Windows xp kwa lugha ya kiswahili..!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Windows xp kwa lugha ya kiswahili..!!

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by sijui nini, Dec 7, 2011.

 1. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #1
  Dec 7, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Haya tena wadau, kwa wale ambao bado hawajabahatika kupata Kiolesura Fungasha Kiswahili cha Windows® XP (language pack) leo nakileta mbele yenu..(kwa watakaopenda) ..Kiolesura Fungasha Kiswahili cha Windows® XP hiki kinabadilisha lugha ya komputa yako (achana na faili za program ulizoingiza/install mwenyewe) yenyewe inabadilisha lugha ya sistimu yako tu (windows). Kumbuka hii ni tofauti na njia ile inayotumika na wengi ya ku rename sehemu mbalimbali za koputa yako...hii ni sawa na wale wanaotumia komputa zao kwa lugha zingine kama kijerumani, ki arabu na nyinginezo..angalia mfano wa picha (screenshot) nilizochukua baada ya kubadili lugha kwenye pc yangu):

  swahili2.jpg swahili.jpg swahili1.jpg
  ili kupata Kiolesura hiki gonga hapa : Lugha gongana

  (wakati wa kudabiri /install utahitajika uwe na cd ya windows XP maana ili ubadili lugha ni lazima sistimu ichukua baadhi ya mafaili ya windows xp kutoka kwenye cd)
  endapo utahitaji kubadili lugha tena kurudi kingereza unafuata utaratibu wa kawaida tu wa kubadili lugha kupitia panel dhibiti(control panel).

  kwa maelezo zaidi : Maelezo ya upakuaji: Kiolesura Fungasha Kiswahili
   

  Attached Files:

 2. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #2
  Dec 7, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  nina simu ina menyu ya kiswahili lugha yake ni ngumu mno.sasa ya pc si ndio nitadelete mafile kabisa?
   
 3. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #3
  Dec 7, 2011
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Rununu hiyo uliinunua wapi?
  Hii Xp ya Kiswahili itaifaa sana ngamizi yangu
   
 4. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #4
  Dec 7, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  ni kweli kuna simu (hasa hivi vi nokia tochi flani hivi) vina lugha ya kiswahili...ila iko poa tu..kwenye ngamizi (pc) sasa ndo mapaka raha..utadeleteje..kwani kiswahili hujui..!??
   
 5. IrDA

  IrDA JF-Expert Member

  #5
  Dec 7, 2011
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 638
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 60
  kiswahili kinachotumika hapo ni kigumu sana,si kile cha kawaida kilichozoeleka....viu kama sanikisha,ngamizi,kichupio na maneno mengne mengi ya aina hii ni misamiati mipya kwa wengi wetu.....hivyo kutumia language pack hii kwaweza kumfanya mtu afanye mabadiliko mabaya kwenye kompyuta yake.....bora ingetengenezwa language ya kiswanglish
   
 6. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #6
  Dec 7, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,015
  Likes Received: 743
  Trophy Points: 280
  Hii lugha yetu ya Tanganyika katika TEKNOHAMA inakuwa ngumu.
   
 7. Donnie Charlie

  Donnie Charlie JF-Expert Member

  #7
  Dec 7, 2011
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 6,581
  Likes Received: 848
  Trophy Points: 280
  :poa, Vipi kwa window 7?
   
 8. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #8
  Dec 7, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  unajua kuna watu hawajua hata kingereza cha kuombea maji lakni wanaijua computer kila kona.. Kuna mtoto mmoja yuko darasa la 2 ila mpe computer! Mazoea nayo yanachangia..
   
 9. mtanganyika tz

  mtanganyika tz Member

  #9
  Dec 8, 2011
  Joined: Dec 3, 2011
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huyo dogo atakuwa ni jini! hakuna miujiza ya nmna hiyo! unataka kuniambia anaweza na kuburn DVD? haaaaaaaaaaa1 patachimbika aiseeeeeeeeeeee!
   
 10. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #10
  Dec 8, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  hi mimi nilishawahi kuiweka miaka 4 iliyopita kwenye PC. desktop yangu Marafiki zangu wakalalamika niondoe kabisa nikaiondowa walikuwa wanasema lugha yetu ya kiswahili kwa

  kutumia Ngamizi (Computer) ni ngumu huwezi kuielewa kabisa ipo mpaka Microsoft Office ya kiswahili hii Hapa Kipeto cha Kiolesura cha Kiswahili cha Office 2003 Maelezo ya upakuaji: Kipeto cha Kiolesura cha Kiswahili cha Office 2003
   
 11. Thinker96

  Thinker96 JF-Expert Member

  #11
  Dec 10, 2011
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 294
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  kweli nimeipenda lakini lugha yangu huwa mara nying inaishia airport...jitahidi uelewe
   
 12. sijui nini

  sijui nini JF-Expert Member

  #12
  Dec 10, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 2,382
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  this is serious man..ni mtoto wa shem wangu..anasoma la pili (next year la tatu)..actually shem an desktop na laptop home so dogo amekuwa akicheza nazo tangu akiwa mdogo kabisa bt kadri anavyokuwa ndo anazidi kuijua, mara nyingi shem huwa anampa vi kazi vidogovidogo vya ku type na dogo anawasha mwenyewe laptop, anatype ingawa ni kwa kudonoa(nakiri kuwa hajui mambo ya formatting hii anafanya marekebisho shem mwenyewe) na kusave akimaliza, anajua kufungua picha, muziki au kutizama CD/DVD zake za watoto kwa kutumia pc..hapo bado mambo ya games humtoi..so kwa level yake (ambayo hata hiko kingereza bado hakijui kivile ) lakini kuifaham pc hivyo ni nadra sana kwa wasiojua kabisa kingereza..na si kweli kuwa kila anaefahamu kuburn DVD basi ndo anaijui computer vizuri mkuu..
   
Loading...