Wimbi la kuibuka Mitume na Manabii, hicho cheo hupewa na mfumo fulani au huwa wanajipa wenyewe?

officialBossmtoto

JF-Expert Member
Jul 1, 2019
369
1,178
Habari ya uzima wanajamvi.

Mimi leo nina swali dogo ama niseme mdahalo mdogo ulioko kichwani mwangu ambao ningependa kushirikishana na nyinyi ili muweze kunisaidia katika hili.

Kumekuwa na wimbi kubwa la kuibuka kwa viongozi wa kidini hasa upande wa ukristo wanajiita mitume na wengine manabii.

1) Je, Hawa watu wanakidhi viwango gani kupata hio sifa?

2) Je, hicho cheo cha mtume au nabii mtu hujipa mwenyewe au kuna mfumo ambao unampa jina hilo?

3) Kama kuna mfumo unaompa hicho cheo. Je, Mfumo huo unaendeshwa ama kuongozwa na binadamu au Roho?

4) Nasikia kuna Rais wa Mitume na Manabii, kazi yake hasa ni nini?

Naomba tueleweshane na kufundishana na sio kukandiana. Twende kazi.
 
Ni biashara kama biashara nyingine hapo hakuna cha mtume wala nini. Watu wanapenda maigizo ya miiujiza ile ya kudodondoka na kuambiwa matatizo yao yote yamesababishwa na kurogwa na kufungwa toka watoto.

Yani ni biashara moja kubwa sana. Imebarikiwa na serikali kwasababu hao wanawafanya raia wawe watulivu, ndiyo maana wote mara nyingi uwa ni rafiki wa Serikali.

Ni rahisi kumcontrol mtu anayeamini katika kitu kuliko kumcontrol mtu asiyeamini katika chochote.
 
Hawa wahuni wanajipa wenyewe, biblia inavitambua hivyo vyeo lakini si kwa wahuni kama akina Gwaji-boy na wenzake.

Lakini pia, watakatifu ambao huwa tunaomba wauombee, tena wote ni "wazungu" huwa wanapewa ama wtunawapa wenyewe?
 
Ongezeko la ugumu wa maisha linafanya watu kukimbilia huruma/huduma ya kiroho. Huko ndo wanakutana na wale waliouona ugumu wa maisha wakaamua kujiongeza kutafuta kipato kwa kuitumia Fursa ya biblia.
 
Ukiwatazama wahudhuriaji wa hizo ibada yn mpaka unajiuliza 'hawa watu wametoka kulima mpunga au, mbona wamechoka hivi.?'
 
Siku nikisikia kuna mtume ama nabii kaweza kuomba kwa lugha mpaka ATM ikatoa pesa nitaweza kuwaamini hawa Wachungaji fake.

Sent from my SM-J260F using JamiiForums mobile app

Watakukunbusha kwamba imeandikwa usimjaribu Bwana Mungu wako. Ila watapuuzia na kujisahaulisha kwamba nabii Eliya aliomba mpaka moto ukawaka ili kudhihirisha kweli Mungu yupo.
 
Ongezeko la ugumu wa maisha linafanya watu kukimbilia huruma/huduma ya kiroho. Huko ndo wanakutana na wale waliouona ugumu wa maisha wakaamua kujiongeza kutafuta kipato kwa kuitumia Fursa ya biblia.
Laana kubwa sana, the so called "manabii na mitume " ni wapigajimkuliko hatabpapaa msofe:
Hawa watu wanatumia biblia na saikolojia kurubuni, hasa wanawake walioko desperate kupata waume na wenye kutaka shortcut ya maisha [Miujiza badala ya kufanya kazi] ndio wamejazana humo
 
Watakukunbusha kwamba imeandikwa usimjaribu Bwana Mungu wako. Ila watapuuzia na kujisahaulisha kwamba nabii Eliya aliomba mpaka moto ukawaka ili kudhihirisha kweli Mungu yupo.
mbona wanamjaribu mungu kwa kufufua wafu. Haki tena siku nikisikia kuna Nabii ama Mchungaji kaomba na pesa zimetoka kwenye ATM naachana na imani yangu naandamana na kanisa lake.
 
Back
Top Bottom