Wimbo Mpya wa Vitali Maembe - Vuma

Wimbo Mpya wa Vitali Maembe - Vuma

Mphamvu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
10,702
Reaction score
3,345

[JFMP3]https://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=177707&d=1408090155[/JFMP3]
attachment.php

Mashairi:-
Vuma

We mama mkaa ndanii, Toka nje usikiee,
Kutwa we kila siku ndanii, Toka basi usikiee.
kuna habari ina vumaa

Vuma x6

Na wee kaka Ughaibuni, Rudi Afrika usikie,
Wewe miaka yote mbali eeh, Rudi basi usikiee,
Kuna habari ina vuma

Vuma x6

Huko unguja mawee, Huko unguja maweee,
Kuna mtu kasimama, Kwenye kona ya Jahazi,
Anahoji uhalali, Uhalali wa Muungano.
Na mwingine kasimama, juu ya kidau chake
Analilia nchi yake, analilia Zanzibari eeh
Huko bara nakoo, kunamtu kasimama
Juu ya kaburi lake, analilia roho yake
Analilia Tanganyika eeh, Vuma vuma vuma

Vuma x6

Safu safu wanapita, wamejaa kwenye mitaa,
Na mabango wameshika, Wanalilia gesi yao,
Wanalili nchi yao wanalilia jina lao
Na wengine wanajipanga waje wadai mlima wao,
Watadai mito yao, Watadai migodi yao,
Watadai mbuga zao, Watawaua na wenzao
Kumbe imekwisha, Kumbe imetoweka amani eeh
Kumbe imepita, Kumbe haina hodi vita
kumbe imefika
Kumbe si demokrasia, kumbe ni demoghasia
Kumbe si democracy, kumbe ni democrazy
‘demonstration of craziness'
Viongozi wanajivunia kuwa watanzania
Wananchi wanavumilia kuwa watanzania

Nchi imetiwa giizaa, Macho yana kiu ya nuuruu
Kumbe imekwisha, Kumbe imetoweka amani eeh
Kumbe imepita, Kumbe haina hodi vita
kumbe imefika
We mama mkaa ndani
Toka nje usikie, kutwa we kila siku ndani eeh
Toka basi usikie.
Na wee kaka ughaibuni, Rudi Afrika usikie,
Wewe miaka yote mbali eeh
Rudi basi usikie, kuna habari ina vuma

Vuma x6
SHUSHA HAPA: View attachment Vuma - Vitali Maembe.mp3
 

Attachments

  • vitali.png
    vitali.png
    27.5 KB · Views: 1,881
Kama una ile album yake yote iweke apa au nyimbo zake nyingine mana nlckia zipatikana free kweny mitandao ila nikisearch sizipati namkubali sana uyu jamaa japo hapati airtym ya kutosha
 
Huyu Jamaa anaimba nyimbo za ukombozi kuanzia sumu ya Teja mpaka hii Vuma na ile anayoelezea watu walikufa wanazikwa na udongo gani mbona hawarudi? Sumu ya teja ukonga keko segerea! We mwanangu Kubali kesi mtoto wa mbone kaenda karudi mnene!
~"Viongozi wanajivunia kuwa watanzania lakini wananchi wanavumilia kuwa watanzania" word up!
 
Bila kusahau kawashauri ma-Diaspora warudi bongo wasikae huko huko! Wamuige billionea!!
 
mimi nilikuwa na program furani ya miaka 2 pale bagamoyo nilimtafuta sana huyu jamaa walau tu ni muone nikashindwa sasa ninasafari nyingine tena lazima nitamuona huyu jamaa anaakiri sana shilingi 5, sumu ya teja na sasa vuma big up kamanda
 
Kama una ile album yake yote iweke apa au nyimbo zake nyingine mana nlckia zipatikana free kweny mitandao ila nikisearch sizipati namkubali sana uyu jamaa japo hapati airtym ya kutosha
Huo tena sasa ni wizi na unyonyaji kwa wasanii.
 
[h=3]Mwanzo wa kuvuma: Na Vitali Maembe.[/h]

[h=2]Vuma![/h]
Katikati ya mwezi Julai 2014 niliwasiliana na Vitali na akaniambia baada ya siku mbili atakuja studio, anazo nyimbo anataka kurekodi. Mimi nilimeza maneno yake kupitia masikio yangu, nikaendelea na shughuli za kawaida.
Baada ya siku mbili Maembe alinipigia simu kunieleza kuwa yupo njiani anakuja studio. Hadi muda huo nilikuwa sijajitayarisha kwa ujio wake. Haikuwa tatizo. Wakati natafakari nini kitafanyika, Nelly akanipigia simu kunieleza kuwa anakuja studio. Ilikuwa afadhali sana maana wiki hiyo nilimtegemea Nuru atakuwapo studio kwa kadhaa zilizokuwapo kipindi hicho. Na mimi niliwasiliana na 'Mugabe' (aka Sindimba Tete) tuweze kupata uwepo wake pia.
Kwenye muda wa saa tano, Maembe alifika na vijana wake wawili - Hussein na mwingine yule anapiga ngoma. Nakumbuka hatua za mwanzo za 'kuvumisha' zilianza kwa ushiriki wangu kidogo baada ya hapo Nelly aliendelea.
Tarehe 2 Agosti 2014, Maembe aliingia kwenye ukumbi wetu hapa 'The Corner' kama mtoa burudani; alikuja na vijana wake kama kawaida - midundo ya muziki 'live' ilisikika. Kwa kuwa John Vocal na Tete wapo mtaani kwetu, waliwasindikiza wageni wetu katika kutoa burudani. Siku hiyo ilikuwa ya uzinduzi wa 'The Corner' - jamii iliburudika.
Waliendelea kurekodi studio hadi tarehe 8/8/2014 ndio nilipousikia wimbo 'Vuma'; niliskia kweli unavuma. Nilijua nitaandika kuhusu wimbo huu, na watu kadhaa walitokea kwenye akili yangu. Na walitokea akilini kwa sababu nyingi tu - ndio zilizopelekea kundelea kuandika.
Nilimkumbuka rafiki yangu Innocent Mnyuku kwa makala moja aliwahi kuandika kuhusu 'Usiku Wa Umoja' uliojumuisha wasanii na vikundi mbali mbali kama vile Zemkala, Vitali Maembe & The Spirits, Gwandumi na Machifu Band..... wengine nimesahau. Huyu jamaa mara nyingi anatoa msisitizo kwangu kuwa nisiache kuandika.
Nilimkumbuka dada 'angu Irene Sanga, maana toka wakati alipotoa album yake ya UTANDAWAZI, sijasikia wimbo uliofanana na 'Wanapangisha' kutokana na nini kimeshibishwa kwenye wimbo. Mpangilio wa vyombo, sauti, na zaidi 'kalamu' - kwa maana ya utunzi.
Niliwakumbuka Jhiko Manyika na Gwandumi ambao ninafahamu uwezo wao na misimamo yao kimuziki na majukumu yao kwa jamii. Pia ni wahitimu wa Bagamoyo College of Arts.

Hapo juu nimeandika kuwa 'nilisikia kweli unavuma' kwa maana tofauti. Kwa sauti za vyombo, nyuzi butu limevuma kwa kiwango. Ushuhuda ninao maana nilikuwapo wakati Tete analivurumisha. Utunzi ni jambo lingine linaloufanya huu wimbo uvume. Wakati muafaka - jamii ipo katika kipindi cha 'kuwekana sawa' kuhusu Muungano, Katiba n.k.
"Kumbe imekwisha, kumbe imetoweka amani. Kumbe imepita."
Hayo maneno yalirudisha kumbukumbu ya miaka ya nyuma, toka wakati wa utoto wangu hadi hivi sasa. Yalinifanya nitambue nini nilichopata. Hayo maneno yalitaka niingiwe na uwoga wa kupoteza/kuishiwa/kutoweka kwa amani. Je imekwisha? Nilijuliza!!
Nilisikiliza tena wimbo huo - nikaamua kuuweka katika makundi mawili; kundi la kwanza ni utabiri na kundi la pili ni rekodi. Rekodi inayowekwa kwa ajili ya kukumbusha hisia za jamii yetu kwa wakati uliopo.
 
I love ths man so much-hasa nyimbo zake ziko poa sana na lugha yake anayoitmia
 
Kitu kizuri kingine kwa huyu jamaa MKALI V. MAEMBE, hutakaa umsikie analialia, ooh wameiba nyimbo yng, ooh nabaniwa, ooh njooni ktk show yng - ntafanya makamuzi ya kufa mtu, oooh sipewi airtym!
Yeee kimya! Anapiga kazi tu, hadhira itatathmini!
 
Kibanga,

Ahsante kwa kushiriki nasi taarifa ya muziki wa Vitali. Nampenda huyu bwana kwa kuwa ni mmoja kati ya wasanii wenye vipaji zaidi hapa nyumbani na zaidi anatumia muziki sauti na gitaa lake kuelimisha na kuhamasisha mabadiliko chanya.
 
Last edited by a moderator:
Kama una ile album yake yote iweke apa au nyimbo zake nyingine mana nlckia zipatikana free kweny mitandao ila nikisearch sizipati namkubali sana uyu jamaa japo hapati airtym ya kutosha
Here's a video to help you sing better: How To Start A Singing Career
 
Kama una ile album yake yote iweke apa au nyimbo zake nyingine mana nlckia zipatikana free kweny mitandao ila nikisearch sizipati namkubali sana uyu jamaa japo hapati airtym ya kutosha

Mm ninayo kama upo dar unaweza kuipata kwani ilitolewa bure
 
Mmoja wa wanamuziki mahiri hapa Tanzania
 
[video]http://www.google.com/url?sa=t&rct=j&q=&esrc=s&source=web&cd=7&ved=0CEsQtwIwBg&url=http%3A%2F%2Fwww.youtube.c om%2Fwatch%3Fv%3Da0uJz1ISjqo&ei=bkk6VO_WJYXtapSogqAF&usg=AFQjCNFYWngOAAIa_9EH-ZclB9P2f-Oiqg&bvm=bv.77161500,d.d2s[/video]
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom