Salam waugwana wa jukwaa hili pendwa.
Nimekuwa mtumiaji wa simu ya mkononi kwa muda mrefu tu pia badhii ya vifaa kama kompyuta n.k. Sasa kifaa kama simu ikiwa kitatunzwa vizuri bila kupata misukosuko yoyote hutumika kwa muda mrefu sana.
Naomba kwa mtu yoyote anaejua vizuri tofauti ya vifaa hivi:-
Simu hutoa wino muda wote unapoandika ujumbe,namba na mambo kadhaa wa kadhaa lakini wino wake huwa hauishi.
Fax,Photocopy,Printer hizi zinawekwa wino na wino wake baada ya matumizi mengi huisha na kuhitaji wino mwingine ili kazi iweze kuendelea kama zamani.
Wataalam naomba ufafanuzi ili nami nielewe utofauti uliopo.