Wilaya ya Tunduru hali si shwari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wilaya ya Tunduru hali si shwari

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Sep 27, 2012.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Sep 27, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Na Steven Augustino,Tunduru IMEELEZWA kuwa Serikali isipochukua hatua za makusudi kuzuia na kutuliza vitendo vya uchomaji wa mabanda ya Nguruwe,kuharibu mali za watu pamoja na kuchoma moto nyumba vinavyo endelea kwa siku tano mfululizo huenda wimbo wa amani na utulivu ambao umekuwa ukiimbwa kila pembe ya nchi yetu ukatoweka hususani maeneo ya Wilayani hapa.

  Minong'ono na kauli za baadhi ya Wananchi kuanza kukosa uvumilivu imeanza kujitokeza kufuatia matukio hayo yanayo onesha kuhatarisha amani yanayo jitokeza mjini hapa huku vikundi vinavyo daiwa kutumia mwamvuli wa madhehebu ya Waislamu wenye msimamo mkali kuendelea kuvamia na kuchoma moto makazi ya watu na mazizi ya nguruwe.

  Kwa mujibu wa matukio hayo katika kipindi hicho Jumla ya mazizi 24 yamelipotiwa kuteketezwa na moto ambao jumla ya nguruwe 61 wameuawa pamoja na kuunguza nyumba za makazi ya watu vyote vikakadiliwa kuwa na thamani kiasi cha zaidi ya milioni 11 vimehalibiwa na kuziacha familia husika zikirudi katika lindi la umasikini uliopindukia.

  Wakiongea kwa nyakati tofauti, waathirika wa matukio hayo ambao wanaishi mitaa wa Nakayaya,Tuleane na Xtended mjini hapa, Luka Victor na Casian Asenga walisema kuwa kikundi hicho ambacho kimekuwa kikifanya matukio hayo majira ya usiku wa manane na kuharibu mali kwa kuchoma mazizi na nyumba zao na kuua nguruwe wameharibu na kuvuluga mifumo ya maendeleo yao.

  Nae Douglas Mwasimba alisema kuwa wahalibifu hao wa mali zake walivamia katika nyumba yake majira ya saa nane usiku wakati amelala na kwamba alisikia nguruwe wanalia kwa pamoja kilio kilichoashiria tukio lisilo la kawaida na alipoamka na kuelekea kwenye mazizi aliona moto mkubwa na tayari nguruwe wake 38 walikuwa wameteketea na moto huo huku nguruwe 51 wakiwa wamejeruhiwa kwa kuunguzwa na moto huo.

  Akielezea kwa masikitiko makubwa Thomas Mumba muuzaji maarufu wa nyama ya nguruwe mjini hapa, alisema kuwa kikundi hicho usiku huohuo kilifika kwake mnamo saa tisa na kilifanikiwa kuchoma zizi na kuua nguruwe 3 na kuwajeruhi wengine 5. Nako kwa Godfrey Mgao nguruwe 4 wameuawa na 5 wamejeruhiwa.

  Aidha Kikundi hicho hakikuishia hapo kwani siku ya pili kiliendelea na kampeni yao hiyo hadi katika Mtaa wa Tuleane na kuchoma moto Mazizi ya Mradi wa Kanisa Angarikana wanaofugiwa katika nyumba ya mchungaji wa Kanisa Mch. Edwin Nakajumo pamoja na mazizi ya Afisa maendeleo ya Jamii Mary Ding'oi ambako walifanikiwa kuchoma mazizi na moto huo kudhibitiwa mapema.

  Walisema inaonesha wazi walengwa wa matukio hayo ni Waumini wa madhehebu ya kikristo Siku ya tatu kikundi hicho kilirudi tena mtaa wa Nakayaya hadi kwa Mchungaji wa Kanisa La Biblia Mch. Yakobo Milanzi na -kufanikiwa kuchoma mazizi na kujeruhi nguruwe 8.

  Haikutosha kikundi hicho kilifika mbali zaidi kwa kutaka kuua watu usiku wa siku iliyofuata kikudi hicho kilifika na kuunganisha umeme (to shorten) kwa makusudi na kuiunguza nyumba na Mashine ya kusaga mali ya Godfrey Christopher pia walifanikiwa kuteketeza kwa kuchoma moto nyumba ya Jastene Severin Magwinda Walifanikiwa na nyumba hiyo iliwaka moto.

  Haikuleta madhara kwa binadamu kwani wote waliolala humo walinusulika kifo kutokana na tukio hilo.Usiku wa kuamkia jana kikundi hicho kimechoma magari mawili likiwemo la mkaguzi wa elimu ya msingi anaitwa haule na gari lingine la milinga kwakweli hali ilipofikia sio pazuri demokrasia inatoweka tunduru

  Akizungumzia matukio hayo Mweyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama, Mkuu wa Wilaya hiyo Chande Nalicho mbali nakukiri kuwepo kwa matukio hayo aliwahakikishia wananchi wa mji waTunduru na Wilaya kwa ujumla kuwa serikali imejipanga kuhakikisha kuwa hali ya usalama inarejea katika hali ya kawaida.

  Aidha Dc,Nalicho aliendelea kubainisha taarifa yake kuwa tayari serikali imeandaa mikakati mbalimbali ya kuhakiksiha kuwa watuhumiwa wa matukio hayo wana kamatwa ili sheria iweze kufuata mkondo wake na akatumia nafasi hiyo kuwaomba Wananchi kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa kwa kuwataja watuhumiwa kwa siri katika ofisi yake.

   
 2. G

  Gene Senior Member

  #2
  Sep 27, 2012
  Joined: May 2, 2012
  Messages: 192
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bado wanafugwa ngoja ufike wakati husika
   
 3. Mlaleo

  Mlaleo JF-Expert Member

  #3
  Sep 27, 2012
  Joined: Oct 11, 2011
  Messages: 9,862
  Likes Received: 3,309
  Trophy Points: 280
  Hivi hata huko Mikoani Magaidi wapo mi nilidhania mikoa ya pwani tu na visiwani!
   
 4. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #4
  Sep 27, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  magaidi hata ikulu wapo.bTW; natamani ningekuwa Tunduru ili niwafundishe hawa watu adabu ya kwetu, kuwa mtu yeyote haruhusiwi "KUCHOMA MBOGA".
   
 5. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #5
  Sep 27, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,012
  Trophy Points: 280
  Serikali ipo katika usingizi wa pono. Eti watu wanachoma moto nyumba na kuharibu mali kwa siku tano mfululizo bila dola kuchukua hatua. Huu ni upuuzi usiomithilika. Umefika wakati sasa raia tuamue kujilinda wenyewe na tusitoe ushirikiano wa aina yeyote kwa jeshi la polisi kwa kuwa wao ndio wasaliti namba moja wa jukumu lao. Polisi wamegeuzwa wanasiasa nchi imemomonyoka. Ingelikuwa na chama pinzani kinafungua tawi hapo Tunduru kamanda wa vikosi maalum(magaidi wa ccm) angelikuwa keshatia timu kuzuia na hata kuua watakaokaidi amri batili ya polisisiem.*Mungu inusuru Tanzania na janga hili la chama dola.
  .
   
 6. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #6
  Sep 27, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,628
  Likes Received: 9,841
  Trophy Points: 280
  duh kazi kweli kweli.......ila wenzetu wanatafuta thawabu hapo kwa mungu...........
   
 7. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #7
  Sep 27, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,903
  Likes Received: 5,365
  Trophy Points: 280
  Nani anaua nyama tamu kuliko zote???
   
 8. s

  sugi JF-Expert Member

  #8
  Sep 27, 2012
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 160
  chombo cha dola kije kufanya nn?kwani hayo ni maandamano?
   
 9. f

  filonos JF-Expert Member

  #9
  Sep 27, 2012
  Joined: Oct 13, 2011
  Messages: 651
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  hilo tatizo lilianzia india na pakstan..wahindi hawali ngombe na wapakstan hawali nguruwe..chumuhim ni ueshim utmaduni wa wengi usilazimishe fuga nyoka ngombe mbizi hawata chomwa haijaanzia tunduru hiyo kule tukuyu hawachomwi sababu ni utamaduni wao na moshi ni utamaduni wao pia sasa wewe upo hapo tunduru umewakuta wana utamaduni wao hata dar mboni hawafugi ngurue au ngombe kariako???
   
 10. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #10
  Sep 27, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  kwakweli hali ni tete ndugu yangu hawa jamaa hawaeleweki kabisa wanajiita kikundi cha uamsho
   
 11. f

  filonos JF-Expert Member

  #11
  Sep 27, 2012
  Joined: Oct 13, 2011
  Messages: 651
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  kafuge ngaruwe zanzibar au mafia au kilwa au bagamoyo igunga usilazimishe biashara yako wewe kila mtu aipende tueshim na tamaduni za watu mlio wakuta pale ....fuga ngombe au nyoka .... Likini ukifuga simba watu wasio mtumia wata wazuru na mwisho watawachoma moto pia ndio maana kule ..syria .egypt ..iraq ..lebanon kuna sehem imetegwa kwa waislam na wakristo....fuga hata panya nyoka .nk
   
 12. Hayajamani

  Hayajamani JF-Expert Member

  #12
  Sep 27, 2012
  Joined: Jul 2, 2012
  Messages: 883
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Kuna kazi kubwa, yote hii ni sababu ya kutotilia mkazo elimu na ajira. Unafikiri hizo ititadi walizonazo laiti wangekuwa na elimu hata ya form VI (ya ukweli sio cheti tu) na angalau wana kazi fulani ya kujipatia kipato hakuna hata mmoja ambaye angefanya hicho kichaa na bado wangeendelea kuwa na imani zao hizohizo. We angalia wote wanaofuata mkumbo wa hayo mawendawazimu ni watu wasio na elimu, kazi malazi mabaya masikini na hata akili zinakuwa masikini vilevile. Pia tunapata somo la kuwa na uzazi wa mpango ili tuweze kuwamuda watoto kwa mahitaji ya msingi ikiwa ni pamoja na chakula na kupata maadili ya wazazi wote wawili. Sio kukimbilia kuoa na kuzaa na kusema Mungu anajua na anapanga, kusema na kuamini hivyo ni kichaa. Mungu alituumba na akili angala kwa mbaaali kama yeye hatupo kama ng'ombe au chura, hivyo sisi hatuongozwi na silika badala yake akili kichwani! Poleni sana wote mliopata hiyo mikasa.
   
 13. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #13
  Sep 27, 2012
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,655
  Likes Received: 2,894
  Trophy Points: 280
  Sasa hao wakishachoma nguruwe hawali nyama yake kweli? Kule Zanzibar walikuwa wakivamia baa wanakunywa kwanza maji ya dhahabu then ndio wanachoma!
   
 14. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #14
  Sep 27, 2012
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  maji ya dhahabu kupotezea harufu
   
 15. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #15
  Sep 27, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,512
  Likes Received: 5,742
  Trophy Points: 280
  Waambie wasubiri wanakuja wenye nchi wako dodoma wanapeana vyeo kwanza ok?
  Reply if ntd pls
   
 16. RICH OIL SHEIKH

  RICH OIL SHEIKH JF-Expert Member

  #16
  Sep 27, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 882
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hivi si kuna mipaka ya ufugaji, maana nadhani hata kiafya si sahihi mifugo kuishi jirani na makazi ya binadam. Wakafuge kwenye mashamba yao huko.
   
 17. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #17
  Sep 27, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,628
  Likes Received: 9,841
  Trophy Points: 280
  mkuu kama sijakusoma vile.........
   
 18. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #18
  Sep 27, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,474
  Likes Received: 5,858
  Trophy Points: 280
  Hivi huyo mungu sijui allah alimuumbia nini huyu mdudu na kumjazia mautamu yote yale?..its just a waste of time really
   
 19. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #19
  Sep 27, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,628
  Likes Received: 9,841
  Trophy Points: 280
  kwa hiyo hapa ni syria??
   
 20. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #20
  Sep 27, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,474
  Likes Received: 5,858
  Trophy Points: 280
  Kwani nyiye mlikatazwa kula au mlikatazwa watu wengine wasiwafuge?
   
Loading...