mbongombishi
JF-Expert Member
- Sep 23, 2014
- 588
- 291
Hivi hii mikutano ya CCM wahudhuriaji wake ni wanachama wa CCM pekee kila mahali?Mbona kila mkutano asilimia 85 ya wahudhuriaji wanakuwa wamevaa njano na kijani tu? Ukiaangalia mikutano ya kampeni ya vyama vingine,huwezi kuta jambo hili. Hii maana yake ni nini? Je,wanaohudhuria mikutano ya CCM wote ni wanachama wao?Kama ni hivyo,ina maana wanachama wa vyama vingine na wasio na vyama CCM haina haja nao au wao ndio hawana haja ya kwenda kuwasikiliza CCM?Je, huyo mgombea uraisi wa CCM ikitokea bahati mbaya kwa Watanzania kuwa amekuwa raisi wa Tanzania,atakuwa ni raisi wa wanachama na wapenzi wa CCM pekee?