Win XP to Win 8 or Linux?! (ATM OS)

Win XP to Win 8 or Linux?! (ATM OS)

Rutayuga91

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2011
Posts
449
Reaction score
250
Hapo April microsoft waliacha kusupport windows XP! lakini 95% ya ATM duniani wanatumia Windows XP. Hali hii inaziacha ATM mashine nyingi duniani kwenye risk ya kudukuliwa (hacked) na wadukuaji/wadukuzi.

Kwa maana hiyo benki nyingi duniani zinapaswa kutenga fungu kwa ajili ya kuupgrade Operating System (OS) za ATM machine zao. Ila kwa kiasi fulani sio bank peke yao hata baadhi ya taasisi za serikali nyingi duniani bado wanatumia win XP, mfano Serikali ya china iligomea kununua Windows mpya na kung'ang'ania Win XP.

Hali hiyo sio kwa nchi hizo kubwa tu bali pia hata Tanazania inahusika katika balaa hili. Serikali na taasisi zake zote, mabenki kama CRDB, NMB na NBC wanapaswa kuwekeza kwenye kununua win7 au win 8, windows ambazo kwa sasa Microsoft wanazisupport, hivo kuonekana kama ni salama zaidi kuliko win xp.

Ikumbukwe kuwa kuna OS nyingi za bure ambazo ni secure kulliko hata windows kama Linux based OS mfano Linux mint, Ubuntu na Fendora ambazo pia zinapatikana bure tena mutumiaji ana uhuru wa kuedit OS namna yoyote anavyotaka. kwa kutumia OS hizi benki na serikali watakuwa na uhuru wa kutengeneza OS zao wakitumia Kernel za Linix.

Kwa upande wangu mimi naona huu ni wakati muafaka wa dunia kuwapa mgongo Microsoft na kugeukia Linux, jambo ambalo litasaidia taassisi nyingi duniani kusave pesa, muda na mawazo/stress za huyo Bro Gates.

Nawaachia wadau wa JF kuliangalia swala hilo! mwaonaje wadau ?!
 
Kwanza nikusahihishe tu gates sio mmiliki mkubwa wa msft miez kadhaa iliopita ameuza hisa nyingi sana.

kuhusu hao china nao wanafiki tu sababu toka mwanzo hawatumii hio xp bali wanatumia clone ya xp inaitwa red linux ambayo kila kitu ni kama xp.

kuhusu atm kuhamia linux kwangu ni 50 kwa 50 japo linux ni secure ila support za community zinaweza pia acha openings kwa watu wachache kuweza kunufaika

nafkiri muda umefika wa atm kuwa na os yao sasa. Msft hawez eka xp open source na google ndio choice ya mwisho, apple atawacharge sana itabidi wahamie huko huko linux ila inabidi waanze kutengeneza from scratch
 
Rutayuga91
chief-mkwawa

Mnaposema Linux ni secure nashindwa kuwaelewa !

Naombeni ufafanuzi kidogo !

kwenye Linux Based OS huwezi kuinstall program yoyote bila admn permission! hata baadhi ya program ikitaka kurun inahitaji permission mfano kwenye Ubuntu kuna comands kama Sudo ambazo unatakiwa kurun na keweza kuinstall program.
Linux based OS zina shell strong kuliko hata Windows.
Virus developers wamebase kwenye Windows kuliko hata Linux based OS hivo kufanya Windows kuwa dhaifu ukiilinganisha na Linux based OS.
 
Back
Top Bottom