Mwanakulipata
JF-Expert Member
- Jul 17, 2018
- 718
- 1,202
Habari ya weekend. Katika pita pita zangu hapa jijini Dar haswa maeneo ya centre, nimekuja kushtukia naombwa nauli na watu tofauti tofauti tena waweza kuta unaombwa mara mbili kwa siku moja.
“Samahani kaka nimetokea Kigogo nilikuwa naomba nauli niweze kurudi nyumbani, maana hapa nimepoteza nauli ya kurudi” hii ndo gia anayokuja nayo.
Hivi inawezekanaje watu wengi wapoteze nauli kwa wakati mmoja, na kama wanapoteza, mbona sisi hatuokoti hizo hela wanazopoteza. Au kuna mtu kashawahi kuokota hela stend?
Bila shaka huu ni usanii na sasa hivi ni kuwaepuka vikali.