ni wimbo mzuri wenye mdundo mzuri na ujumbe unaotia. simanzi lakini uliokosa uhalisia na unaitwa ni wimbo wa dini lakini kimsingi asilimia tisini haujakaa kidini bali ni hadithi ya maisha
Tuangalie uhalisia unapokosekana
1.Baaada ya kupata masaibu ya mme wake anahangaika kutafuta msaada wa mawifi na rafiki wa mumewe lakini kila mtu anakuwa na udhuru, ina maana kati ya wote hakuna hata mmoja mwenye msaada?basi kama ni hivyo una matatizo wewe
2.Anajaribu bank lakini akounti zote anakuta zina shida hivyo hawezi kutoa pesa ,,,katika dunia hii ya utandawazi ni kitu ambacho hakiwezekani na ikitokea hivyo una bonge la nuksi
3.Unafika hospitali daktari anakataa kumtibu mgonjwa kwakuwa huna pesa lakini unamiliki vogue .jamani tuwe wakweli ina maana unamiliki vogue lakini huna hata bima ya afya yenu? na hiyo ni hospital au ni kidispensari? kwakuwa hospital kubwa ya hadhi yake hawatangulizi hela bali matibabu kwanza malipo baadae
4.Daktari anakataa kuchukua gari kama bond kwakuwa inakula sana mafuta, hv unaweka bond au unampa dokta aitumie? na hicho ni kidispensari cha mtu binafsi na si hospital .hospital ya kweli ni taasisi ambayo kuna utaratibu wake hivyo huwezi kwenda kuongea na dokta kuhusu malipo
5.una miliki vogue lakini nyumbani huna hata hakiba ya laki5? au huna biashara au huna rafiki binafsi wa kuweza kumkopa ?au hujui wale wanaochukua mali na wakatoza riba ukachukua kiasi unachohitaji?
Tatizo la Bukuku ni tatizo la waimbaji wengi hawana watu mahiri wa kuhariri kazi zao wanatunga wanapeleka studio produser anaweka beat ngoma inaenda hewani matokeo yake ni kutoa sub standards
Napenda kumtetea Bahati Bukuku dhidi ya shutuma zilizotolewa dhidi yake kama ifuatavyo;
Hoja 1. Baaada ya kupata masaibu ya mme wake anahangaika kutafuta msaada wa mawifi na rafiki wa mumewe lakini kila mtu anakuwa na udhuru, ina maana kati ya wote hakuna hata mmoja mwenye msaada?basi kama ni hivyo una matatizo wewe
JIBU. Hapa anajaribu kuonesha hadhira ya watizamaji na wasikilizaji kwamba yapo madhaifu ya wanaume katika ndoa zetu na jamii inayotuzunguka wakati wa matatizo
Hoja2.Anajaribu bank lakini akounti zote anakuta zina shida hivyo hawezi kutoa pesa ,,,katika dunia hii ya utandawazi ni kitu ambacho hakiwezekani na ikitokea hivyo una bonge la nuksi
JIBU Ni kweli ilikua nuksi maana hutokea intenet zikawa hazifanyi kazi kwa wkt fulani benk zikawa zimefungwa (sikukuu)
Hoja 3.Unafika hospitali daktari anakataa kumtibu mgonjwa kwakuwa huna pesa lakini unamiliki vogue .jamani tuwe wakweli ina maana unamiliki vogue lakini huna hata bima ya afya yenu? na hiyo ni hospital au ni kidispensari? kwakuwa hospital kubwa ya hadhi yake hawatangulizi hela bali
matibabu kwanza malipo baadae
JIBU Siku ya kufa nyani miti yote huteleza. Daktari alikua na shida yake sio gari lakini hata pale Muhimbili watu wanakufa kwa kukosa fedha
Hoja 4.Daktari anakataa kuchukua gari kama bond kwakuwa inakula sana mafuta, hv unaweka bond au unampa dokta aitumie? na hicho ni kidispensari cha mtu binafsi na si hospital .hospital ya kweli ni taasisi ambayo kuna utaratibu wake hivyo huwezi kwenda kuongea na dokta kuhusu malipo
JIBU Umeshajibiwa ref Qn No.4
Hoja 5.una miliki vogue lakini nyumbani huna hata hakiba ya laki5? au huna biashara au huna rafiki binafsi wa kuweza kumkopa ?au hujui wale wanaochukua mali na wakatoza riba ukachukua kiasi unachohitaji?
JIBU Hapa anamwakilisha mama wa nyumbani (mke wa boss) wa jamii isiyothamini wake zao mbona wapo wengi tu.Alafu kuwa na Vogue sio issue labda ya mkopo?
Kwa ujumla unapaswa (kama usomavyo kitabu) kuusikiliza wimbo huu hadi mwisho ili uweze kuelewa ujumbe uliobebwa na wimbo wenyewe;
1 Uaminifu katika ndoa umepotea kwake mume, mke na daktari hivyo jamii
2 Rushwa ya ngono kwa daktari na hivyo maofisini
3 Upendo umetoweka miongoni mwetu tusaidiane wakati wa matatizo
4 Kuomba msamaha kwa uliyemkosea ili kuweka sawa mambo yako na MUNGU
5 Uwezo wa MUNGU wa kumsamehe mwanadamu
6 Tunanyoosheana vidole kati yetu "nani kati yenu hana kosa na awe wa kwanza kumtupia mawe" walitawanyika wote pasiwepo wa kumtupia mawe.NAWAKILISHA.