Elections 2010 Wito kwa walinzi wetu.

rastaman

Member
Nov 1, 2010
41
0
Jamani kulingana na hali halisi iliyopo hapa nchi, mambo si shawri kabisa.
Mawazo yangu naomba wakuu wa vyombo vyetu vya ulinzi (Hasa walinzi wakuu) wasilichukulie hili swala kiurahisi. hili tatizo ni zito. walipe uzito wake mapema kabla mambo hayajawa mabaya.
Kwa kuwa wote tunaishi hapa hapa Tanzania, nadhani nanyi mnayaona na kuyasikia yanayo zungumzwa na wananchi. mimi si mwana siasa, ila kwa hili tusikuchukile kuwa ni ushabiki wa siasa. yanayosemwa yaangalieni kutoka kona nne na myachambue. Haiwezekani kila mtu amtaje mtoto wako kuwa ni mwizi halafu wewe baba au mama unyamaze kimya tu. itabidi ukae chini utafute sababu kwani nini mtoto wako anatajwa na wengi kuwa mwizi?? hapo lazima ufanye utafiti kujua kama yanayosemwa ni ja kweli au la. haya ni sawa na malalamiko ya wanasiasa na wananchi kwa ujumla wao lalamika kuwa kura zimeibiwa. msiyapuuze. wakuu wetu mnao linda amani yetu. mimi na waamini kuwa na watu wenye hekima kubwa. kwa hiyo tumieni hekima yenu kunusulu matatizo makubwa yanayo weza kuikumba nchi yetu kwa sababu ya watu wachache tu wenye urafi na tamaa ya madaraka. Msikubali kutumiwa kama baadhi ya watu wanavyo lalamika kuwa chombo kimoja cha usalama kinatumiwa na watawala kufanya kazi ya wizi. Ikiwezekana kaani chini na wanasiasa wa pande zote mbili ili kutafuta suluu kabla mambo hayajawa mabaya. hekima mliyopewa na mwenyezi muungu itumieni hiyo kuliokoa taifa la tanzania. kama huyo anaye lalamikiwa kufanya mbinu za kuiba hatakubali.
suluhisho lingine litapatikana baada ya kuwa mumenongea.
Tusisubiri mambo yaende mbali ndo muingilie kati.
chukuweni hatua za haraka.
haya ni mawazo yangu.
 
Back
Top Bottom