Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Aliyekuwa rais Nelson Mandela na mkewe wa zamani Winnie Mandela
Aliyekuwa mkewe Nelson Mandela amepoteza harakati zake za kutaka kurithi makao yalio mashambani ya rais huyo wa zamani wa taifa la Afrika Kusini.
Mahakama kuu ya Mthatha ilipuuzilia mbali ombi la Winnie madikizela mandela na kumtaka alipe gharama zote za kesi hiyo.
Alihoji kwamba nyumba hiyo ya kijiji cha Qunu ambapo Mandela alihudumu mda wake mrefu hadi kifo chake mwaka 2013,ni mali yake kulingana na sheria za kitamaduni.
Nelson Mandela na Winnie Mandela
Bw Mandela ambaye alikuwa rais wa kwanza mweusi wa taifa la Afrika Kusini mwaka 1994 aliipatia familia yake nyumba hiyo.
Alimpa talaka Bi Madikizela Mandela mwaka 19196 baada ya miaka 38 ya ndoa.Serikali ilipinga harakati za bi Madikizela kurithi nyumba hiyo.
Chanzo: BBC Swahili