Wito kwa Mh Sugu: Barabara mbovu Mbeya

Wito kwa Mh Sugu: Barabara mbovu Mbeya

Kiufupi nimeshakata tamaa na Sugu..

Kashindwa kushughulikia Suala la Soko La Mwanjelwa..Hapo sina imani nae tena..

Soko linaelekea kuwa Machinga Complex kwa uwiano wa kufeli
 
Pesa za kuendeleza jimbo anatumia kujiendeleza, poiliho posho za enzi zile hakuna. Msubirini ikifika June,2020 atawatengenezea na itaharibika tena Nov,2020. Ndio mtazidi kumuita raisi wa huko
Tuache politik, kazi yake kama mbunge ni kupiga makelele juu ya kero zozote zilizoko jimboni mwake ili hatimaye serikali isikie na ilifanyie kazi. Kwa vyovyote vile si sawa kutumia pesa yake hata kama angekuwa nazo.
 
mh Sugu heshima kwako HE president wa Mbeya.

sikumbuki kusikia au kusoma mahala kokote siku za karibuni kama umeshaiwashia mamlaka yenye dhamana ya barabara kuhusiana na hiki kipande cha barabara ya Tunduma, kuanzia Forest hadi Nzovwe ambacho kimevurugwa vurugwa na kimekuwa kero kubwa kwa watumiaji.

ikumbukwe kuwa hii barabara ni sehemu ya Trans-African Highway 4 (TAH 4), inayounganisha majiji ya Cairo na Capetown (Cairo–Gaborone–(Pretoria/Cape Town) Highway).

ni fedheha kuona sehemu ya barabara hii maarufu na muhimu barani Afrika inakuwa mbovu kiasi hiki tena sehemu hiyo ikiwa ndani ya jiji lako la (nchi yako ya) Mbeya.

wananchi wanategemea kusikia ukilipigia kelele hili huko bungeni kwa nguvu zote!
Swali tu hiyo bara bara ipo chini ya nani halmashauri au serikali kuu jibu ipo chini ya serikali kuu kwaiyo acha msumbua mbunge nenda tanroad ukawaulize
 
Tuache politik, kazi yake kama mbunge ni kupiga makelele juu ya kero zozote zilizoko jimboni mwake ili hatimaye serikali isikie na ilifanyie kazi. Kwa vyovyote vile si sawa kutumia pesa yake hata kama angekuwa nazo.

Pesa za maendeleo ya jimboni haujui kuwa wanapewa pia au!? Inabaki kucheza na akili za wapiga kura tu watajiju nae. Wengine hata madarasa wanajenga au kurekebisha wanafunzi wasome vizuri.

Nipitie hukooooo
 
Swali tu hiyo bara bara ipo chini ya nani halmashauri au serikali kuu jibu ipo chini ya serikali kuu kwaiyo acha msumbua mbunge nenda tanroad ukawaulize
aisee!!!
 
Tanroad wanahusika sio sugu
mkuu, kwa hiyo sisi wananchi tukalalamike wenyewe "Tanroad"?
huoni kuwa njia sahihi kwa sisi kulalamika "Tanroad" ni kupitia bungeni ambako serekali ndiko inakowajibishwa?

huu wito kwa mh Sugu niliyempa kura yangu 2015 ni wa kumkumbusha tu ili atekeleze jambo hili ambalo ni moja ya maeneo ambayo mbunge anaweza ku-score credit kama serekali ita-respond positively. nashangaa wengine wanadhani kufanya hivi ni kumponda au kumsumbua mh Sugu. it's very sad!
 
mkuu that's the point.
tunataka apige kelele ili serekali ikili yenyewe hivyo. vinginevyo wananchi wanaweza kumchukulia kama ni hajali vile, ingawa deep down najua naye anakereka!
Kuishi kwa kupiga kelele nasikia ndiyo kazi ya mbunge
 
Back
Top Bottom