nataka ninunue Nokia X5, naomba sifa yake tafadhali,naipenda.
mkuu tuanze na browser
watu wengi wanashangaza sana wanataka na wp nayo iwe na firefox, dolphin, chrome. vya nini? kwenye pc unavyo na simu ya android unavyo huku pia unataka sidhani kama ni jambo la busara. wp ina browser zake unique mkuu tena nzuri tu ntakutajia chache hapa
1.surfcube 3d browser
hii ni browser yenye ladha ya 3d wanatumia engine ya ie kama sjakosea lakini ina muonekano mzuri ambao hauchoshi kutumia
![]()
2. nokia express browser
huyu anatumika kama operamini ina uwezo wa kucompress data hadi asilimia 90. ni nzuri kibongo bongo kupunguza matumizi ya bundle.
![]()
3. ucbrowser
wote tunaijua wote tunaipenda uwezo wake wa kudownload na kusuport resume tunautambua so still mkuu unasema hakuna alternative za browser?
hizi ni browser chache ninazokumbuka.
kuclose app kwenye multitask window
mkuu natumia android ila nikidownload hata nikiclose app kwenye multitasking window inadownload (ilitakiwa ikill process? ndo ulivomaanisha?) na hata wp uache apps 10,000 haiafect maana haina true multitasking mkuu
system wide file manager(na sio file manager)
even android haina system wide file manager mkuu hadi leo miaka 6 sasa, zile file manager ni oems kama samsung, huawei, htc wanaeka wenyewe so ni just matter of time kabla ya oem wa wp hawajaeka zao. wp8 ndo kwanza ina miezi 6.
kuhusu file manager wp inayo thats why unaplay miziki native, video unaangalia picha.
tofauti ya file manager na system wide file manager ni kuwa file manager inaonesha format zinazosuport kwenye simu tu wakati system wide inaonesha mafile ya pc, mac na chochote unachoeka.
then wp ina mass storage incase unahitaji ku uncompress file unaplug kwenye pc tu.
-local search sjaelewa hebu nielezee zaidi
-can u tell me kitu gani kipo google search kwenye bing hamna (toa sababu ya mazoea)
kuhusu unified notification centre inaweza kuwa muhimu kwa wengine na kwa wengine isiwe muhimu maana nature ya wp ina home screen yenye tiles na people hub. mfano ikiblink notification ya people hub basi ujue kuna notification ya social it may be facebook, twitter, email nk unaclick unaiona
its hard mkuu ukitaka hizi os mbili ziwe sawa tumia device zake ndo utazielewa
oh! my God, kwahiyo inabidi niwe na kitochi kwa ajili hiyo tu...
Android mpango mzima window phone no nzuri lakini huwezi kufurahia kama android
mkuu kwanini usikamate hicho kitu kwenye avatar yako!!
Ni kawaida sasa hivi kwenye redio kusikia matangazo ya lumia, samsung galaxies zinazidi kushika kasi, techno wanakomba soko la Tanzania na huawei nyingi za tigo zinazidi kusambaa. yote haya yanaweza kukuchanganya na kufanya usifanye uamuzi sahihi wakati wa kuchagua simu. hebu tuangalie windows phone ni nini na android ni nini na baadae utajua ufanyeje kuchagua simu sahihi.
Windows phone 8
Hii ni operating system iliyotengenezwa na microsoft inatumika kwenye simu za nokia, htc, samsung na huawei mpaka sasa. imekuja kumreplace windows phone 7 ambayo haikupokelewa vizuri na wateja. tofauti na android windows phone inatumia tiles badala ya icon design yake hii imeipa umaarufu sana.
![]()
Android
Hii ni operating system iliyotengenezwa na google na inatumika na watengeneza simu zaidi ya 80 wachache wao ni samsung, htc, huawei, tecno, sony, lg na asus. Hii inatumia icon tofauti na windows phone. pia ina homescreen ambayo unaweza kueka app zako unazozipenda.
![]()
Je ukitaka kununua simu ya windows phone uangalie nini?
Its about people vs apps
Kitu kimoja kizuri kuhusu windows phone ni uwezo wake wa kukusanya watu wote unaowajua na kuwaweka pamoja na kukupa habari zao zote. kuna peoples hub ambayo inakua na list ya marafiki zako na kama wana acount za facebook, twitter, unaona habari zote kwenye contact bila hata kufungua app ya twitter au facebook.
![]()
![]()
Ukitoa peoples hub kuna feature kama kids corner ambayo ni simu ya mtoto ndani ya simu yako, hapa unachagua application, video, miziki ambayo unataka mtoto wako aone akishika simu ili kumzua asifanye vitu vibaya. pia kuna rooms ambayo inakua ni private area kati yako na watu unaowapenda kama mke wako na wakwe zako eneo ambalo mtashare location na kila kitu. haya na mambo mengi yanaifanya windows phone kua very strong kwenye upande wa watu.
One thing cool about android ni ina application nyingi sana. so far kuna application zaidi ya 700,000 wakati windows phone ina application 150,000 tu. hili linafanya vichwa vikubwa kama instagram kupatikana android na kukosekana kwenye windows phone.
![]()
So wakati unachagua simu uangalie mahitaji yako kati ya hivyo vitu viwili hapo juu.
Its about microsoft vs google
Kuna msemo siku hizi kuwa hununui simu bali unanunua ecosystem. huu msemo ni sahihi kabisa kwani kila platform siku hizi ina apps zake ambazo ni exclusive kwao tu, hapa nitaelezea ecosystem inayopatikana kwenye android na windows phone. kupunguza ukubwa wa thread nitazimention tu kama utataka maelezo zaidi utacoment
Hizi ni chache za muhimu so utaangalia ecosystem ipi unaipenda hapa nimeexclude apps za nokia maana ni special case.
- microsoft office(wp) vs quickoffice(android)
- search (bing search) vs search (google search)
- map (nokia,bing map) vs map (google map)
- video (hakuna) vs video (youtube)
- mail (outlook,hotmail) vs mail(gmail)
- cloud(skydrive) vs cloud (google drive)
- video chat(skype) vs video chat (hangout)
- gaming (xbox) vs gaming (hakuna)
Its about design vs customization
Kama nilivoelezea hapo juu windows phone imekuja na design mpya kabisa ya tiles ambazo ni live zinakupa information papo kwa hapo hizi tiles huwezi kuzichange na kuweka customization kama android lakini unaweza eka design unayotaka. unaweza resize tiles zikawa kubwa, za kati au ndogo na pia unaweza ukachange skin.
![]()
![]()
![]()
Andoid yenyewe ipo vizuri kwenye customization kuliko windows phone unaweza ukaieka home screen yako the way unavyopenda wewe. zipo launcher mbali mbali zenye themes tofauti tofauti kwa kazi hii. kwenye android pia kuna launcher ambazo zinakuwezesha kuweka themes za 3d ili kuwezesha wewe kufeel tofauti ukitumia simu
![]()
Its about security vs freedom
Kwenye windows phone mpaka sasa huwezi kuroot simu wala kufanya hacking ya aina yoyote simu imefungwa kila kona hili linaongeza ulinzi kwenye simu yako hutaathiriwa na virusi wala malware wa aina yoyote device itakua salama lakini tatizo linakuja unakosa uhuru hutaweza kufanya vitu unavyotaka wewe.
Kwenye android unakua huru unaroot simu unaeka custom firmware unafanya vitu unavyotaka wewe lakini tatizo linakuja kwenye security android kuna malwares wengi wanaweza wasiwe virusi lakini vitu kama spyware na adware ni vigumu kuviepuka kwenye android.
its about productivity vs playing
nafkiri hapa ndo pa muhimu zaidi panapozitenganisha hizi simu. kuwepo kwa microsoft office, skydrive, photobeamer, security kubwa, offline navigation na simu kuwa fasta kunaifanya windows phone kuwa nzuri kwa wafanya biashara kuliko android.
kuwepo kwa HD games, na application mbali mbali kunaifanya android iwe simu nzuri ya kuchezea so hapa unatakiwa uangalie unahitaji nini je wewe unapenda kuchezea simu au unataka simu yako iwe productive? maana unaweza ukaenda windows phone then ukakuta games chache ukaanza kulalamika. na unaweza kuwa mfanya biashara ukaenda android ukaanza kulalamika betry na simu kuwa slow.
Hayo ndio mawazo yangu kuhusu windows phone na android nikiwa kama mtumiaji ambaye nishatumia platform zote. pia kuhusu windows phone nimeongelea windows phone 8 na sio 7 better unaponunua simu ya windows phone ununue 8, kama huna uhakika ni vizuri uulize.
nimeona Lumia 950 iko pouwa kweli hasa in terms of OS (windowas 10) pretty amazing. Camera yenye triple flash ya 20 MP nyuma kwa 5mp mbele. yaaani kiujumla imekaa vizuri sana. CHIEF MKWAWA waonaje ujio huu wa Microsoft na hii Lumia 950? karibuni tuendelee na mjadala wa hii simu na OS yake ya Windows 10
Daa nimeipenda kaka... 32 internal memory... 5.2 inches... Li-Ion 3000 mAh battery.. Ni ujio mzuri sana.. Sijui kwenye bei kutakuaje...
nimeona Lumia 950 iko pouwa kweli hasa in terms of OS (windowas 10) pretty amazing. Camera yenye triple flash ya 20 MP nyuma kwa 5mp mbele. yaaani kiujumla imekaa vizuri sana. CHIEF MKWAWA waonaje ujio huu wa Microsoft na hii Lumia 950? karibuni tuendelee na mjadala wa hii simu na OS yake ya Windows 10
hii thread ni nzuri, wakuu kati ya samsung mega na htc lates ipi mnanishauri kununua maana zote nazipenda na nimekosa choice na s6 edge ina kipi exceptional kisichopo kwenye s4 na s5