Wito kwa Rais Kikwete

Wito kwa Rais Kikwete

Magezi

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2008
Posts
3,359
Reaction score
704
Mh. Rais nadhani ni muda mwafaka wa kuwafunga gerezani wote waliohusika na mkataba tata wa TRL na ktk hili uanze na aliyekuwa waziri wa miundo mbinu bw. chenge, katibu mkuu wake, na wakurugenzi, waziri wa fedha na maafisa wa hazina.

Kwa nini unaogopoa kuchukua hatua huku uchumi wa nchi unavurugwa na mikataba ya kijinga namna hiyo? Tumekubali ya richmonduli, EPA, Kagoda, Meremeta, deep green, mwananchi gold, kiwira n.k. Sasa wewe kama rais huyaoni haya kwamba yanaangamiza nchi??

Kitu kingine cha wewe rais kujiuliza ni kwa nini wafanyakazi karibu wote kwa makampuni ya kihindi wanalalamika kila siku? Na maisha na afya zao ni mbovu? Hujiulizi ni kwa nini?

Kwa ushauri wangu ni kosa kubwa kuingia mkataba na kampuni za kihindi kwani hata kwao india wanafanya madudu mengi tu na wanakwepa kodi lakini kwa sasa serikali mjini New Delhi imekuwa na sheria kali sana ndo maana kwa miaka kama 20 sasa india imeweza kupiga hatua lakini bado sana.

Nahitimisha kwa kusema nataka wote waliohusika na uhuni wa TRL/Rites wafungwe jela haraka.
 
Salva Rweyemamu tafadhali fikisha ujumbe huu kwa Mh Kikwete na mshauri aufanyie kazi.
 
Kwa nini afikishe Salva Rweyemamu....Fikisha wewe MAGEZI si muheshimiwa rais alishatoa namba zake za simu? Sasa mbona unamwambia Rweyemamu?
 
ujumbe murua kwa JK; ataupata tu
 
Back
Top Bottom