Wito kwa Serikali: Msizuie Mkusanyiko wa 6 Desemba mahakamani Kisutu ili Muutumie kama Kipimo cha Wasio na Kazi, Shughuli Rasmi

Muda si mrefu wataanza mazoezi mabarabarani ili kutishia watu, tutaona cinema zote, ila chadema washikilie msimamo wao tupo tayari kumwaga damu zetu ili tukomboe nchi yetu
Hahahahaha

Ww na nani mlio tayari kumwaga damu kwa ajili ya upuuzi wa aina hiyo!! Mm usinihusishe na ujinga huo.

Wangefuata masharti ya dhamana wangefutiwa dhamana? Umewahi kuona mshitakiwa akifutiwa dhamana kwa kufuata masharti ya dhamana?

Mbona kina hohe hahe wakikiuka masharti ya dhamana hufutiwa dhamana na hatushangai, iweje kwa hao wenye uelewa tena watunga sheria?
 
Wapinzani wajaribu kutafuta mahali sahihi pa kubadili lasivyo watateseka/tutateseka kupambania hewa. Katiba inatoa mianya ya mtu/kikundi cha watu wachache kutumia dola vibaya. Taasisi zetu hasa mahakama,bunge na jeshi hazina uhuru wa kutosha kufanya maamuzi. Yote hii nivile mhimili mmoja unaamua uwalipeje? Uwape hela ama la nk.
Ilitakiwa bajeti ikishapigwa fedha za mihimili zitengwe na kukabidhiwa kitengo maalumu cha mhimili husika!kusiwe na mhimili mmoja unaupangia mwingine uwape sh. ngapi na lini. Abaki CAG kuhakiki na serikali kuu kusimamia utekelezaji sanifu.
MTU anakuteua na anaweza kukufukuza,ndiye anayekupangia hela na cheo chako,anaweza kukufunga akijisikia huwezi kuwa huru naye haya siku moja. MF nchi nyingine mishahara ya walimu inalipwa na chama cha walimu baada ya kutengewa fungu na bunge,hili nijambo bora sana pia lifanyike vitengo vingine isipokuwa majeshi yetu tuu. Majaji wasiteuliwe na rais!! Mawaziri waajiriwe sio kuteuliwa kikukomoana ama kiurafiki, MTU alipinga sera za ccm leo NW tena tamisemi?!??! Nchi inaendeshwa kivituko sn ndomaana wananchi wanashabikia vitu vya ujinga kuliko mambo ya msingi...no specific direction!! nami ninaamini vizazi vijavyo vitatushangaa tuliwezaje kuwa wajinga kiasi hiki. Tujielekeze tunapopaswa tusigeuzie mwili kulia huku kichwa kimejielekeza na kufikiria vya kushoto...niujuha
Nadhani hili swala ndo litakua linatatua matatizo ya uhuru wa kitaasisi
 
Thubutuuuuu nakwambia Jumatatu yatatoka matamkooo kibaoooo ,,had RPC wa DODOMA ataongea wakt mkusanyiko utakua Dar
 
Kama mahakama ilikua imemkataza mbowe kutosafiri nje ya nchi kama sehemu ya mashariti ya dhamana kwa nini mahakama isingemnyanganya hati ya kusafiria.
 
Nadhani hili swala ndo litakua linatatua matatizo ya uhuru wa kitaasisi
Wenzetu mf. walimu wakiandamana hawaidai serikali wala Rais wa nchi,wanadai chama cha walimu kihakikishe maslahi yao yanazingatiwa. Fikiria Rais anakwambia nakulipa mshahara nisisikie mpinzani ameshinda unadhani utafanyaje zaidi ya kuwafyekelea mbali,vyuo vikuu maprof. wanaogopa kumkosoa vile yeye ndiye anayewalipa!! Kifupi tumemfanya yeye ndiyo mwanaume (BABA) nasisi ni vivulana (VITOTO). Anakusanyiwa pesa zetu na kuamua anavyotaka yeye kama ni kujenga maghorofa kwao sawa...Huu ni ujinga wa hali ya juu kama enzi za utumwa na wapambe wao wakiafrika!! Kwanini tunashindwa kujitambua?? Ndiyo maana hatuendelei na hatutoendelea sana tutapigana mavita kijinga.
 
Wanabodi,

Leo ni Jumapili, siku ya mapumziko, wa kusali tutasali na wa kumpumzika tutapumzika huku tukisemezana na kushaurina haya na yale kwa mustakabali mwema wa taifa letu. Kwa saa hizi bado sijaamua leo nitasali wapi, maana siku huwa zinatolewa taarifa baadhi ya watu watasali wapi, hivyo sisi waandishi ndio tunakwenda kusali hapo na kuwaletea taarifa za ibada. Siku hizi hata ratiba tuu za sala ambazo ni ratiba binafsi, tunazitolea press release, leo fulani kahudhuria ibada ya Jumapili kanisa fulani.

Ninachotaka tusemezane Jumapili ya leo ni kuhusu tangazo la Chadema imeitisha mkusanyiko wa wanachama wake nchi mzima kukusanyika Mahakama ya Kisutu siku ya tarehe 6 Desemba, 2018 ili kusikiliza kesi ya Mwenyekiti wake, na wanachama wengine itakayotajwa siku hiyo kama ilivyoripotiwa hapa na mwana jf huyu Mathias Raymond Nyakapala
CHADEMA WAITA WANACHAMA NCHI NZIMA TAREHE 6-desemba-2018 - JamiiForums

Mkuu Mathias Raymond Nyakapala, kwanza asante kwa taarifa hii,

Japo siungi mkono kitendo cha Mwenyekiti wa Chadema, Mhe. Freeman Mbowe na Mbunge Esta Matiko kufutiwa dhamana, kwa sababu lengo la mtu kushikiliwa mahabusu no ili asitoroke kujibu mashitaka yanayomkabili, the common sense logical inaelekeza mtu kuwa Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani Tanzania, hiyo pekee tuu ni dhamana tosha, na Mbowe sio Mwenyekiti tuu wa Chadema bali pia ni Mbunge wa Bunge la JMT, hii pia ni dhamana tosha, sasa kwa kesi hii ambayo haina kichwa wala miguu, Mwenyekiti wa chama na Mbunge akimbie wapi, akimbie nini?!.

Ipo haja ya kufanya mapitio ya sheria zetu kuhusu haki ya dhamana na sifa za mtu kujidhamini mwenyewe na masherti ya dhamana.

Pili nawaomba sana sio tuu wana Chadema bali sisi Watanzania kwa ujumla wetu tujenge utamaduni wa kuheshimu sheria bila shuruti, sheria ni msumeno inakata kote kote. Kama shuruti la dhamana ya Mbowe ni pamoja na kutokusafiri nje ya nchi bila ya kibali cha Mahakama, na Mbowe akasafiri bila kibali hicho, huku ni kukiuka masharti ya dhamana yake, hivyo Mbowe akiadhibiwa kwa kufutiwa dhamana yake sio kuonewa. Sheria ni sheria.

Kuhusu hili la watu kukaa mahabusu, naiomba sana serikali yetu tena hapa naipigia hadi magoti kwa unyenyekevu, isitake pride ya kuwakomoa raia wake wenye tuhuma tuu kwa kuwasweka mahabusu. Serikali inayofurahia rais wake kuteseka ni barbarian, au barbaric. Viongozi wanao ona raha watu kusota mahabusu, hawa ni viongozi ma sadist's.

Kule Arusha kuna wakili kijana Midian Mwale na wakili mwenzake Ojare, wako wanaozea mahabusu huu sasa ni mwaka wa 7 unakwenda mwaka 8 kesi haijaanza kusikilizwa!.

Pale Keko the former Commissioner General wa TRA, Harry Kitlya anakwenda mwaka wa 3!. Kuna kina Rugemalila, Peter Noni, Dr. Ringo Tenga, Jamal Malinzi na wengine wengi with names or no names, wako ndani ya mahabusu kwa vipindi virefu bila kesi zao kusikilizwa, wengine hata wakikutwa na hatia, adhabu zao ni za vifungo vya miezi 6!. Mfano Mwale akakutwa hana hatia, nani atamfidia hiyo miaka 8 ya mahabusu?.

Kuna kinaitwa karma, wito kwa serikali yetu iache kujitengenezea a bad karma kwa mateso ya raia yake kwa kuwasweka mahabusu na kujisikia furaha. Karma always hits back, tusijitafutie majanga kwa vitu vinavyoepukika.

Kufuatia wito huu wa Chadema kwa wanachama wao, na kufuatia tabia ya serikali Ku panic na vitu vidogo vidogo ambavyo havipo, kama ilivyopanic kwenye yale maandamano ya Mange, huu wito kwa serikali yetu, this time isipanic na wito huu.

Naiomba serikali kupitia jeshi letu la polisi, isizuie mkusanyiko huo kwa sababu, kwanza ni haki kwa mtu yoyote, kujitokeza mahakamani kusikiliza kesi yoyote inayo mhusu, hivyo ni haki kwa wana Chadema nchi mzima kukusanyika na kujitokeza kwa wingi kusikiliza kesi ya Mwenyekiti wao ili kuijua hatma yake.

The motive behind mkusanyiko huo ni kusikiliza tuu kesi ya kina Mbowe, naiomba sana serikali yetu isiibuke na motives nyingine zozote za kubuni kutoka taarifa za kiinteligensia za mifukoni ili kujenga uhalali wa kuyazuia.

Kama ni kweli Chadema nchi mzima watajitokeza kwa wingi hapo Kisutu hiyo tarehe 6 Desemba, it's obviously eneo la Mahakama ya Kisutu litakuwa halitoshi, lakini hii excuse ya eneo ndogo, isitumike kama kigezo cha kupiga maarufuku mkusanyiko huo.

Badala yake IGP Kamanda Sirro, atoe vijana wake wa kutosha na kuwapanga pale Mahakama ya Kisutu na maeneo ya jirani, kwa kazi moja tuu ya kuwapanga vizuri wana Chadema ili hapo Kisutu patoshe.

Ikitokea wana Chadema nchi mzima kuitikia wito huo na wakajitokeza kwa wingi mpaka aneo la Mahakama ya Kisutu pakawa hapatoshi, then Jeshi la polisi liwazue Wanachadema wasizidi kuingia, bali wakakusanyike eneo la wazi la karibu ambapo ni vile viwanja vya Gymkhana, na bado wakizidi kuongezeka, wawapange eneo la wazi la pwani ya Ocean Rd, (Barak Obama) Rd, kuelekea Feri kuna eneo kubwa tuu la kutosha.

Lengo la kuiomba serikali yetu isizuie mkusanyiko huo kwanza ni kutimiza takwa la kikatiba la freedom of association, freedom of movement, na lawful assembly.

Lakini pia idara nyingine za serikali kuutumia mkusanyiko huo kufanyia several social researchers kama ni kwa kiasi gani watu hawana kazi, kiasi
cha kujitokeza kwa wingi kwenda kusikiliza kesi kwenye hatua ya mention tuu, yaani kutajwa, ingekuwa upepelezi umekamilika na kesi sasa umefikia hatua ya kusikiliza, hapo ndio inge make sense Wana Chadema waitwe kujitokeza kwa wingi kwenda kusikiliza, lakini kesi iko kwenye hatua ya kutajwa tuu, halafu wana Chadema nchi mzima waitwe kujitokeza kuja kusikiliza mention, then watakao kuja ni wale tuu wasio na kazi au shughuli maalum ya kufanya kuendesha maisha yao.

Pia watu wa political science researchers wautumie mkusanyiko huo kupima kuendelea kukubaka kwa Chadema, licha ya kazi nzuri ya rais Magufuli. Hii ni kufuatia hama hama ya viongozi wa Chadema kuhamia CCM, usikute wanachama na wafuasi wa Chadema karibu wote wamehamia CCM kimya kimya kuunga mkono juhudi za rais Magufuli, hivyo wanapoitisha nchi mzima, usikute watakao jitokeza, hata Kisutu isijae, then watumie matokeo ya utafiti huu kuthibitisha Chadema kwisha kazi, wamshauri tuu rais Magufuli, sasa aruhusu maandamano na mikutano ya vyama vya siasa nchi mzima, muone turn out, hivyo kupunguza nchi yetu na rais wetu kupigiwa kelele kuwa anaminya demokrasia.

Tena kwenye mkusanyiko huo eneo ya bahari Kyle upande wa nyuma wa Feri, na kwa vile hauna miti ya vivuli, huruma ikiwaingia, watu kukusanyika juani, mnaweza hata kuwafungulia yale mageti na kuwakaribisha watu kumpumzika ndani ya uzio wa ule ukuta mnene, kwenye vivuli vingi, na baada ya kumalizika kutajwa kwa hiyo kesi, kwa walio nje, kule viwanja vya Gymkhana, wasisitizwe kusogea ndani ya uzio wa ule ukuta mnene, muwakaribishe viongozi wa Chadema kuwahutubia kwa kuwaazima Ile mobile PA, mnaweza msiamini umati wote kutangaza kuunga mkono juhudi za rais Magufuli na kutangaza kuhama Chadema na kuhamia CCM.

Mkusanyiko huo utatumiwa na watu wa Mahakama kupima public interest ya kesi hiyo, hivyo kama watu ni wengi eneo la Mahakama ya Kisutu halitoshi, next mention Mahakama ihamie uwanja wa taifa. Sheria, kanuni na taratibu zinaruhusu eneo lolote kugeuzwa chumba cha Mahakama, ikionekana kesi ya Mbowe ime draw national public interest hadi watu nchi mzima kukusanyika kuja kuisikiliza, then ili watu watoshe, inaweza ikaamuliwa iwe inasikiliziwa uwanja wa taifa.

Lengo la hatua hii ni kufanya transformation kwenye changing attitudes and mindset kuwaza mema, kuwa positive, na positive attitude, watu wakisema wanakusanyika kwa ajili ya jambo fulani, waacheni wakusanyike, wapatieni ulinzi, na kila kesi ikitajwa wawe wanakuja.

Nawatakia Jumapili Njema
Paskali
Viwanja vya mahakama vitajaa defender kila mahali na askari wenye mitutu watajaaa kila kona.

Maandamano ya Mange yalikuwa mfano tosha wa vitisho vya dola kwa raia.
Yes hili ni jambo la kawaida kulinda amani, kuhakikisha kuna ulinzi wa kutosha na hali ya amani, utulivu na usalama.
P
 
Sijaunga mkono mbowe kufutiwa dhamana, mambo mengine tunayakuza na kuonekana hatuna demokrasia na tunakiuka haki za binadamu, let him go free!
Mkuu Saguda, maadam kulikuwa na masherti ya dhamana, na yamekiukwa, why not Mbowe au yeye ni soo special?.
P
 
Back
Top Bottom