Windows phone zimeendelea kufa kifo cha mende mbele ya Android na iPhone

thesym

JF-Expert Member
Aug 15, 2012
3,791
4,679
Kwa mujibu wa takwimu kutoka shirika la kitafiti la marekani ya maswala ya TEHAMA Gartner zinaonyesha simu za windows zimeshuka kwenye soko na kufikia 0.4% mwaka huu kutoka 3.3% mwaka 2013 na kuthibitisha rasmi windows phone ni simu zilizofeli na kushindwa kuteka soko mbele ya Android na iPhone.

Hivyo kama wewe ni developer ama mfanya biashara haina haja ya kupoteza muda wa kushughulika na simu zinazotumia OS ya windows.

Gartner Says Chinese Smartphone Vendors Were Only Vendors in the Global Top Five to Increase Sales in the Third Quarter of 2016

Gartner Says Smartphone Sales Grew 46.5 Percent in Second Quarter of 2013 and Exceeded Feature Phone Sales for First Time
 
mkuu focus ya nadella haipo tena kwenye windows phone ila hazitakufa na wala developer wanatakiwa wasiache kutengeneza. microsoft hajatoa simu mpya muda mrefu hivyo usitegeme kuwe na marketshare wakati hakuna simu ya kuuza

sasa hivi app zinazokuwa developed ni UWP yaani universal windows program, app hizi hurun kwenye simu, tablets, computer, xbox, hololens, surface hub etc,

future ya windows phone ni surface phone kama unafatilia utajua kuwa siku si nyingi microsoft na qualcomm wamezindua windows ya arm, windows hii itarun kwenye processor za simu na itarun app hadi za x86 kama photoshop kupitia emulator maalumu.

unaweza ukaangalia hii video kujua zaidi

Hizo apps mkuu zitafanya pia na kwa simu za window z zamani
 
WP walikosea pale walipofanya app development kuwa Rocket Science!
 
ukitumia xamarin si unadevelop kote kote? pia kuna project islandwood ambayo ina convert app za ios kuwa universal windows app na ipo project centennial ambayo inaconvert app za win32 (x86) kuwa za UWP

mfano wa app zilizokuwa za ios na wakaziport ni candycrush saga, pia kuna uwezekano app mpya za facebook, instagram na messenger ni project islandwood ndio imetumika.

kwenye centennial kuna app kama kodi na photoshop lightroom wameziconvert na sasa ni UWP kama una laptop ya win 10 unaweza kutest kodi ukaona.

pia kuna windows app studio ambayo huniwezesha mtu kama mimi ambae sio developer kutengeneza simple application ndani ya masaa tu bila kuandika hata mstari mmoja wa code na kui publish store
 
Windows phone ni smooth sana kwenye matumizi ila kitu ambacho sikipendi kwenye hii OS ni UI yake tu sijui ni kwa nini
 
mkuu focus ya nadella haipo tena kwenye windows phone ila hazitakufa na wala developer wanatakiwa wasiache kutengeneza. microsoft hajatoa simu mpya muda mrefu hivyo usitegeme kuwe na marketshare wakati hakuna simu ya kuuza

sasa hivi app zinazokuwa developed ni UWP yaani universal windows program, app hizi hurun kwenye simu, tablets, computer, xbox, hololens, surface hub etc,

future ya windows phone ni surface phone kama unafatilia utajua kuwa siku si nyingi microsoft na qualcomm wamezindua windows ya arm, windows hii itarun kwenye processor za simu na itarun app hadi za x86 kama photoshop kupitia emulator maalumu.

unaweza ukaangalia hii video kujua zaidi

Kushindwa kutoa simu muda mrefu si ni ishara ya kushindwa, biashara ingekuwa nzuri sidhani kama wangekaa muda wasizarishe bidhaa mpya!!
 
Hapana! Haimaanishi kwamba Microsoft wameshindwa, ukiangalia kwa ukaribu hivi karibuni Satya Nadela na wenzie wamejikita sana kwenye utafiti na uendelezaji(R&D) na siyo kukurupuka na kutoa simu mpya zisizo na chochote kipya. Wakati huohuo Microsoft inafanya kazi kwa ukaribu na watengenezaji wengine kama HP (HP Elite WP) kujaribu kufunga gap lilokuwepo kwa upande wa performance na matumizi kati ya desktop/laptop na smartphones ndiyo maana unaona kwa sasa unaweza ku-dock simu ya Windows kwenye monitor na ukafanya kazi zako za PC kama kawaida.
Wengi hawaielewi Microsoft kwa sasa, focus kubwa kwa Microsoft kwa sasa ni innovation na siyo imitation angalia bidhaa zao mpya kama Surface Studio kwa ajili ya creative professionals, angalia Microsoft SurfaceBook, bila kusahau Holo Lens concept zote hizi zimekuja kuleta tofauti kwenye computing industry na kuonyesha njia kwa watengenezaji wengine.
Hivyo basi kwa wale fans wa mobile computing mwaka 2016 umebadilisha mengi sana na mwaka 2017 utakua zaidi na kama alivyosema CHIEF MKWAWA Surface phone inakuja, na haitakua ya kawaida, inakuja kuleta tofauti na mwelekeo mpya kwa Windows OS.
 
Kushindwa kutoa simu muda mrefu si ni ishara ya kushindwa, biashara ingekuwa nzuri sidhani kama wangekaa muda wasizarishe bidhaa mpya!!
mkuu Mars Rover amejibu vizuri hapo juu, kifupi microsoft wamebadilisha CEO, huyu mpya hajaafiki ununuzi wa Nokia na windows phone hivyo focus yake ipo kwengine. hata ukiangalia wenyewe ndani wahusika wa windows phone kina Joe belfiore (mkuu wa windows phone) alipewa likizo ya mwaka mmoja toka 2015
Joe Belfiore is taking a year off from Microsoft
na aliporudi akapewa kazi nyengine kabisa
Joe Belfiore Returns To Microsoft, Will Drive Windows 10 Consumer Shell Initiatives - Thurrott.com
hivyo kifupi ni kama haiexist windows phone departmet, wataalamu wengi Nokia imewarudisha sasa hivi wapo HMD wanajiandaa kutoa simu za android na department ya feature phone pia microsoft wameiuza.

future ya windows phone sasa hivi ipo chini ya Panos Panay na surface team yake, huyu jamaa kwa miaka kama mitano iliopita amefanya mambo makubwa sana microsoft na wengi siku hizi wanamuita kama mrithi wa Steve Job. yeye ndio yupo nyuma ya bidhaa kama surface studio,surface hub, surface book na surface tablets, kukamilisha hio list inabidi kuwe na surface phone, na hapo ndio unaona future ya windows ya simu ilipo. ukichanganya na ile video ya juu windows ikifanya kazi kwenye arm soc inamaana surface phone itarun x86 program.

hivyo imagine unamiliki kifaa kimoja tu, ukichomeka kwenye monitor kinakuwa desktop, unachomeka kwenye tv kinakuwa gaming console au unaeka kodi tv yako inakuwa smart, kifaa hicho hicho ni simu, kinaweza kuwa server, unachomeka pad kinakuwa handheld gaming etc mimi naona hii ni kete yao ya mwisho microsoft, na toka zamani nimeandika sana humu nasubiria simu ya namna hii,
 
Mkuu wewe upo vizuri katika windows
Kwenye izi ishu za Surface hub, book, tablet zinakuwa na ukubwa wa inches ngapi?
Tatizo la izi Surfaces ni ukubwa bila kutembea na mabegi inakuwa ngumu
 
ukubwa tofauti tofauti mkuu kuanzia inch 10 mpaka 28
-surface studio ndio kubwa kabisa inch 28 ni desktop ya mezani
surface-studio-hands-on-13-720x720.png

-surface book inafuatia kwa ukubwa ina inch 13.5 hii ni laptop ndogo inayoweza kugeuka kuwa tablet ukichomoa keyboard
Surface_Book_MosaicPanelFeatures_side2-V3.jpg

-surface pro 3 na 4 hizi ni tablets zina inch 12 na zina option ya cover la kutype kama laptop
en-INTL-L-Surface-Pro4-SU3-00001-RM1-mnco.jpg

-surface za kawaida ambazo sio pro zina inch 10 hizi ndio ndogo zaidi
SurfacePro3Primary_Print-w640_thumb.jpg
 
Mkwawa Nina swali je kwa Simu Kama 950 na 950xl je kutakua na namna ya kuzifanya( update) kwenda surface au kufanya kua na uwezo sawa na hizo surface phone
 
hawajatoa taarifa yoyote mkuu kama zitakubali ama zitakataa, tusubiri event yao ya kuzindua surface pro 5 pengine watatangaza
 
Anha ni lini hasa Mkuu na pia nokia6 ni high end product au ? Bongo hasa lini? Dual?
nokia 6 sio highend ni low to mid range, pengine mwezi wa 5 itatoka na ina dual sim sema ni hybrid either unaeka memory card au unaeka line,

na surface pro 5 siku yoyote itatoka mkuu hakuna tarehe,
 
Kip bora niende Nokia 6 au ni weit surface surface pro5 itaweza cost bei gani ? Wanaposema kava ya Nokia 6 ni metallic sijui Nini? Wanamaamisha kava ngumu Kama za iPhone au
 
Back
Top Bottom