Proved
JF-Expert Member
- Sep 10, 2018
- 27,549
- 34,877
You nailed it man....Huu mjadala kuhusu "weakened America" sanjari na mijadala mingine inayofanana na huu haijaanza leo. Wamarekani na wasomi/wanazuoni mashuhuri wakiwemo kina Samuel Huntington walikuwa wakijadili kuhusu "kudhoofika kwa Marekani" tangu miaka ya 50. Kama mitandao ya kijamii ingekuwepo kuanzia kipindi hicho ikiwemo JamiiForums yetu, ni dhahiri nasi tungekuwa tumekwisha jadili humu muda mrefu sana kuhusiana na suala hili.
Mjadala huu umekuwa sasa kama utamaduni wa mara kwa mara wa Wamarekani. Tangu kipindi cha uimara wa Umoja wa Kisovieti (USSR) uliochochea mapinduzi makubwa ya kiyasayansi zikiwemo operesheni mbalimbali za anga za mbali, kuwepo kwa migogoro mbalimbali ukiwemo ule wa mafuta wa mwaka 73 pamoja na kuwepo kwa vita mbalimbali zilizoihusisha Marekani tangu miaka ya 50, mjadala huu na mingine inayofanana na huu imekuwa ikishamiri.
Katika kipindi chote hicho, wanazuoni walikuwa wakiutazama mwenendo wa utawala wa Marekani katika masuala mbalimbali ya kidunia na kuilinganisha nchi hiyo na mataifa mengine duniani. Leo hii tunaizungumzia China kama mpinzani mkuu wa Marekani katika masuala mbalimbali ya kidunia. Lakini, kipindi cha miaka ya 50 mpaka miaka ya 70 mwishoni, Umoja wa Kisovieti ama USSR ndiyo nchi iliyokuwa akitazamwa kama mpinzani mkuu atakaye pelekea "anguko la Marekani" kwa miaka kadhaa ijayo.
Baada ya USSR kuanza kudhoofika miaka ya 80, wasomi wetu haohao wakahamia kwa Mjapani na kumtaja kama mpinzani mkuu wa Marekani katika masuala mbalimbali hasa kiuchumi. Wasomi, kina Stanley Hoffmann na wengineo walikuwa miongoni mwa wapinzani wakubwa sana wa sera za Marekani miaka ya 80 na walituambia kuhusu habari hiihii ya "anguko la Marekani" huku wakilitumia anguko la USSR kama mfano. Mwaka 1990 na kuendelea, Japan ikaangukia katika mgogoro wa kiuchumi, habari ya Japan ikaishia hapo.
Hivi sasa, wasomi wetu wamehamia kwa Mchina. China sasa inatajwa kama mpinzani mkuu wa Marekani katika muktadha uleule wa kina Japan pamoja na USSR.
Ninachotaka kusema ni kuwa, mjadala huu si jambo geni. Umekuwa ni mjadala wa kujirudia kila baada ya wakati fulani. Wasomi wa miaka ya 50 waliujadili, wasomi wa miaka ya 70-80 wakauendeleza mjadala. Na hivi sasa, wasomi wa miaka hii nao wanajadili kitu kilekile na huenda mjadala ukaendelezwa na wasomi wa miongo kadhaa ijayo na kuendelea. Who knows! Lakini kama ni suala la "weakened America to emerge victorious against communist China" ama kinyume na hapo, muda utatupatia majibu sahihi. Tofauti na hapo, acha tuendelee tu kuuendeleza mjadala.
Asante!