuli kwamba suala la mauzo ya nyumba kwa ndugu zake ni kinyume cha utaratibu. Hata hivyo, imeelezwa kwamba Magufuli alilazimisha huku akisema mdogo wake hana tatizo kwa sababu alikuwa tayari mfanyakazi wa Serikali.

Musa aliajiriwa kwa mkataba wa miezi mitatu, baada ya mwezi mmoja akauziwa nyumba na baada ya miezi miwili akaacha kazi.

“Kwa upande wa Sundi, kwanza ilikuwa Sundi auziwe nyumba moja kwa moja. Lakini Magufuli alipoonywa akashtuka na kusema suala hilo aachiwe yeye mwenyewe. Na ndipo akaibuka na jina la Stanley Manongi kwamba ndiye mnunuzi halisi na baba yake Sundi,” vinasema vyanzo hivyo vya habari, vingine ambavyo vilishiriki moja kwa moja katika mchakato wa uuzaji nyumba hizo.

Habari hizo zinaendelea kueleza kwamba baadaye, Sundi alishtuka akitilia shaka uaminifu wa Manongi, kwamba angeweza kumdhulumu nyumba hiyo.

“Ndipo Magufuli aliibuka na mpango wa Sundi kuwa mtoto wa Manongi na mrithi wake na kisha kwa kuhakikisha kwamba hakuna dhuluma yoyote, mtoto wa Sundi naye akarithishwa na kama mrithi wa pili,” chanzo hicho cha habari kinaeleza.

Chini ya sheria ya Executive Agency Act No. 30 ya mwaka 1997, TBA ilipewa madaraka yote ya kuuza nyumba za Serikali, kujenga nyumba mpya, kuzikarabati zilizopo pamoja na kugawa nyumba za madaraja A, B na C kwa wafanyakazi wa Serikali.

Sheria hiyo inaipa mamlaka ya kipekee ya kufanya shughuli zote bila kuingiliwa na chombo chochote.

Chini ya sheria hiyo, Waziri anaruhusiwa kuteua wajumbe wa bodi ya ushauri watakaomshauri Katibu Mkuu wa Wizara juu ya namna nzuri ya TBA kusimamia mamlaka yake.

Hadi Machi mwaka huu, wajumbe hao walikuwa ni J. Kijazi, E. Lipambila, E. Lugwisha, Msangi, E. Mwakalinga, D. Kisasi, P. Ncheye, F. Werema na A. Bukuku.

Hata hivyo, sheria haitoi nafasi yoyote kwa Waziri kusimamia shughuli za uuzwaji au upangaji wa nyumba za serikali.

Mtendaji Mkuu wa TBA Togolayi Makumba Kimweri, alipoulizwa kupitia kwa Katibu Muhtasi wake, alimwambia mwandishi wa Rai aandike maswali kisha asubiri kuruhusiwa kuingia ndani ya ofisi.

Hata hivyo, baada ya kusubiri kwa muda wa saa moja, mwandishi alipokwenda kuuliza akaambiwa kwamba Kimweri tayari alikwishaondoka ofisini kupitia mlango wa nyuma na asingeweza kurudi ofisini.

Lakini baadhi ya wafanyakazi wa TBA wameiambia Rai kwamba kinachoandikwa kwenye magazeti kuhusu ushiriki wa Magufuli kuuza nyumba za Serikali ni kidogo mno kuliko hali halisi.

Kama ilivyokuwa kwa mdogo wake Musa, waziri Magufuli alishinikiza mtoto wa dada yake anayeitwa James Doto Mgosha auziwe nyumba za serikali kwa kumtengenezea ajira ya muda mfupi katika TANROADS.

Tofauti na Musa, Doto ameuziwa nyumba hiyo kwa jina la mtu mwingine lakini anaishi katika nyumba hiyo, namba 64 iliyopo Kinondoni Flats.

Habari kutoka TBA zinaonyesha jina la mtu mwingine (tunalihifadhi) kuwa ndiye aliyeuziwa nyumba hiyo mtu huyo alipata kupitia utaratibu wa Magufuli kupeleka jina lake kwenye wakala wa majengo na kulazimisha apewe nyumba.

Alipoulizwa kwa njia ya simu, Doto alisema suala la ajira na nyumba waulizwe waliomwajiri na kumpa nyumba. Akakata simu.

Mfanyakazi mwingine alieleza Rai kwamba msichana mwingine (jina tunalihifadhi) akiwa na miezi minne tu kazini alipelekwa na Magufuli katika Wakala wa Majengo akilazimisha auziwe nyumba hata kabla ya kuthibitishwa kazini. Nyumba hiyo iko Block A, Ocean Road.

Hata hivyo, habari hizo zinaeleza kwamba msichana huyo ambaye hadi sasa anaishi na wazazi wake, ameipangisha nyumba hiyo kwa mfanyakazi mmoja wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa na analipwa kwa dola za kimarekani.

“Kuuza nyumba za serikali sawa, lakini kweli katika mtindo huu? Sisi tunaoshiriki kuzikagua na kuziratibu tukiomba hatupati, lakini wengine wanaingia serikalini miezi miwili wanapata nyumba. Na wengine hata si wafanyakazi, wanapata, hii si sahihi, alilalamika mfanyakazi mmoja aliyeandikia Rai kwa njia ya barua pepe.

Hadi Machi mwaka huu Wakala wa Majengo wa Serikali (TBA) walishauza nyumba 8,288 ambazo hata hivyo zilitakiwa kuuzwa kwa watumishi wa serikali.

Katika mauzo hayo, Serikali ilitarajia kupata jumla ya shilingi 60,016,556,439.00. Hata hivyo hadi sasa Serikali imepata shilingi 22,684,108,115.08.

Kwa sasa, Serikali imebakiwa na nyumba 1,098 zinazosimamiwa na TBA. Kati ya hizo, nyumba 692 zimetengwa kwa wafanyakazi wa Serikali, nyumba 675 kama tied quarters, nyumba 111 zinatumika kama Rest House za Serikali, wakati nyumba 40 zinatumika kama state lodges. Nyumba 24 zinatumika kama ofisi na nyingine 29 ni kama karakana na bohari.

SALVA RWEYEMAMU
RAI
Mmmmmmh
 
Pascal Mayalla usibishe inaweza kabisa ikaonekana wewe ni mtu wa kongo huko kivu katikati ya machafuko ya vita ya wenyewe kwa wenyewe. tena inaweza julikana babu yako ni kutoka sudani au hata syria na ikataikiwa upelekwe huko mpakani ukajitegemee. mbona wengi tu walishawah kuonekana si wazaliwa au si raia wa nchi hii. mimi nmekwambia kama ndugu yako. uchunguzi huwa haudanganyi hasa ukifanywa na serikali tukufu..unaweza kuta babu wa babu yako wa babu yake babu yake wa babu yake wa kipindi kile alikuwa ni mkimbizi na miaka hiyo ya 1120 hakuchukua uraia.so unarudishwa kwenu halafu ndo uombe uraia kwa kufuata process.

huko tandale kwa tumbo unapoishi usije msababishia mwenye nyumba matatizo. unajuaje hajajenga eneo la wazi?au kwenye mkondo wa bahari? au kwenye eneo la barabara? mi nakupa angalizo tu.kuuliza uliza huku angalia sana. maana mdomo uliponza kichwa. rais hakosei..allways he is right. inatakiwa tu uwe unashangilia anachofanya na kusema. yeye ni msema kweli na ni mpenzi wa mungu.. haya usije sema sikusema.
Mkuu GuDume, kwanza nilikushukuru kwa angalizo, name pia ni mwana fasihi, hivyo nakusoma vizuri sana in between the lines kuhusu mtukufu wetu, tuko pamoja sana!.

Paskali
 
Tumsaidie Magu, hata km anasema serikali yake ni Tajiri, yeye ni baba hatakiwi kusema hana pesa, yaani aseme hana pesa hadharani alafu na majirani wajue(wajaluo). Baba yetu siyo Dictator ila ni mkali..na mkali kweli.. angekuwa Dictator ingekuwa mkifika mahabusu mnapewa hata sumu ya kuwaua baada ya miaka 2 au 1.

Binadamu yeyote hata akiwa na roho ngumu vp, lakin ukiwa unamtukana, au unambeza, unamkejeli, au dharau anakosa confidence na moyo wake unakwa hauna amani..
Wakati mwingine dada yetu yule wa nje anatukana mambo ya nguoni kbsa kwa Rais, na watu wanafurahi..siyo fair kabsa..huyu naye ni mtu, ana ngozi, ana damu, ana moyo, ni baba, ana watoto, ni mtanzania pia siyo mmarekani pia atachulia poa tu.. No, tunavuka mipaka.
jamii forum inaheshimika sana, tutumie jukwaa hili vzuri kwa kushauri na kukosoa kwa staha kwa sasa bado wanapita pita, inamana wanatuheshimu sana, sasa tutoe nondo siyo uhanarakati.

Tumshauri, tumkosoe kwa staha, he's president, tumsifie akifanya mambo mazuri, tumpe moyo..tumpe support, ni baba yetu mpaka 2020 akipita tena mpka 2025. tuache utimu wa kupinga kila kitu na kusifia kila kitu. let us focus our life, Maisha yetu yana umuhimu sana badala ya kupoteza muda kuwaongela wanasiasa.

Ushauri wenye alternative ndiyo wenye Afya kwa Taifa.

tusiwe emotion, tusiwe washabiki wa watu bali wa hoja, tusiendeshwe na unazi bali itikadi, falsafa na hoja.

NB: MIMI SINA CHAMA, ILA KURA NAPIGA NA HILI NDILO LA MSINGI; KILA JUKWAA NAANDIKA KUTOKANA NA MAHITAJI YA WAKATI.

UJUMBE WA LEO: USHABIKI KWA CHAMA NA WANASIASA HULETA UPOFU WA FIKRA.

Mkuu Chipa, hili la kumkosoa kwa staha, nimelizungumza kwenye uzi huu​

Paskali
Rejea
WanaJF, Je tuisaidie Serikali yetu inaposhindwa au tusubiri ishindwe, tuibeze na kuizomea kuwa haiwezi?
Wito Kwa wana JamiiForums kuhusu ukosoaji wa Rais Magufuli
Rais Magufuli na serikali yake wakosolewe kwa hoja sio kwa viroja - Jicho letu, Star TV
Psychoanalysis: Superiority Complex ni Dalili ya Inferiority Complex!. Maneno Mafupi Vitendo Virefu.
 
Kwa waandishi wa habari kama nyie Mayala hamtaki kuwaambia wananchi ukweli wa mambo ulivyo. Sielewi mnafanya hivi kwa ajili ya kukosa Knowledge au basi ni maamuzi yenu tu?

Mayala na waandishi wetu wa uswahilini mme base sana kwenye stories au informations kuhusu udaku udaku rather than scientific issues. Na mara nyingi habari zinazo husu makosa ya serikali yetu. Informations kama hizo zinuzika vizuri sana kuliko ukweli wa mambo halisi.

Tunajipumbaza sisi wenyewe kwa taarifa za aina hiyo moja mda wote. Lazima muwe mna alternate au ku-varry taarifa mnazozitoa kwa wananchi.

Nakusihi Mayala na waandishi wa habari wenzako wa usawahilini, pamoja na critics zote mnazo zitoa kuhusu serikali yetu, muwe pia mnawaeleza wafuasi wenu kuwa kuna mazuri pia ambayo yanatendeka na serikali yetu. Msipende tu kuwa feed watu mambo mabaya tu ya serikali kama kusimulia ubaya tu wa Magufuli, kana kwamba yeye ni Rais ambaye ni Monster. Mmesahau kuwa huyo Rais amechaguliwa na watanzania kwa misingi ya katiba yetu na ana haki ya kutawala nchi mpaka atakapo gombea tena na kushindwa au kumaliza mihula yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu Maneno Meier
Karibu pande hizi
P
 
Yeye mwenyewe vipi lugha yake anayoitumia kwa wengine ,Vilaza ,katerero ,ukimwi nyinyi ,matetemeko mfano wa hotuba yake bora kabisa ya wahanga wa tetemeko kagera .
 
Wanabodi,
Huu ni wito tuu kwa wana jf kuhusu ukosoaji wa Rais wa nchi, Mhe. Dr. John Pombe Joseph Magufuli, ufanyike kwa kutanguliza mbele uzalendo, kutanguliza mbele utaifa, kutanguliza mbele Taifa la Tanzania kwanza ndipo Magufuli afuate.

Kama kuna mahali rais kama binadamu amekosea, au amefanya ndivyo sivyo, tupaseme kwa unyenyekevu kwa lugha ya heshima na staha, kisha tuweke na ushauri wa the right thing to do, hivyo ukosoaji kwa rais, ufanyike constructively kwa nia njema ya kujenga na sio kubomoa, yaani tufanye "a constructive criticism" hivyo ukosoaji huu utakuwa na nia ya kumsaidia rais wetu kuwa rais bora zaidi na kulisaidia taifa kusonga mbele na sio kurudi nyuma kwa sababu kwa mujibu wa katiba yetu, rais hawezi kukosea ndio maana hawezi kushitakiwa.

Rais ana sehemu mbili, rais ni presidential institution hivyo hawezi kufanya kosa lolote ni perfect na kila kauli yake ni sheria, inafuatiwa na utekelezaji tuu, lakini hiyo institution inashikiliwa na mtu anayeitwa John Pombe Joseph Magufuli, huyu ni binadamu wa kawaida kama sisi wengine wote, he is a human anaweza kukosea. Katika kumkosoa rais, tumkosoe in such a way tusije kujikuta tunakosa uzalendo, badala ya kumkosoa, tumamuaibisha na kujikuta tunajiabisha sisi kama taifa.

Nakiri kupandisha uzi huu kutokana na mchango wa mwana jf huyu

Rais wa nchi ndio kioo cha taifa, ni kama baba wa familia, anahitaji kuheshimiwa.

Hata ikitokea baba mwenye nyumba au baba nyumbani amekosea jambo fulani, anakosolewa kwa heshima kiutu uzima kwa kutumia lugha ya heshima na staha na sio lugha za dharau, kebehi, machukizo au matukano! .

Hata akidanganya haitwi muongo anaitwa hayuko sahihi sana, au ameshauriwa vibaya kwa sababu rais wa nchi hawezi kudanganya, wala hawezi kusema uongo!.

Hata akichelewa kwenye shughuli haambiwi kachelewa maana mkubwa hachelewi bali anakuwa bado hajawasili kutokana na kutingwa na shughuli muhimu, na asipotokea kabisa ni kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu!.

Simaanishi rais Magufuli yeye ni malaika hivyo hawezi kukosea au kufanya makosa, no!, rais Magufuli naye ni binaadamu tuu kama sisi binaadamu wengine wote, na siku zote sisi binaadamu ni viumbe dhaifu, hivyo rais Magufuli naye ana madhaifu yake ikiwemo kuonekana kama ni mtu wa kupenda misifa kupindukia, anapoongea kuna wakati anaonekana kama ni msema hovyo au kama anapayuka, au anaropoka, na katika kufanya maamuzi, kuna wakati anaonekana kama anatenda kwa pupa au papara na baadhi ya maamuzi yake, kuonekana kama ni maamuzi ya chuki au kukurupuka ila kwa vile yeye ndie kiongozi wetu Mkuu, kuna mambo ambayo hatupaswi kuyasema hivyo yalivyo, hata kama ni kweli, ikiwemo kumuita rais ni muongo hata kama ni kweli sometimes anaweza kusema kitu cha uongo hatupaswi kusema rais ni muongo bali rais alikuwa hajashauriwa vizuri au alikuwa ana joke tuu, au anazungumza kwa utani tuu, yaani rais anatania au rais ameteleza tuu ulimi!.

Mfano rais alipohimiza kufyatua tuu watoto kisa atasomesha bure. Tamko hili lilikwenda kinyume cha uzazi wa mpango, hapa rais kiukweli aliropoka na kuteleza ulimi, lakini haiwezi kusemwa kuwa rais karopoka, bali rais alikuwa anatania tuu watani zake, wazaramo!. Siku alipotamka hivyo, hata mimi nilishitushwa na tamko lile ( Rais Kusitisha Uzazi wa Mpango Kwa"Fyatueni Watoto wa Kutosha",Ni Yake au ni ya Wale Wazee wa..?!.)
Lakini baada ya siku mbili tatu, Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu aliibuka na kulitolea ufafanuzi wa kina tamko lile kuwa lilikuwa sii kweli bali rais alikuwa akiwatania tuu watani zake Wazaramo!.

Mfano kwenye hoja ya udikiteta, ni kweli rais Magufuli ni dikiteta fulani hivi, lakini hivyo ndivyo alivyo, na sio kwamba anajifanyisha, ila pia, kwa Tanzania hapa tulipofika, seriously tulihitaji sana mtu mwenye sifa, silika na haiba za udikiteta ndio anaweza kuinyoosha hii nchi ilivyopinda, siku nyingi tumekuwa tukilaani u pole wa Kikwete hadi kumuita "dhaifu" hivyo tumekuwa tukisali kumuomba Mungu atupe kiongozi imara, shupavu, thabiti, ambaye sio mtu wa mchezo mchezo, na kweli hatimaye Mungu akaisikia sala yetu ametupatia Magufuli ambaye ni dikiteta kweli ila sio dikteta mbaya kama Hitler, huyu ni dikiteta mzuri " a benevolent dictator", hivyo badala ya watu kuulaumu huu udikiteta wa rais Magufuli, tunapashwa kumshukuru Mungu kutupatia Magufuli.
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata!. Atakayeleta Fyoko, Ataisoma Namba!

Watu walipoitwa Vila.za, hatukunyamaza, tulitoa ushauri humu.
Wito kwa Baba Jesca: Watendee Haki Kina Jesca Wote Ili Nao Wapate Bahati Kama Jesca!.

Hata alipozungumzia mishahara ya peponi, pia tulitoa ushauri humu
Rais hana mamlaka ya kupunguza mshahara wa mtumishi yeyote

Hata majumbani mwetu hasa majumba ya Kiafrika na Kiswahili, baba ambaye ni mkuu na kichwa cha nyumba, kuna mara kibao anakosea hasa sisi mababa wa Kiafrika tunaofuata mila zetu za kiasili za Kiafrika na mambo yetu yalee ya Uafrika wetu, na pia sio malaika hivyo tuna madhaifu mengi tuu ambayo wamama huyajua huyaona, huyavumilia lakini hawayasemi hadharani.

Kuna namna ya ukosoaji wa heshima na staha wenye lengo la kujenga, a constructive criticism ambao hufanywa in good faith na kuna ukoasoaji wa udhalilishaji wenye lengo la kubomoa ambao hufanywa in bad faith, ridiculously au kumdhalilisha, mkosolewa kwa nia ya kumjengea chuki, achukiwe, kumshushia hadhi na heshima ili aonekane ni mtu wa hovyo, etc huu sio ukosoaji mzuri hata kama ni kweli amekosea, yaani japo is the truth but the motive behind is ill motive.

Simaanishi sasa ndio wote kazi yetu iwe ni moja tuu, kumhusu rais wetu, iwe ni kumuimbia tuu nyimbo za sifa na mapambio, no !, tumkosoe rais Magufuli kwa heshima na kwa kutumia lugha ta staha kwa nia njema kabisa kwa lengo la kumrekebisha na kumsaidia na sio kumdhalilisha.

Tanzania ni yetu sote, sio Tanzania ya Magufuli pekee, na japo CCM ndio chama tawala, haimaanishi Tanzania ni ya CCM, Tanzania sio ya CCM pekee, ni Tanzania ya wote, hivyo we all have a role to play and a responsibility of duty of care kujenga nchi yetu kwa kutanguliza uzalendo na kuweka mbele maslahi ya taifa kwa kujenga na sio kuibomoa na kumjenga rais wetu na sio kumbomoa regardless tunampenda, hatupendi, tulimchagua, hatukumchagua, kama wazalendo wa nchi hii ni lazima kuijenga nchi yetu na kumsaidia rais wetu as a responsibility and a duty of care, kama inavyotokea kuwepo kwa mtoto mwenye ulemavu katika familia, hakuna anayependa ulemavu, lakini imetokea, lazima tumpende and we have a duty of care kumsupport, kumsaidia na kupenda kwa dhati, vivyo hivyo ndivyo ilivyo kwa rais Magufuli, ndie rais wetu wa sasa na hivi alivyo ndivyo alivyo, tumkubali, sio lazima tumpende lakini tunawajibu wa kumpa kila aina ya ushirikiano ili aweze kulitawala vyema taifa letu.

Kuna watu katika kumbonda rais Magufuli, kila siku kazi yao wao ni kuponda tuu, hata akifanya mazuri vipi, wao wataponda tuu, kubeza, kukosoa kila kitu na kumbomoa tuu, na katika kuponda huku, sometimes hujikuta wanaponda over and obove na kuliaibisha taifa letu, na wengine humsifia Nyerere, yaani kumtumia wasifu wa Nyerere as a reference, ila kiukweli ukimwangalia rais Magufuli kwa jicho la karibu, yuko kama Nyerere kwa karibu kila kitu
Magufuli Kama Nyerere:Ni Mtu wa Watu, Hapapasi, Hamung'unyi, Ni Kazi Tuu, Ila Pia,Sio Kama Nyerere!.

Katika kujenga nchi the motive iwe ni kujenga kila kitu ikiwemo kujenga watu akiwemo rais anahitaji kuendelea kujengwa na sio kubomolewa tuu.

Japo nafahamu katika kujenga, kuna sehemu inaweza ikakubidi ubomoe kwanza ndipo ujenge, ubomoaji huo hufanyika kwa makini sana ili usibomoe kusiko husika na kila ubomoaji huo ukifanyika hufuatiwa na ujenzi papo kwa papo! .

Nitapenda kuiona jf ya hivyo, wale waashi mahiri wa jf ambao kazi yao ni kubomoa tuu, wapewe jukumu la kujenga pia sio kila siku wao ni kubomoa tuu, mwisho watapewa sifa ya kuitwa wabomoaji tuu ili hali tuna wajenzi imara na mahiri humu tena waliopitia kozi za uanagenzi kwa wale mahiri kabisa.

Wana jf tuwe wakweli kumhusu rais Magufuli toka ndani ya nafsi zetu sio kwa kuvaa miwani yenye kuona upande mmoja tuu wa mabaya tuu, mapungufu tuu na makosa pekee, bali kama kuna mema pia tuyaone, kama kuna mazuri pia tuyaangazie na kuyasema as encouragement kwa rais wetu mpendwa Mhe Dr John Pombe Joseph Magufuli.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali
Rejea kuhusu ukosoaji. Zifuatazo hapa chini ni baadhi tuu za mada zangu za ukosoaji.

Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria! .
JF Modes, Magufuli ni Rais Wetu, Asiabudiwe, Asiogopwe, Bali Aheshimiwe!.
Katazo la Rais Kusafiri Nje ya Nchi bila Vibali: Je, Halikiuki Haki za Binaadamu?!..
Rais hana mamlaka ya kupunguza mshahara wa mtumishi yeyo
te
Rais Magufuli, Waliomchagua Wanajuta!, Wasiomchagua Wanamshangilia!. Akishika Chama, Watakoma

Magufuli, "Kama Unaona Kazi ya Urais ni Ngumu Kwako, Jiuzulu! ".

Je inawezekana huu ndio mwisho wa utumbuaji wa papara na kukurupuka?! Mkuu kutumbuliwa soon!
Hongera sana Braza Paskali kwa bandiko zuri.

Dhana ya JF kuwa great thinkers ni pamoja na kuja na mijadala yenye akili na yenye tija kwa wakubwa akiwemo namba 1.

Kumheshima Rais wa nchi ni kuiheshimu nchi na utaifa wetu. Rais JPM kwa wengi wetu licha ya kuwa "Mkuu wa Kaya" kwa Tanzania, pia kuna baadhi yetu ana hadhi ya kuwa baba. Maana baba zetu, JPM ni age mate wao.

Kubwa kuliko lote, ili mtu akusikize unapomkosoa, lazima umheshimu yeye kama binadamu na mkuu wa Taasisi ya Urais. Ubinadamu ni kumpa mtu mzima staha na kuheshimu "kiti anachoketi". Uzoefu unaonesha, mtu ukimheshimu na kumpa staha, ni rahisi kukusikiza pale unapompa hoja hata kama hakupenda kuisikiza.

Kuna wakati Mfalme Daudi (Israel) aliua mtu anaitwa Uria kwa kumpeleka mstari wa mbele. Baada ya kufa, Daudi akachukua mke wa Uria.
Nabii alietumwa kumpa ujumbe, hakumpa Mfalme "Daudi za Uso" Busara na hekima, ilimpa nafasi ya kusikizwa na Mkuu wa Nchi.

Tumkosoe Rais anapokea kama binadamu. Ila tunao wajibu wa kiutu uzima wa kutumia busara na akili nyingi maana huyu baba Jeska ndiye baba yetu sote chini ya mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
 
Pascal mayalla unathibitisha kweli wewe ni great thinker. Vijana tunatakiwa walau kuchukua busara zako walau hata nusu tu ili tuweze kufika mbali
 
Back
Top Bottom