Windows phone vs android niende wapi?

Windows phone vs android niende wapi?

nadhan Hata Kwenye I Devices Pia Hakuna Hyo System Wide
bb hazina, iphone hazina, android haina (os) ila unapata third party

nimetafuta sana playstore file manager zenyewe zina limitation sio kwamba ni nzuri kama za symbian au windows explorer kwenye pc.

1. ukicopy kitu ukapaste hapo hapo ukifanya activity nyengine kinapotea kwenye clipboard
2. havionyeshi system files (kama symbian)
3.haimanage vitu unavyoconect na usb (kama symbian)
 
chief asante sana hakika nimepata shule tosha. ila kwa nini wasikupe Nokia E.A marketing manager?
 
Wakuu mm nipo zaidi kwenye upande wa Android coz hii os kwanza ni opensource hii inamaanisha kwamba mtu yeyote mwenye uwezo anaweza kuicustomize iweze kuingia kwenye handset yake kama unavyoinstall window latest version kwenye komputer yako!!!!its totally possible!!!mm binafsi ninatumia the latest android version ambayo nimeidownload na kuiinstall kwenye simu yangu ingawa kampuni ya simu yangu walishaacha kusupport latest android releases kwenye hii model ya simu yangu....Ukija kwa window phone utagundua kwamba Hiz window os sio opensource na imefungwa na hawa jamaa wa microsoft kwa hiyo wewe kama una nokia flani ina window phone 8 then huko mbele ikatoka window phone 9 for example na nokia wasitoe upgrade release ya window phone 9 kwa handset yako then solution ni kununua phone mpya yenye window phone 9 ile uweze kupata features za hiyo os mpya!!!Tofauti na android kuna custom os nyingi out there unaweza ukainstall kwenye handset or tablet yako!!!! pia bila kusahau ubuntu wanatoa os ambazo zinaweza kuingia kwenye android tablets na simu ambayo unaweza ukaiinstall desktop apps kwenye handset yako!!!! soma hapa Ubuntu on tablets | Ubuntu!!!! Mtazamo wangu......🙂
 
mkuu open os ina faida na hasara zake. mfano makampuni mengi kazini hawatumii open os sababu code za open os zipo wazi mtu yoyote anaweza akaona unachofanya.

wp8 so far haijawa hacked ni safe kwa wafanyabiashara ila ile wp7 washaihack kule xda vitu kama file manager, custom rom vipo.

hata hii wp8 watu wakihack utaweza kufanya hayo mambo ya kueka rom wp8 ina miez sita tu wakati android ni mwaka wa 6 huu.

kuhusu simu kurun desktop app nahitaji convicing power kubwa sana kuchange mind yangu sababu ni hii.

-desktop app zimekua programed kurun katika special processor (za intel na amd)

-even arm pc hazirun desktop app mfano windows rt based tablets

-even inttel atom haiwezi kuhandle power ya desktop app

je simu zitaweza? na hivi vi qualcom na mediatek?

unaweza pata ui ya desktop ila power ya apps kama photoshop sidhani kama itakubali kwenye simu
 
chief-mkwawa inaonekana kweli wewe umzoefu na hivi vijamaa! mimi nimenunua nokia lumia 610 huko sweden si kwa sababu maalum bali kuipenda tu, lakini nilipofika nayo tz ikawa inanisumbua haitaki mambo ya tigo pesa wala kabaang! yaani ukiweka codes tu *150*01# inakwambia session terminated, jee imewahi kuliona hili, jee tatizo katika simu au mtandao wenyewe, jee jambo hili linaweza kurekebishika na wali? kwa sasa nimeona shida hii tu kwa sababu mimi napiga simu na kutumia tigo/m-pesa etc sijawahi hata kupiga picha au kuweka mziki!!! naomba msaada wako, thanks!
 
chief-mkwawa inaonekana kweli wewe umzoefu na hivi vijamaa! mimi nimenunua nokia lumia 610 huko sweden si kwa sababu maalum bali kuipenda tu, lakini nilipofika nayo tz ikawa inanisumbua haitaki mambo ya tigo pesa wala kabaang! yaani ukiweka codes tu *150*01# inakwambia session terminated, jee imewahi kuliona hili, jee tatizo katika simu au mtandao wenyewe, jee jambo hili linaweza kurekebishika na wali? kwa sasa nimeona shida hii tu kwa sababu mimi napiga simu na kutumia tigo/m-pesa etc sijawahi hata kupiga picha au kuweka mziki!!! naomba msaada wako, thanks!

mkuu hizo ussd hazikubali hio simu.
 
mm naomba msaada wa kuinstal apps na haya mambo ya android or window cna uelewa nayo sana. simu yangu ni iphone 4s. MSAADA TAFADHALI
 
mm naomba msaada wa kuinstal apps na haya mambo ya android or window cna uelewa nayo sana. simu yangu ni iphone 4s. MSAADA TAFADHALI
 
Msaada nili-root simu yangu inayotumia android,nikafuta Rom kwa bahati mbaya,nikiwasha simu inaishia logo ya Tecno tu,na inataka ku-update hyo Rom from Sd nifanyaje?
 
mkuu open os ina faida na hasara zake. mfano makampuni mengi kazini hawatumii open os sababu code za open os zipo wazi mtu yoyote anaweza akaona unachofanya.

wp8 so far haijawa hacked ni safe kwa wafanyabiashara ila ile wp7 washaihack kule xda vitu kama file manager, custom rom vipo.

hata hii wp8 watu wakihack utaweza kufanya hayo mambo ya kueka rom wp8 ina miez sita tu wakati android ni mwaka wa 6 huu.

kuhusu simu kurun desktop app nahitaji convicing power kubwa sana kuchange mind yangu sababu ni hii.

-desktop app zimekua programed kurun katika special processor (za intel na amd)

-even arm pc hazirun desktop app mfano windows rt based tablets

-even inttel atom haiwezi kuhandle power ya desktop app

je simu zitaweza? na hivi vi qualcom na mediatek?

unaweza pata ui ya desktop ila power ya apps kama photoshop sidhani kama itakusbali kwen
 
ni kawaida sasa hivi kwenye redio kusikia matangazo ya lumia, samsung galaxies zinazidi kushika kasi, techno wanakomba soko la tanzania na huawei nyingi za tigo zinazidi kusambaa. yote haya yanaweza kukuchanganya na kufanya usifanye uamuzi sahihi wakati wa kuchagua simu. hebu tuangalie windows phone ni nini na android ni nini na baadae utajua ufanyeje kuchagua simu sahihi.

windows phone 8
hii ni operating system iliyotengenezwa na microsoft inatumika kwenye simu za nokia, htc, samsung na huawei mpaka sasa. imekuja kumreplace windows phone 7 ambayo haikupokelewa vizuri na wateja. tofauti na android windows phone inatumia tiles badala ya icon design yake hii imeipa umaarufu sana.


android
hii ni operating system iliyotengenezwa na google na inatumika na watengeneza simu zaidi ya 80 wachache wao ni samsung, htc, huawei, tecno, sony, lg na asus. hii inatumia icon tofauti na windows phone. pia ina homescreen ambayo unaweza kueka app zako unazozipenda.

je ukitaka kununua simu ya windows phone uangalie nini?

its about people vs apps
kitu kimoja kizuri kuhusu windows phone ni uwezo wake wa kukusanya watu wote unaowajua na kuwaweka pamoja na kukupa habari zao zote. kuna peoples hub ambayo inakua na list ya marafiki zako na kama wana acount za facebook, twitter, unaona habari zote kwenye contact bila hata kufungua app ya twitter au facebook.

ukitoa peoples hub kuna feature kama kids corner ambayo ni simu ya mtoto ndani ya simu yako, hapa unachagua application, video, miziki ambayo unataka mtoto wako aone akishika simu ili kumzua asifanye vitu vibaya. pia kuna rooms ambayo inakua ni private area kati yako na watu unaowapenda kama mke wako na wakwe zako eneo ambalo mtashare location na kila kitu. haya na mambo mengi yanaifanya windows phone kua very strong kwenye upande wa watu.

one thing cool about android ni ina application nyingi sana. so far kuna application zaidi ya 700,000 wakati windows phone ina application 150,000 tu. hili linafanya vichwa vikubwa kama instagram kupatikana android na kukosekana kwenye windows phone.


so wakati unachagua simu uangalie mahitaji yako kati ya hivyo vitu viwili hapo juu.

its about microsoft vs google
kuna msemo siku hizi kuwa hununui simu bali unanunua ecosystem. huu msemo ni sahihi kabisa kwani kila platform siku hizi ina apps zake ambazo ni exclusive kwao tu, hapa nitaelezea ecosystem inayopatikana kwenye android na windows phone. kupunguza ukubwa wa thread nitazimention tu kama utataka maelezo zaidi utacoment

  • microsoft office(wp) vs quickoffice(android)
  • search (bing search) vs search (google search)
  • map (nokia,bing map) vs map (google map)
  • video (hakuna) vs video (youtube)
  • mail (outlook,hotmail) vs mail(gmail)
  • cloud(skydrive) vs cloud (google drive)
  • video chat(skype) vs video chat (hangout)
  • gaming (xbox) vs gaming (hakuna)
hizi ni chache za muhimu so utaangalia ecosystem ipi unaipenda hapa nimeexclude apps za nokia maana ni special case.

its about design vs customization
kama nilivoelezea hapo juu windows phone imekuja na design mpya kabisa ya tiles ambazo ni live zinakupa information papo kwa hapo hizi tiles huwezi kuzichange na kuweka customization kama android lakini unaweza eka design unayotaka. unaweza resize tiles zikawa kubwa, za kati au ndogo na pia unaweza ukachange skin.


andoid yenyewe ipo vizuri kwenye customization kuliko windows phone unaweza ukaieka home screen yako the way unavyopenda wewe. zipo launcher mbali mbali zenye themes tofauti tofauti kwa kazi hii. kwenye android pia kuna launcher ambazo zinakuwezesha kuweka themes za 3d ili kuwezesha wewe kufeel tofauti ukitumia simu


its about security vs freedom
kwenye windows phone mpaka sasa huwezi kuroot simu wala kufanya hacking ya aina yoyote simu imefungwa kila kona hili linaongeza ulinzi kwenye simu yako hutaathiriwa na virusi wala malware wa aina yoyote device itakua salama lakini tatizo linakuja unakosa uhuru hutaweza kufanya vitu unavyotaka wewe.
kwenye android unakua huru unaroot simu unaeka custom firmware unafanya vitu unavyotaka wewe lakini tatizo linakuja kwenye security android kuna malwares wengi wanaweza wasiwe virusi lakini vitu kama spyware na adware ni vigumu kuviepuka kwenye android.

its about productivity vs playing
nafkiri hapa ndo pa muhimu zaidi panapozitenganisha hizi simu. kuwepo kwa microsoft office, skydrive, photobeamer, security kubwa, offline navigation na simu kuwa fasta kunaifanya windows phone kuwa nzuri kwa wafanya biashara kuliko android.
kuwepo kwa HD games, na application mbali mbali kunaifanya android iwe simu nzuri ya kuchezea so hapa unatakiwa uangalie unahitaji nini je wewe unapenda kuchezea simu au unataka simu yako iwe productive? maana unaweza ukaenda windows phone then ukakuta games chache ukaanza kulalamika. na unaweza kuwa mfanya biashara ukaenda android ukaanza kulalamika betry na simu kuwa slow.

hayo ndio mawazo yangu kuhusu windows phone na android nikiwa kama mtumiaji ambaye nishatumia platform zote. pia kuhusu windows phone nimeongelea windows phone 8 na sio 7 better unaponunua simu ya windows phone ununue 8, kama huna uhakika ni vizuri uulize.
mkuu Nina haka ka htc 8x tiles Zimetawanyika tofauti na nilivonunua nimejaribu kutafuta option ya factory resseting ili kuirudisha nimeshindwa je nafanyaje kupanga zile tiles. Na je Ni kweli simu hii haina fm radio cz mi huwa napendelea kusikiliza radio kwenye simu
Asante!
 
mkuu Nina haka ka htc 8x tiles Zimetawanyika tofauti na nilivonunua nimejaribu kutafuta option ya factory resseting ili kuirudisha nimeshindwa je nafanyaje kupanga zile tiles. Na je Ni kweli simu hii haina fm radio cz mi huwa napendelea kusikiliza radio kwenye simu
Asante!

bonyeza tiles husika kwa mda mrefu mpaka utaona kwa pemben kumetokea kimshale kibonyeze hiko kimshale kubadilisha ukubwa wa tile kuwa ndogo saizi ya kati au kubwa. pia hapo hapo utaweza kumove kutoka eneo moja kwenda nyengine ili kuziba nafasi ambazo zipo wazi.

kuhusu suala la fm radio ni kwamba simu hizi za windows phone hazikuja na radio ila hardware zake zina radio hivyo zikawa zinahitaji tu application ili kuwepo hio radio.

manufacture wote ikiwemo htc wakatoa update (gdr 2) ili kuzipa simu zao uwezo wa kua na fm radio. kama simu yako haina fm radio ina maana huja update bado unatumia version ya zamani.

nenda setting then kacheki update, kisha update simu yako fm radio itakuja
 
Android mpango mzima window phone no nzuri lakini huwezi kufurahia kama android
 
Back
Top Bottom