Wimbo: Elimu Dunia by Daz Baba

Wimbo: Elimu Dunia by Daz Baba

NGAYANIMO

Member
Joined
Feb 17, 2026
Posts
36
Reaction score
55
1772397780303.jpg
1772401143908.jpg

DAZ BABA - ELIMU DUNIA.

VERSE.. ( AFANDE SELE)

We ni mfungwa sasa 'si mtu huru/
Ukilalamika sana utakuwa kama unakufuru/
Tu..!!
Lazima ujue sisi ni vifaranga na maisha ni kama mwewe/
Mama yetu ni elimu’ ulio mkataaga we mwenyewe/
zamani..!!
Ulimkataa elimu ya duniani 'ukampiga hadi mwalimu darasani/
Hukusikia la Muadhini wala la mnadi Swala hukuliamini/
Umri ulikudanganya ukawa mbabe shuleni/
Sasa ndio hivyo uko nasi gerezani/
Jiamini mdogo wangu 'kwani jela sio kaburini au kwa Mungu/
Umetengwa na jamii, hujatengwa na dunia hii/
Jifunze kupokea furaha sawa na huzuni/
Kumbuka kwamba tabu na raha zipo duniani/
Zipo kwa ajili ya watu na watu ndio mi na wewe/
Kila mmoja atabeba madhambi yake mwenyewe /
'imeandikwa..!!
Kama umekunywa sumu sasa ya nini uombewe.?
Eenh..?
Sasa ya nini uombewe?

Suleimani msindi a.k.a afande sele member wa Crew ya Watu pori & Ghetto boys msanii kutoka Mji kasoro bahari Morogoro alifanya kweli katika wimbo huu wa msanii
David Selestine Nyika a.k.a Daz baba kutoka kundi la "
" Dangerous Zone Nundaz " au kwa kifupi Daz nundaz ..

Msanii Daz baba alicopy jina la msanii wa Marekani Kwa USA, Daz ni jina la jamaa anaitwa Daz Dillinger, alikuwa mtu wa karibu sana na marehemu 2Pac.

Lakini pia hata huu wimbo wa "Elimu Dunia " Daz baba alitumia Idea ya wimbo wa Marehemu Lucky Dube mwimbaji wa nyimbo Aina ya Reggae kutoka Afrika ya kusini..

Wimbo huo unaojulikana kwa jina la " Prisoner " unaweza ukaunganisha matukio yaliyosemwa na Daz baba katika wimbo wake wa " Elimu Dunia" maudhui yake yanamfanano kabisa na lycris za msanii luck dube kwenye wimbo wake wa "prisoner"

Hukusikia la "Muadhini"(Anaeita adhana) wala la "Mnadi Swala"(anaeinadi swala kuashiria muda wa ibada umefika).

Ukwaju wa kitambo
0767 542 202

Tuwekane sawa hapo ni msanii Afande sele akiwa na shabiki yake na sio Daz baba..
Andiko lililopita la msanii "Pablo " lilileta usumbufu wa uwepo wa maswali & lawama nyingi kwangu mwandishi...
Soma kwa makini andiko before ujacoment

Kifupi mtaalam umekopi na kupaste, sio mbaya japo uandishi hauvutii kivile..
Kwanini umechagua kuweka verse ya qfande sele na ambayo ni ya 3 na ya mwisho kwenye wimbo husika, na hujaweka vesre hata moja ya mwenye wimbo.. ulikuwa unazungumzia ngoma ya elimu dunia ama afande sele ndani ya elimu dunia..

Sio mbaya asante pia, hii ni kati ya ngoma zangu bora kavisa
 
Nilipendezwa zaidi na Verse ya afande sele na sio Daz baba kingine sijacopy jaribu kufuatilia page yangu huko Facebook natumia Ukwaju wa kitambo mara kadhaa ndio imekuwa desturi yangu ya kuandika lycris za nyimbo za zamani.

Dont take it easy ndugu
 
Basi mkuu boresha uandishi wako..
Kichwa cha habari kiendane na habari, na kivutie msomaji..
Hapo ungesema labda cheki afande alivyoinogesha ngoma ya daz baba elimu dunia.
Ama
Afande ni hatari sana kuchana kwendana na mada.. ama vinginevyo,
Mtu unakuwa umemuandaa anajua anasoma kitu fulani na ndio qnakikuta katika mada..

Kila la kheri mkuu
 
Ni ka play ngoma nianze kufuatisha verse nafungua uzi tofauti oya umenimalizia bando nilipe
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom