william Mtitu vs Step Entertaiment Kimenuka sasa

william Mtitu vs Step Entertaiment Kimenuka sasa

cement

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2012
Posts
581
Reaction score
221
BILA STEPS INAWEZEKANA

NA WILLIUM MTITUKwa muda mrefu nimekuwa nikiulizwa sababu ya kuamua kusambaza filamu zangu mwenyewe badala ya kuzipeleka kwa wasambazaji ambao nilikuwa nikifanya nao kazi kwa muda mrefu, yaani kampuni ya Steps Entertainment.Najua maswali yamekuwa mengi kwa kuwa kuna watayarishaji wengi wa filamu nchini wanaohangaika usiku na mchana ili kupata mkataba wa kufanya kazi chini ya kampuni hiyo kwa kuwa Steps Entertainment ndiyo kampuni ya usambazaji inayolipa vizuri zaidi kuliko makampuni mengine yote kwa sasa.Leo nimeamua kuongea walau kidogo …….“Kwanza nikiri kuwa maneno ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, mhesimiwa Dr. Jakaya Kikwete aliyotamka siku aliyoiita Ikulu kamati ya mazishi ya marehemu Steven Kanumba ndiyo yamekuwa yakinisukuma sana hadi kufikia uamuzi huu mzito.Kati ya waliounda kamati hiyo iliyoitwa Ikulu, mimi nilikuwa katibu, Mwenyekiti alikuwa Gabriel Mtitu au maarufu kama Mtitu Game, pia kulikuwa na wajumbe wengine kama Ruge Mutahaba, Asha Baraka, Jacob Steven ‘JB’ na Mzee Chilo. Baada ya kuongea mengi kuhusiana na msiba wa Kanumba na mazishi yake, mheshimiwa rais aliuliza ‘Hivi marehemu Kanumba kaacha filamu ngapi?”Kwa aibu tulimjibu mheshimiwa rais kuwa marehemu Kanumba hajaacha hata filamu moja, zote ni za msambazaji wake na hata mbili ambazo zilikuwa hazijatoka yaani ‘Ndoa yangu’ na ‘Love & Power’ tayari zilikuwa ni za msambazaji kutokana na aina ya mkataba tunayoingia na msambazaji.Mheshimiwa Rais alisikitika sana, akatuambia kuwa yeye hawezi kutumia nguvu kutukataza kuuza mali zetu lakini angependa kuona kuwa tunamiliki wenyewe filamu zetu na tutakapoona tumekwama tumwambie. Aliongeza kuwa kuuza haki zetu ni kama kuuza utu wetu. Maneno ya mheshimiwa Rais yalinichoma sana.Mimi ni msanii wa kwanza kufanya kazi na kampuni hiyo kama mtayarishaji wa filamu na filamu yao ya kwanza kuisambaza ilikuwa ni ‘Jeraha la Ndoa’ ambayo niliitengeneza mimi. Na kwa kuthibitisha hilo, mwaka huu kampuni hiyo ya Steps ilitoa tuzo ya heshima kwa kampuni yangu ya 5 Effects Movies Ltd kwa ajili hiyo.Nasikitika kukiri kuwa filamu zote ambazo nilizitengeneza kisha zikasambazwa na kampuni ya Steps, siyo zangu tena. Kampuni hiyo imekuwa ikinunua haki zote za filamu wanazopelekewa kwa ajili ya kuzisambaza kwa hiyo baada tu ya kusaini mkataba wao unakuwa huwezi kufaidika tena na chochote kutokana na mauzo au faida nyingine zinazotokana na filamu yako.Kwa aina ya mikataba ambayo wasanii na watayarishaji tunaingia na kampuni ya Steps Entertainment, sisi tumekuwa ni wasimamizi tu wafilamu za zao, yaani ni kama manyapara kwenye mashamba ya mkonge wakati kwa ukoloni. Ni waajiriwa tusio na mafao ya uzeeni.Kwa taarifa tu ni kwamba filamu zote mnazoziona mitaani zikisambazwa na kampuni siyo za hayo makampuni yanayotajwa kutengeneza filamu hizo bali ni filamu za Steps Entertainment. Ndiyo maana hata ukienda kwenye Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA) utakuta wasanii wakubwa hawamiliki kabisa filamu lakini kampuni ya Steps inamiliki filamu zaidi ya 400.Kifupi ni kuwa hadithi ni zetu, sehemu za kuigizia ni zetu, tunaigiza sisi, tunarekodi na kuhariri sisi lakini filamu ni za Steps Entertainment na ndiyo maana hata kampuni ya marehemu Steven Kanumba ‘Kanumba the Great’ imesambaratika baada ya kifo chake na mama yake akikabiliana na ugumu wa maisha lakini filamu za Kanumba bado zinatesa kwenye soko la filamu ndani na nje ya nchi.Nawashangaa watu wanaomshutumu mama mzazi wa Kanumba kuwa amemaliza mali za mwanae na sasa anaishi kwa kufadhiliwa na Lulu, wangejua kilicho nyuma ya pazia wangemuonea huruma badala ya kumshutumu. Wakati Steps wanakiri kuwa filamu iliyowahi kuuza sana katika historia ya kampuni yao ni ‘Ndoa yangu’ ya Kanumba, hawasemi kuwa familia yake imenufaika vipi zaidi ya kupewa tuzo.Pamoja na kununua haki zote za filamu, kampuni ya Steps hawatoi malipo ya filamu wanazozinunua kwa muda muafaka hivyo kutufanya tuendelee kuwa mafukara siku hadi siku. Hii ni sababu ya pili ya mimi kujitoa Steps, sitaki familia yangu ije kudhalilika baada ya kifo changu.Fikiria unapeleka filamu yako Steps, mnaingia mkataba wa kuuziana, lakini hawakulipi mpaka wakati watakapoamua kuiingiza sokoni hivyo hata wakikaa mwaka bila kuiingiza utakaa mwaka mzima unasuburi pesa. Hivi kweli mwaka huo utakuwa unakula nini kama umeamua kuifanya sanaa kuwa kazi yako?Cha kuchekesha hata wanapoamua kuiingiza sokoni hawakulipi mpaka baada ya wiki mbili au tatu baada ya filamu yako kuwa imeingia sokoni, utasema hapo wamekulipa au umejilipa mwenyewe baada ya kuwa imenunuliwa?Mfano mwingine hai ni wa marehemu Said Juma Kilowoko (Sajuki) ambaye ni miongoni mwa wasanii maarufu na watayarishaji wa filamu. Marehemu Sajuki alilazimika kuzunguka na wasanii wenziye mikoani akiwa anamuwa taabani ili tu aweze kupata fedha za matibabu jambo ambalo naamini lilimzidishia matatizo ya kiafya.Na kutokana na kuuza haki zetu zote ilibidi mkewe Sajuki, Wastara atengeneze ‘Mr & Mrs Sajuki’ ili aweze kupata fedha za kujikimu na kurekebisha mambo mbalimbali yaliyovurugika wakati akimuuguza mumewe. Kama tungekuwa hatulazimiki kuuza haki zetu zote, familia hiyo ingeweza japo kupeleka filamu zake kwenye vituo vya runinga barani Afrika ambako ni chanzo kingine cha mapato kwa msanii.Baada ya kutafakari kwa kina niliamua kulipia leseni ya usambazaji wa filamu kupitia kampuni yangu ya 5 Effects Movies Ltd ili niwe nasambaza filamu zangu nikitegemewa kupata sapoti kubwa kutoka kwa wasanii wenzangu hasa mastaa wakubwa lakini imekuwa kinyume chake. Kwa sasa naonekana adui mbele ya wenzangu.Kupitia kampuni yangu ya 5 Effects Movies Ltd, niliingiza sokoni filamu ya ‘Omega the Confusion’, na ndani ya masaa matano ya kwanza nilifanikiwa kurudisha gharama zangu zote na kupata faida kidogo. Toka hapo hadi sasa inaendelea kukimbia sokoni hivyo natengeneza faida tu na bado filamu ni yangu, naweza kuifanyia chochote kama kuipeleka kwenye runinga za kimataifa n.kNimalizie kwa kuweka wazi kuwa sina ugomvi wowote na kampuni ya Steps, mmiliki wake wala mtumishi yeyote wa kampuni hiyo. Pia sina chuki na yeyote kati ya wanaoendelea kufanya kazi chini ya kampuni hiyo. Kikubwa ni kuwa haya ni maisha na kila mmoja ana mtazamo wake katika kuyakabili na kujiletea mafanikio”.“WOGA WAKO NDIO UMASKINI WAKO”‘TEAM NYATI’
 
je hayo madudu ya kuuza utu wenu ndo mmeyajua leo hii?
 
Inasikitisha sana....

Ina maana Kanumba,familia yake hawapati chochote sasa hivi licha ya maigizo yake kuendelea kuuzwa kila kukicha!!!,

Yaani filamu yako unaiona inaendelea kuuzwa kila siku ila wewe hauna unachopata tena baada ya yale malipo ya mwanzo!!
 
Mleta mada, hebu twambie on average, ukiuza film yako moja kwa huyo distributor unalipwa shillingi ngapi? Nauliza hivi ili kuweza kujua na kuchangia zaidi kwenye mjadala huu otherwise itakuwa ngumu kumlaumu mwenye kampuni kwa anachokifanya na lakini vile vile kujua kama uamuzi ulioufanya wa kuachana na huduma yake ni wa busara.

Tiba
 
sasa zile vurugu zote za kujifanya wanaendesha mikoko ya bei mbaya na kuishi maisha ya hali ya juu sana huwa mpunga wanatoa wapi, na ina maana hizo filamu zao zinapoonyeshwa na tv za nyumbani kam EATV, Cluods, TBC huwa hawapati kitu, very disturbing.!
 
je hayo madudu ya kuuza utu wenu ndo mmeyajua leo hii?
You dont get. The guy has mobilised resources and opened his own company. Kwanza tumpe hongera kwa ujasiri wa kuamua kufungua kampuni yake mwenyewe [no small feat] sisi wengine tumpe ushirikiano wetu kwa kununua kazi zake.
i for one siyo mpenzi sana wa sinema za bongo kwani nikiangalia 20 ninaweza kutabiri itakuwaje mbele na 9 out of 10 ninakuwa sawa lakini hata hivyo nitanunua kila filamu ya kijana huyu atakayotoa kupitia kampuni yake na ninaomba wanajamii tufanye hivyo kwani mafanikio yake yatawatia changa moto wenzake ili kuondoa hiyo monopoly ya steps intertainment.
 
Mleta mada, hebu twambie on average, ukiuza film yako moja kwa huyo distributor unalipwa shillingi ngapi? Nauliza hivi ili kuweza kujua na kuchangia zaidi kwenye mjadala huu otherwise itakuwa ngumu kumlaumu mwenye kampuni kwa anachokifanya na lakini vile vile kujua kama uamuzi ulioufanya wa kuachana na huduma yake ni wa busara.

Tiba

Mkuu uko serious kweli?
 
Inasikitisha sana....

Ina maana Kanumba,familia yake hawapati chochote sasa hivi licha ya maigizo yake kuendelea kuuzwa kila kukicha!!!,

Yaani filamu yako unaiona inaendelea kuuzwa kila siku ila wewe hauna unachopata tena baada ya yale malipo ya mwanzo!!

so sad kwa kweli, unanyonywa huku unajiona.
 
sasa zile vurugu zote za kujifanya wanaendesha mikoko ya bei mbaya na kuishi maisha ya hali ya juu sana huwa mpunga wanatoa wapi, na ina maana hizo filamu zao zinapoonyeshwa na tv za nyumbani kam EATV, Cluods, TBC huwa hawapati kitu, very disturbing.!

lazima wawe wanatumia njia mbadala ya kuwaingizia kipato maana kila leo wanalia sanaa hailipi.
 
lazima wawe wanatumia njia mbadala ya kuwaingizia kipato maana kila leo wanalia sanaa hailipi.
Kutokana na maneno yao wenyewe ni kwamba sanaa inalipa lakini siyo sana na hii inatokana na mfumo wa monopoly wa distributers. Lakini kitu kingine kinachowamuza wasanii wetu ni ushamba wa kujijengea image ambayo ni artificial. wana invest zaidi kwenye muonekano wao kwenye vivazi, vipando, sehemu za starehe nk. hivyo ndiyo vinawaumiza sana bila ya wao kujua. Vilevile hawa jamaa ni wapuuzi kiasi hawawezi kuunda umoja wa kusimamia kazi zao na ndiyo maana hatua aliyochukua huyu kijana inapaswa kuungwa mkono nasi kwani mafanikio yake yatawaamsha wenzake ambao bado wako kwenye viscious circle
 
Hii kitu ni hatari sana kwa kweli?inabidi serikali ipitie vizuri mikataba ya hawa distributor coz wanawaibia sana wasanii na familia zao wetu
 
Wasanii wa bongo movie Tanzania ni wabinafsi sana,na hata wale wenye umaarufu kidogo imefikia hatua wamejitenga na wenzao kabisa kwa kujiona wao ni masuper star!Kwa yaliyotoke akwa Sajuki (R.I.P BRO) inadhihirisha kuwa hawautaki umoja na kila mtu anaangalia maslahi yake!Kwa maelezo aliyokuwa akitoa Wastara ni kuwa Sajuki alidondoka jukwaani kutokana na mshtuko ambao ulitokana na taarifa alizozipata ya kuwa kuna wasanii wenzao haohao wa bongo movie wanafanya onyesho mahali hapo hapo nia ikiwa ni kumharibia asipate hata hiko kiasi kidogo cha pesa alichohitaji kwa ajili ya matibabu!
Bob Marley alisema "Money can't buy life".Hayo yalikuwa maneno yake ya mwisho kumwambia mwanae Zigy,ina maana kuna kitu alikiona kabla ila kwa hawa wasanii na wasambazaji wanaojiita masuper star,mwisho wa ubaya wao utafika japokuwa utakuwa mbali kidogo!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom