Wito kwa JK: Jenga Serengeti Highway na Fast speed Rail | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wito kwa JK: Jenga Serengeti Highway na Fast speed Rail

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Tinker, Mar 3, 2012.

 1. T

  Tinker Member

  #1
  Mar 3, 2012
  Joined: Dec 30, 2011
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wale wanamazingira wa Wakenya waliongoza kupinga tusijenge barabara ya serengeti na cha ajabu serikali yetu ikafyta mkia

  leo wamezindua mradi wa bandari mpya ya lami wenye madhara makubwa zaidi kule Lamu na barabara kuelekea Ethiopia na Sudan.

  Inasemakana \ni mradi mkubwa kuliko yote Africa na hakuna alitetia neno juu ya mazingira

  pia wameamua kujenga Airport karibu na mlima kilimanjaro upande wa Kenya ili waiue kabisaa airport ya KIA

  Sasa cha kujiuliza wale wazalendo wanaopenda maendeleo ya WaTanzania wako wapi?

  Nashauri:

  JK fanya maamuzi kama kiongozi wa China Wen Jianbao na idhinisha not only barabara bali option ya high speed rail huko serengeti.

  Kama kuna mtu hapendi ahame nchi akaishi Kenya
   
 2. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #2
  Mar 3, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,515
  Likes Received: 5,650
  Trophy Points: 280
  Naah my fellow Tanzanian!!
   
 3. Wacha

  Wacha JF-Expert Member

  #3
  Mar 3, 2012
  Joined: Nov 23, 2006
  Messages: 856
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Huu wito unatoa kwa nani? Msaliti aliyeiba kura ama?
   
 4. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #4
  Mar 3, 2012
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Acha wakenya waendelee tu bana,..hapa naona una twanga maji
  kwenye kinu ikisubiri yalainike.

  Watanzania ni hatuna akili na tutabaki hivo milele.PERIOD.....
   
 5. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #5
  Mar 3, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  It is very unfortunately.....................
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Mar 3, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kama viongozi wetu walishindwa kujitetea na kutetea uamuzi wao wakabakia kujibembeleza mbele ya wakubwa kosa la nani? Hivi watu wanajua jinsi tulivyojenga Reli ya Tazara; mnafikiria kweli leo tungeweza kujenga hiyo reli - ikapita mikumi n.k ?
   
 7. T

  Tinker Member

  #7
  Mar 3, 2012
  Joined: Dec 30, 2011
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa kaka tufanyeje?

  Nchi tunaipenda na tukiwa nje tunaitetea kwa nguvu zote tena mpaka tunataka kurusha ngumi

  Lakini situation on the ground ndio hii

  sasa tufanyeje?

  Naomba utupe mwongozo kaka. Hii patriotism inasaidia nini wakati the game has been rigged ?
   
 8. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #8
  Mar 3, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,576
  Likes Received: 18,549
  Trophy Points: 280
  Tinker, jina lako limenikumbusha "Tinker Tailor Soldier Spy" ya Le Carre!. Patriotism peke yake, haitoshi!. Welcome to ground zero and fight from within!.
   
 9. Kakati

  Kakati Senior Member

  #9
  Mar 3, 2012
  Joined: Apr 11, 2009
  Messages: 151
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Tusikate tamaa. Nchi yetu ni znuri naninatuhutaji.
   
 10. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #10
  Mar 3, 2012
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,972
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Badala ya kumshauri afanye mambo ya maana wewe unamshauri afanye mambo ya ajabu ili azidi kujiharibia. Ama kweli watu mmemchoka huyu jamaa.
   
 11. M

  MALAGASHIMBA Member

  #11
  Mar 3, 2012
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 71
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Hashauriki huyo ndugu yako.
   
 12. S

  Stuxnet JF-Expert Member

  #12
  Mar 3, 2012
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,016
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Kwenye maeneo kama haya ndipo huwa namkumbuka Edward Lowassa kama mtendaji mwenye mapenzi na nchi yake. Mutanisamehe wanasiasa kwa vile mimi sina ushabiki wa upande wowote ila nakumbuka alivyoongoza mapambano ya kupasua ziwa Victoria kwa ajili ya kupeleka maji Kahama na Shinyanga, wilaya zenye utajiri wa madini lakini zilikuwa zina kabiliwa na ukame.
  Lowassa kwa kuungwa mkono na Rais wake Mkapa walipindua vipengele vya mkataba wa kikoloni wa mwaka 1929 ambao ulikuwa unasema maji ya ziwa Victoria yaelekee Misri tu na nchi zingine hazikuwa na haki ya kuyatumia.

  Kwangu mimi hili swala kwa mtu kama Lowassa nina uhakika kufika leo angekuwa anakaribia kumaliza ujenzi wa barabara. Haiingii akilini kuona watanzania wenzetu kwenye maeneo yanayozunguka Serengeti waendelee kuishi kwenye lindi la umaskini uliotopea eti kwa kuwa hawana barabara ya lami na eti kwa vile wana mazingira uchwara wanadai barabara itawasumbua wanyama. Ni Tanzania tu katika dunia hii ambako mnyama ni bota kuliko binadamiu, ni Tanzania tu ambako Chura wa Kihansi ni bora kuliko binadamu. Hawa wana mazingira wanaotumia kivuli cha NGO wanamtumikia nani, nafikiri wanaitumikia Kenya kwa vi bakshishi aanavyopewa na mabwana zao.

  Kibaiolojia wanyama wana tabia ya adaptation to sorrounding environment na ndiyo maana kwenye mbuga ya Mikiumi, barabara ipo oinapita, reli ipo na wanyama wapo. Kwa hiyo hata Serengeti wanyama wataizoea.

  Hili ni swala la mustakabali wa maslahi ya Taifa, fusikae mahali tukaendeshwa na masilahi ya wa Kenya ambao wamedungua vitawi vyao vya NGO ili vipaze sauti wakati nchi yetu inademadema kwenye maendeleo.

  Halafu tunajiuliza kwa nini nchi yetu maskini! Wakati raslimali zilizopo Serengeti zinaendelea kulala!! Wake up Tanzanians
   
 13. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #13
  Mar 3, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 361
  Trophy Points: 180
  Mkuu umenikumbusha mbali! Wananchi wa Mkoa Kigoma wamekosa umeme wa uhakika awamu ya kwanza kutoka maporomoko ya mto Malagarasi eti kuna samaki/vyura adimu duniani! Mradi huo ungekuwa Kenya isingekuwa "issue".
   
 14. H

  Huihui2 JF-Expert Member

  #14
  Mar 3, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 395
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Mkuu stuxnet you have made my day, umesema yote with feelings, I wish Mizengo Pinda ataiona hiyo kwa vile Inasemekana huwa anatembeleaga humu jamvini
   
 15. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #15
  Mar 3, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,858
  Likes Received: 4,537
  Trophy Points: 280
  Mkuu hapo sio kweli. Kama ungejua madhara wanayopata wanyama wa Mikumi kutokana na uwepo wa hiyo barabara,husingeandika hayo juu. Wanyama wengi wanakufa sana kutokana na uwepo wa barabara hiyo na kutokana na raia kutozingatia sheria na alama za kwenye kipande cha barabara kinachopita kwenye hifadhi.

  Kwenye suala la wanyama kuzoea au kuadapt mazingira fulani,ni kweli. Ila kumbuka wao pia wana tolerance limit ambayo ikipitwa ndiyo mambo ya extinction au kuwekwa katika Species Red List ya IUCN. Kumbuka wanyama wengi duniani wametoweka baada ya tolerance limits zao kupitwa kwa kiasi kikubwa. Mfano maarufu ni Dinosaurs.

  Hapa simaanishi kuwatetea wanyama na kuwasahau wanadamu,la hasha. Ninachokitetea na uwepo wa win-win situation kwa sisi wanadamu na kwa wanyamapori. Kwani kila upande unategemea upande mwingine kwa kiwango kikubwa. Wanyamapori wanatupa mapato na aesthetic values. Nao wanatutegemea sisi kwa survival yao kwa njia ya kuwatunya na kuwajali.

  Hivyo ni vyema kufikiria pande zote.
   
 16. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #16
  Mar 3, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,858
  Likes Received: 4,537
  Trophy Points: 280
  Mkuu si kweli. Huo mradi umepigiwa sana kelele na wanamazingira. Kama ulisikia jana kwenye hotuba za Kibaki na Raila waliongelea suala la kelele za wanamazingira juu ya mradi huo. Kwani mradi umeonekana utasumbua Lamu marine ecosystem. Lakini kupitia tathmini za madhara ya mradi katika mazingira,kumependekezwa njia ya kupunguza madhara hayo.

  Unajua katika kufanya maendeleo uharibifu wa mazingira haukwepeki. Ila kinachofanyika kupitia tathmini za athari za mazingira na jamii,ni kutoa mapendekezo ya namna gani maendeleo hayo yatazingatia angalau kupunguza madhara katika mazingira na jamii husika. Yaani kuweka mazingira ya win-win kati ya mazingira na maendeleo.

  Sasa katika mradi wa ujenzi wa barabara ya kupita Serengeti,tathmini zilizofanyika zilionyesha uwepo wa madhara makubwa pindi barabara ingejengwa kama ilivyopendekezwa. Lakini kama kawaida tathmini zikapendekeza namna ya kupunguza madhara katika mazingira kwa kupendekeza mradi kutumia route nyingine,ambayo hata kiuchumi ilikua more viable(ikimaanisha ingeleta more trickle down effects) kuliko kupitisha ndani ya hifadhi.
  Ila tatizo la hilo pendekezo ni kwamba gharama za mradi zingeongezeka kidogo. Lakini in long run economic benefits za hiyo route mpya zingekuwa kubwa na pay back the initial costs.

  Tatizo likaja kwamba,hiyo barabara ni ahadi ya uchaguzi na njia ya kupata kura kwa serikali ya CCM,hivyo kubadili route na kuipitisha mahala pengine kunakua na utata. Hili ndilo tatizo linaloimaliza TZ. Kila jambo linakua politicised,wakati utaalamu unapokua unahitajika.

  Ni lazima tuwe na win-win situations kwa kila upande. La sivyo kukiwa na win-lose situations,mradi utakua sio endelevu na wenye manufaa ya muda mrefu.
   
 17. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #17
  Mar 3, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Kumbe welfare ya wanyama ni bora kuliko binaadamu.
  TAZARA imepita Selous na Mikumi mpaka leo wanyama wapo!
  Ilo la Vyura uko malagalasi limenichosha mbona Kihansi kuna vyura na kuna bwawa.
  Issue sio kuacha mradi bali go for both plans to proceed with the project and conserve the environment.KIHANSI tumeweza uko why tushindwe
   
 18. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #18
  Mar 3, 2012
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,547
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  Kuna umuhimu hiyo barabara kujengwa , utanyanyua uchumi sana kwa watu wa kanda hiyo sana . Ila wakenya wanawachezea wa tz kama watoto wao . Sijui tiss wapo wapi ? Lowassa angekuwepo huu ujinga usingekuwepo.
   
 19. elmagnifico

  elmagnifico JF-Expert Member

  #19
  Mar 3, 2012
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 7,913
  Likes Received: 7,458
  Trophy Points: 280
  jamani mimi nimesoma environmental economics and policy. Na katika shuguli yoyote ya kiuchumi lazima kuna invironmental impact kwakuwa economic development inatokea at the expense of environment huwezi kulikwepa hilo.
  Hivyo basi katika project kubwa kama hizo inabidi ifanyike environmental analysis kupima cost benefits za mradi na mazingira ili kupata kipi bora kati kufanyika huo mradi au kutofanyika ili kutunza mazingira au kama kuna uwezekano wa kutumia njia mbadala ifuatwe.
  Tatizo kubwa ninalo liona hapa kwetu tanzania ni watu kuingiliana katika field yani mambo mengi yamekuwa kisiasa zaidi. Acha kila mtaalamu katika field yake a play his/her role ni mwisho itapatikana best way.
  Huwezi fanya lolote kwenye mazingira bila kudisturb ecosystem balance lakini tunacho angalia ni njia zipi zitapunguza uharibifu na pia cost benedits is what matters zaidi
   
 20. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #20
  Mar 3, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Kama issue ni wanyama kufa tuweke barabara then tuangalie tufanyeje magari yawe yanaenda kwa mwendo wa kawaida yafikapo hayo maeneo. La sivyo sisi tutabaki ***** mtozeni
   
Loading...