Windows partitioning in Windows Vista | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Windows partitioning in Windows Vista

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Original Pastor, Nov 21, 2009.

 1. Original Pastor

  Original Pastor JF-Expert Member

  #1
  Nov 21, 2009
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 1,256
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Habari ya Kazi wadau wa JF

  Napenda kuchukua fruksa hii kiwapa pongezi wale wote waliofanikiwa kuchangia mada zangu za kuomba msaada na nimefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana hizi ni shukran zangu kwa woote na uongozi Adm ya JF. Leo nina ombi moja tu. Nataka kugawanya HDD yangu katika Laptop yangu LG HDD 110 Ram 1GB na ina Window Vista Home Basic pamoja na Office 2007 sasa nataka hii HDD niigawanye mafungu matatu moja niweke Drive C , Drive D na Drive E. Hii C nataka kuweka Program pekee, Hii D baadhi Document zangu muhimu, E nataka kuweka Document zote ambazo nazisave pamoja picha ,video n.k Naomba Msaada waheshimiwa wana JF wenzangu. Wik end Njema.
   
 2. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #2
  Nov 22, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,119
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Right click My Computer, changua Manage, chagua Disk Management, Right click Drive C: Chagua Shrink Volume, weka size unayotaka C iwe.

  Ukisha shrink utakuwa na unallocated space, right click hiyo unallocated space then select new volume, weka size unayotaka D iwe etc >>Finish. Itatengeneza drive D.

  Right click unalloccated space iliyobaki kisha rudia hatua kutengeneza drive E.
   
 3. Original Pastor

  Original Pastor JF-Expert Member

  #3
  Nov 22, 2009
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 1,256
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135

  OK mkuu sasa nimefanikiwa lakini mbona haitaki kugawa kwani inanipa Mb na mimi nataka hiyo HDD 110GB niigawe mara tatu 36.5GB kila moja sasa nitafanyaje kwani inanipa MB 220 tu sasa naomba maelekezo tena mkuu!!
   
 4. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #4
  Nov 22, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,119
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Kiasi gani kiko free kwenye Hard Drive yako? Itabidi uwe una 36.5 X 2 free kama unataka kuigawa hivo.

  Kama nafasi ipo na bado inakataa basi hard drive itakuwa iko fragmented Download Raxco Perfect Disk http://download.cnet.com/PerfectDisk/3000-2094_4-10349543.html?tag=mncol
  (30 days free)

  Kisha ukiirun chagua option ya "Consolidate Free Space" na tick Boot Time, kisha start defragmentation, inaweza ikachukau muda so ni bora kuiacha unapoenda kulala.
   
 5. Original Pastor

  Original Pastor JF-Expert Member

  #5
  Nov 23, 2009
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 1,256
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Unajua Mkuu HDD imebakiza 20.5 BG sasa wewe unasema 36.5 ninini? MB au GB. sasa naomba ushauri nimedawnload inakataa kwani natumia Vista Home Basic sasa nifanyeje mkuu usichoke
   
 6. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #6
  Nov 23, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,119
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Hauwezi ku shrink zaidi ya freespace kama unataka drive C iwe na 36.5GB itabidi usiwe na data zaidi ya hizo 36.5GB, actually chini zaidi maana kuna system files na vitu kama hivyo.

  Imekataa kivipi? Hiyo program inafanya kazi kwenye Vista.
   
 7. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #7
  Nov 23, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,367
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo tiba uliyompa asipopona kiboko!!ukweli hivyo ndivyo anavyotakiwa afanye!!
   
 8. Original Pastor

  Original Pastor JF-Expert Member

  #8
  Nov 23, 2009
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 1,256
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135

  Sawa Mkuu basi inawezekana ku copy data zote then niweze ku shrink? kama inawezekana niweke kwenye External Hard Drive data zote nibakishe Program tu kisha niweze ku shrink? Pia natumia Ant virus ya Kersperk labda ndo ina Block au maana ninayo hapa na net ipo faster nime i save katika desktop yangu nasikiliza ushauri wako mkuu sasa nifanyeje?
   
 9. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #9
  Nov 23, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,119
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Ya inawezekana, hamisha data zote unazoweza kwenye external. Ukiwa na free space nyingi utakuwa na chance kubwa zaidi ya mafanikio.

  Hiyo program (perfect Disk) inachofanya ni kupanga jinsi data zilivyorekodiwa kwenye HD, ili uweze kushrink inabidi free space iwe continuous, so hiyo "Consolidate free space" ndio itakachofanya.
   
Loading...