Wingu na Mbingu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wingu na Mbingu

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Ms Judith, Jun 23, 2011.

 1. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #1
  Jun 23, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  1.
  Nimepata wa thamani, ni hakika si majungu,

  Mwingine sitatamani, nimefunga moyo wangu,
  Sikupotea ramani, nimezikubali pingu,
  Mimi nawe Naimani, ni kama wingu na mbingu!
  2.
  Kila nionapo wingu, sikosi kuona mbingu,
  Huwezi ingia mbingu, bila liingia wingu,
  Wingu liko na mbingu, mbingu zina mawingu,
  Mimi nawe Naimani, ni kama wingu na mbingu!
  3.
  Hayawi hayawi yawa, thelathini siku zawa
  Sio nyingi kama chawa, zi nyepesi kama buwa,
  Kwa sala na zote duwa, maombi yamejibiwa,
  Mimi nawe Naimani, ni kama wingu na mbingu!
  4.
  Tangu tulipozianza, ndoto za baba na mama,
  Ni mengi tumejifunza, tukabakiza kuhama,
  Na sasa twende kufyonza, tamu iliyofichama
  Mimi nawe Naimani, ni kama wingu na mbingu!
  5.
  Mwaka ule si karibu, subira ndio mtaji,
  Tele hayo majaribu, yasiyopozwa na maji,
  Imara kama bawabu, makini kama hujaji,
  Mimi nawe Naimani, ni kama wingu na mbingu!
  6.
  Nyakati nayo majira, na zama zimetimia,
  Mapenzi haya imara, silaha kuu ya ndoa,
  hazijalishi ngawira, mapendo tumekamia,
  Mimi nawe Naimani, ni kama wingu na mbingu!
  7.
  mpira ulipoupiga, niliepa nisidake,
  kwa mengi ulinikoga, japo hunayo makeke,
  na sasa nimejibwaga, hirimu wangu nishike,
  Mimi nawe Naimani, ni kama wingu na mbingu!
  8.
  za mwizi hazikawii, zetu walizikamia,
  pamoja nayo bidii, ya maombi kuazimia,
  agizo sasa kutii, la ndoa na familia,
  Mimi nawe Naimani, ni kama wingu na mbingu!
  9.
  asante mpenzi wangu, kimasomaso menitoa,
  mapendo kama uchungu, kwa machozi nimeloa,
  lishike vizuri rungu, kwako nimeshajitoa,
  Mimi nawe Naimani, ni kama wingu na mbingu!
  10.
  tuijenge hiyo nyumba, yenye kujaa vicheko,
  watoto nao kuumba, mbinguni tupate heko,
  wala tusije kuyumba, kwani tunao upako,
  Mimi nawe Naimani, ni kama wingu na mbingu!
  11.
  udumu cha nyumba kichwa, mimi ni wako ubavu,
  bidii ipite mchwa, ushinde wote uchovu,
  nyuma tusije kuachwa, kwa Yesu uko wokovu
  Mimi nawe Naimani, ni kama wingu na mbingu!
  12.
  Asante wote wapendwa, kwa maombi nazo dua,
  Ni kweli hamkushindwa, shetani kumkemea,
  Upendo uliopandwa, hitaji kuu la ndoa,
  Mimi nawe Naimani, ni kama wingu na mbingu!

  wapendwa,

  pamoja na kuzidiwa na majukumu mengi kikazi, Mungu aliyajibu maombi tena vizuri sana. mchumba wangu anaitwa Naiman na ni mzaliwa wa Iringa. kama mjuanvyo masuala haya yana logistics nyingi na hivyo kukamilisha yote yaliyo ya muhimu inahitaji muda. hadi sasa mengine hayajakamilika. hapo katikati nilibahatika kupata scholarship ya kuripoti chuoni september mwaka huu na hivyo mtaona kuna kibarua cha kupangilia mambo hapo, kupata ruhusa na likizo ya masomo kazini na kuandaa harusi na wakati huohuo kutakiwa kuwa chuoni. so baada ya panga pangua, natarajia kwenda chuoni kwanza na kisha kurudi nyumbani november kwa ajili ya kufunga ndoa.

  Mungu awabariki sana,

  Glory to God!
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Jun 23, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  At least we can breath now!
   
 3. Romance

  Romance JF-Expert Member

  #3
  Jun 23, 2011
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 587
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  teh teh teh tih tih tih tah tah tah.... Khaaaaaaa!!!
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Jun 23, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Thread yangu imefanya kazi...Sometimes kukumbushana si mbaya!
  Hongera MJ, JAPO SIJAMALIZA KUSOMA unachomaanisha!
   
 5. Chauro

  Chauro JF-Expert Member

  #5
  Jun 23, 2011
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 2,969
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Ha haaaaaa kajibu mapigo PJ wapi weye?
   
 6. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #6
  Jun 23, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Santaaa Miss Judith :))
   
 7. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #7
  Jun 23, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180


  Umeanza tena!
  Una maana yeye kukuoa ni faida kwako tu na si kwa solidarity yenu!
  Acha ubinafsi wewe..ongelea mambo ya wawili, si kusema umetolewa kimasomaso peke yako!
   
 8. charger

  charger JF-Expert Member

  #8
  Jun 23, 2011
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 2,324
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Mh umekosa vifaa tu
   
 9. Romance

  Romance JF-Expert Member

  #9
  Jun 23, 2011
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 587
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  aaaaaaiiiiiiiiiiiiiii kwanini msikubali mlisemezana.... mmmmmh!!! mda mfupi aaandikee manenoo yooote hayaaa???? Khaaa!!! mnatupigaa changaa la ubongooo... Khaaaa!!
   
 10. kifrogi

  kifrogi Member

  #10
  Jun 23, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 42
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mashairi yanasema, mengi yanatuambia,
  Kwa watu wenye hekima, kauli huzizingatia,
  Na palipo waadhama, waidha huzingatia,
  Mashairi yanasema, asosikia kiziwi!

  Msigeuze mapenzi,yakawa ni mkurumbasi,
  Isirafu damisi,kwa shehe na makasisi,
  Mjukuu Ibilisi, kisirani na nuksi,
  Mapenzi kama hadithi, huishia muflisi

  Hili lataka kiasi, hakika si wasiwasi,
  Isirafu si nemsi, muulize Abunuwasi,
  Na vitabu kadurusi, uone yake nakisi,
  Mapenzi kama hadithi, huishia muflisi

  Mapenzi kitu halisi, hakichanganywi najisi,
  Haumo kwenye kamusi,uchafu na makamasi,
  Vinginevyo uyabisi,na kikali kiharusi,
  Mapenzi kama hadithi, huishia muflisi.
   
 11. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #11
  Jun 23, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Kifrogi nimependa ushauri nasaha kwa mtarajiwa wetu.
   
 12. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #12
  Jun 23, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,966
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Miss Judith malenga mzuri wewe eeh,shemeji atafaidi ghani zako.
   
 13. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #13
  Jun 23, 2011
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  "Mashangazi" Msisahau kuweka kitambaaa Cheupe...!!
   
 14. kifrogi

  kifrogi Member

  #14
  Jun 23, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 42
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Shukran mkuu
   
 15. nnunu

  nnunu JF-Expert Member

  #15
  Jun 23, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 656
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Hongera sana miss judithi kwa kufanikisha kila ulilolipanga.
   
 16. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #16
  Jun 23, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Miss Judith

  Kwenye uhusiano wenu nani ni wingu nani ni mbingu?
   
 17. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #17
  Jun 23, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,459
  Likes Received: 3,711
  Trophy Points: 280
  Miss wewe
   
 18. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #18
  Jun 23, 2011
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mwalimu naomba tofauti ya hayo maneno mawili
   
 19. kifrogi

  kifrogi Member

  #19
  Jun 23, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 42
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kabla ya harusi huwauliza bibi na bwana harusi
  Ikiwa wanajuana mashangazi watachinja mjusi
  Wageni watazugwa kwa mahanjumati na juisi
  Wallikwa tutafurahi huku tukigongeana gilasi
   
 20. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #20
  Jun 23, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,459
  Likes Received: 3,711
  Trophy Points: 280
  asante mpenzi wangu, kimasomaso menitoa,
  mapendo kama uchungu, kwa machozi nimeloa,
  lishike vizuri rungu, kwako nimeshajitoa,
  Mimi nawe Naimani, ni kama wingu na mbingu!

  Mie nimeona hapo kwenye blue............ nitakutafuta unifundishe mashairi.............. hongera MJ
   
Loading...