Wimbo wa Kanumba: Alitabiri kifo chake?

Muce

Senior Member
Dec 19, 2011
116
14
Kuna wimbo aliuimba steve kabla hajatutoka ni zab. 121

 
Last edited by a moderator:
Nimeusikia ni kama wa dini vile,inaonyesha ni kama alijitabiria kifo chake kutokana na mistari ya wimbo huu.
 
Hiyo ni zaburi ya 121 ila ameongezea maneno kidogo, kiukweli unasikitisha sana. R.I.P KANUMBA
 
Dah hata mie nimeusikia huo wimbo,ni kweli kwa maneno aliyoyaongezea unaweza sema alijitabiria kifo chake..wimbo unateka sana hisia za mtu..kiufupi jamaa alikuwa jembe maeneo mengi hadi kwenye uimbaji.
 
maneno aliyo yaongeza,yamenigusa kwani ni kama aliona mauti
Maneno yanasema
Siku nikifa,watu watasema hakuna wa kuziba pengo langu
Hata wabaya wangu,watabeba jeneza langu
Watu watasema,ametutoka msanii tuliye mpenda.

Huwezi amini kama jamaa kweli aliimba haya maneno

RIP Ma Young Bro.
 
tujuzeni wengine hatujausikia,hyo zaburi 121 inazungumzia nini?


zaburi 121

" nitayainua macho yangu nitazame milima , msaada wangu utatoka wapi ?msaada wangu u katika bwana , aliyezifanya mbingu na nchi, asiuachu mguu wako usogezwe , asisinzie akulindaye; naam hata sinzia wala hata lala usingizi, yeye aliye mlinzi wa israel. Bwana ndiye mlinzi wako; bwana ni uvuli mkono wako wa kuume . Jua halitakupiga mchana , wala mwezi wakati wa usiku. Bwana atakulindana mabaya yote , atakulinda nafsi yako. Bwanaatakulinda utokapo na uingiapo, tangu sasa na hata milele.
 
Wimbo wake nimeurekodi na simu nitajitahidi niuweke
 
jaman wimbo wa kn umenigusa sana, naweza sema alijitabiria kifo ama nafsi yake ilimtuma pasipo kujua kujitabiria kifo. hasa pale aliimba "hata wanaonichukia watabeba jeneza langu" hakika alikuwa anaaga indirect... rip kn!
 
Kwa hiyo unamaanisha watu wasijaribu kuifundisha jamii?Alikuwa akimaanisha siku ya kifo atakaye mzika hamjui!
 
Hata asingeimba angekufa tu siku yake ikifika,hata remmy ongalla aliimba wimbo wa kifo zamani lkn kaja kufa 2010.
 
Wakuu nimetembelea blog ya wavuti nimeona script ambayo ameshawahi kuigiza marehemu kanumba kwenye igizo la baragumu, yule mtoto alieigiza nae ndiye LULU? kwani nimeona kama amefanana nae, kwa anaemjua vizuri tafadhari tuambie
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom