WIKIPEDIA wamkaanga Edward Lowassa, sijui ataponea wapi huyu bana

Kama unaamini mambo ya wikipedia utakuwa mburula kwa maisha yako yote, huko ni suala la mitazamo, uwongo na uzandiki mkubwa. Never trust wikipedia always
So long Wikipedia ni chanzo cha habari, ni vema tukaitumia then analysis tukaifanya kwa mtazamo wetu. By the way, nampongeza Hot Lady kwa kulibaini hili. Hakika Lowasa hana thamani tena
 
Lowassa hafai kuwa rais wa watanzania kwakuwa hawezi kuongoza hata muhula mmoja kwasababu ya afya yake...mgogoro kweli...
Hata akifa baada ya siku mbili haina shida,jambo la msingi ma la mhimu ni kuitoa ccm madarakani kwamza mengine baadae.
 
Edward Ngoyai Lowassa


Edward Ngoyai Lowassa
Mbunge
Bunge laTanzania
Jimbo la uchaguziMonduli (Arusha)
Tarehe ya kuzaliwa26 Agosti 1953
ChamaCHADEMA (tangu 28/07/15)
Tar. ya kuingia bungetangu 1990
Alirudishwa mwaka2005
Waziri Mkuu wa Tanzania
Alingia ofisini2005
Alitanguliwa naFrederick Sumaye
DiniMkristo
Elimu yakeChuo Kikuu
Digrii anazoshikaMA (Development Studies) University of Bath (Uing.)
Kazimwanasiasa
Edward Ngoyayi Lowassa (amezaliwa 26 Agosti 1953) ni mwanasiasa nchini Tanzania.
Alichaguliwa kuwa Waziri Mkuu wa kumi wa nchi hiyo tarehe 30 Desemba 2005 akalazimishwa kujiuzulu tarehe 7 Februari 2008 kwa kuhusika kwake na utoaji wa tenda kwa kampuni ya umeme ya Richmond ambapo yeye alihusika moja kwa moja na upatikanaji wa kampuni hiyo ambayo ilikuja kubainika kuwa ni kampuni hewa
Yaliyomo






Maisha

Lowassa ni mwenyeji na alikuwa mbunge wa Monduli katika Mkoa wa Arusha.
Alisoma shahada ya kwanza katika mada ya tamthilia kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, halafu shahada ya pili katika sayansi ya maendeleo ya jamii kwenye Chuo Kikuu cha Hull nchini (Uingereza).
Mnamo tarehe 28 Julai 2015 alijunga rasmi na chama cha upinzani cha CHADEMA. Hiyo ni baada ya kukatwa jina lake katika kinyang'anyiro cha Urais kupitia chama tawala cha Chama cha Mapinduzi. CCM walilazimika kukata jina lake kutokana na mwanasiasa huyo kukumbwa na kashfa nyingi za kifisadi ikiwa ni pamoja na kashfa ya Richmond pamoja na kutoa rushwa kwa wajumbe wa vyombo vya maamuzi ndani ya chama kama NEC, Kamati Kuu na Mkutano Mkuu
Siku chache baadaye aliteuliwa kuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya CHADEMA mnamo Oktoba 2015.
Nyadhifa mbalimbali alizowahi kushika

Lowassa ni mwanasiasa mkongwe mwenye uzoefu mbalimbali katika siasa za nchini Tanzania, kwa kuwa aliwahi kushika vyeo mbalimbali katika serikali kama vile:

  • Waziri mdogo wa mazingira na mapambano dhidi ya umaskini katika ofisi ya Makamu wa Rais (1988-2000)
  • Mkurugenzi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (1989-1990)
  • Waziri mdogo wa haki na mambo ya bunge katika ofisi ya Makamu wa Rais (1990-1993)
  • Mbunge wa Monduli tangu 1990
Waziri wa ardhi na makazi (1993-1995)

Akiwa Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Mijini, Lowasa alitumia fursa hiyo kujitwalia na kujimilikisha viwanja kadhaa kwa manufaa yake na maswahiba wake. Lowasa anamiliki ranchi kubwa kabisa ambazo awali zilikuwa chini Ranchi ya Taifa na kuwa mikononi mwake. Lowasa anamiliki maeneo mengi huko Monduli Arusha na maeneo mengi ya mikoa ya Arusha na Manyara. Pia Lowasa anamiliki viwanja kadhaa ndani ya miji mikubwa ambapo amejenga majumba kadhaa ya kifahari na nyumba za kulala wageni. Chanzo cha fedha alizotumia kujenga majengo hayo bado kingali kujulikana
Waziri wa Maji na Mifugo (2000-2005)

Miaka 2000–2005 Edward Ngoyai Lowassa alikuwa waziri wa maji na maendeleo ya mifugo. Aliitumia nafasi hiyo kwa upendeleo mkubwa ambapo miradi mingi ya maji aliielekeza kwenye jimbo lake. Alihakikisha kuwa jimbo lake na mikoa ya kaskazini na hasa Arusha na Kilimanjaro inatengewa bajeti kubwa. Pia Lowasa alitumia fursa hiyo kuhamisha miradi ya maji kutoka maeneo mengine ya nchi na kupeleka jimboni kwake Monduli
Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (2005-2008)

Tarehe 29 Desemba 2005 Lowassa aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu. Baada ya kula kiapo cha kutumikia nafasi hiyo, Lowasa alianza kupanga mikakati ya kuliibia taifa. Miongoni mwa mikakati hiyo ni kushirikiana na wataalam ili kutumia mikataba ya serikali kuwaibia wananchi. Lowasa alitumia vema fursa zilizokuwa zinajitokeza kwa manufaa yake. Fursa hizo ni pamoja na ukame na ukosefu wa umeme. Ili kukabiliana na ukame, Lowasa alikuja na mkakati wa kuagiza mvua ya kutengeneza toka Thailand. Hata hivyo, mradi huo haukuweza kutekeleza baada ya kulazimishwa kujiuzulu nafasi ya Waziri Mkuu.
Pia Lowasa alitumia vema tatizo la ukosefu wa umeme. Ndipo Lowasa alipojiingiza kwenye kashfa ya Richmond ambapo alitishia kuwa nchi itakuwa gizani na kwamba ni lazima ipatikane kampuni ya kufua umeme wa dharura. Ndipo yeye akajifanya kuwa ni mtaalam ambapo alikuwa anaingilia majukumu ya wataalam wake. Ijapokuwa kulikuwa na makampuni mengi yenye sifa, kwa ushawishi wake, Lowasa akalazimisha ipewe kampuni ya Richmond ambayo baadaye ilikuja kugundulika kuwa ilikuwa ni kampuni ya mfukoni.
Kutokana na kadhia hiyo, Bunge lililazimima kuunda kamati Teule chini ya Mbunge wa Kyela, Dr Harrison Mwakyembe ili kufanya uchunguzi wa kampuni hiyo tata. Hatimaye Kamati ikawasilisha maoni yake Bungeni ambayo yalimfanya Lowasa asiwe na hadhi ya kuendelea kuwa Waziri Mkuu
MWAKYEMBE AMWAGA LAZI BUNGENI
MH. HARRISON MWAKYEMBE
MBUNGE WA KYELA NA MWENYEKITI WA KAMATI TEULE YA KUCHUNGUZA MADUDU YA KAMPUNI YA RICHMOND, MH. HARRISON MWAKYEMBE, ALISOMA MBELE YA BUNGE RIPOTI YA KAMATI YAKE KWA UWAZI NA UKWELI KWA MUDA WA DAKIKA TAKRIBAN 80.
KAMATI TEULI HIYO IMEBAINI KWAMBA MKATABA WA RICHMOND ULIFIKIWA KWA UPENDELEO, RUSHWA NA UBABE WA VIONGOZI WAANDAMIZI SERIKALINI, NA KWAMBA LICHA YA USHAURI WA KITAALAMU NA HALI HALISI WAKUBWA WALILAZIMISHA USAINIWE. hIVYO PAMOJA NA MAMBO MENGINE KIBAO IMEPENDEKEZA MIKATABA YOTE YA NISHATI IPITIWE UPYA KAMA ILIVYO MIKATABA YA MADINI
KAMATI TEULE HIYO KUPITIA MDOMO WA MH. MWAKYEMBE IMETO MAPENDEKEZO KAMA 15 HIVI, BAADHI YAKE YAKIWA:
1. WAZIRI HUSIKA WA WAKATI HUO (MH. DR MSABAHA) NA KATIBU MKUU WAKE WAKATI HUO WAPEWE ADHABU KALI
2. WAZIRI WA SASA WA NISHATI NA MADINI MH. NIZAR KARAMAGI NA MWANASHERIA MKUU WAWAJIBISHWE KWA KUWEZESHA MKATABA WA RICHMOND KUHAMISHIWA KAMPUNI INGINE
3. UONGOZI WA TAKURU (SASA TAKUKURU) UFANYIWE MABADILIKO HARAKA KWA KILICHODAIWA KUTOA TATHMINI ISIYO SAHIHI JUU YA MAZINGIRA YALIYOUZUNGUKA MKATABA WA RICHMON.
4. MKATABA WA RICHMOND AMBAYO IMEIPASIA KAMPUNI YA DOWANS UCHUNGUZWE UPYA.
5. MSIMAMIZI MKUU WA SERIKALI AMBAYE NI WAZIRI MKUU ATUMIE BUSARA ZAKE KUAMUA NINI CHA KUFANYA BAADA YA RIPOTI KUANIKWA HADHARANI
AIDHA JUHUDI ZINAFANYIKA KUIPATA RIPOTI YOTE HIYO NA KUANGALIA NAMNA YA KUWEKA HADHARANI ILI HADHIRA IJUE KILA KITU KWA UWAZI NA UKWELI.
PSSST! SASA TUNASUBIRI RIPOTI YA MADINI YA KINA KABWE
Uchaguzi mkuu 1995

Mwaka 1995, Lowasa aliamua kuingia rasmi kwenye kinyang'anyiro cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hata hivyo, Lowasa hakufanikiwa kupenya kwenye tano bora kati ya majina 11 yaliyojitokeza kuwania nafasi hiyo ambapo Benjamin Mkapa aliibuka kidedea.
Sababu za Lowasa kutopenya kwenye tano bora zilitolewa ndani ya Kamati Kuu ambapo moja ya sababu ni kutokuwa mwadilifu. Uadilifu ni dhana pana ambapo inajumuisha na kujihusisha kwake na kashfa mbalimbali za ufisadi. Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alitoa sababu za Lowasa kuondolewa licha ya kwamba alikuwa na wapambe wengi ambao baadaye ilikuja kubainika kuwa alikuwa amewahonga
Ahsante Mkuu kwa kutuwekea vema. Wengine tulikuwa tunashindwa kuipakua
 
Wikipedia ! Iyo yeyote anaweza kuandika chochote, wadanganyeni wasiofahamu. Ni nyie wenyewe mmeandika uo uchafu halafu mnakuja kujaza server za jf..
 
Lowassa hafai kuwa rais wa watanzania kwakuwa hawezi kuongoza hata muhula mmoja kwasababu ya afya yake...mgogoro kweli...

"Tuna imani na lowassa"
Wajumbe wa mkutano mkuu wa ccm.
Hivi sisi wengine tukiwa na imani naye mbona inawauma.
 
Kaka zangu, hebu pakueni wenyewe muone jinsi wenzetu wazungu walivyoandika historia ya Edward Lowasa. Hakika inahuzunisha na inasikitisha. Nilijua haya mambo anasingiziwa kumbe hata wenzetu wazungu wanamuona vivyo hivyo. Kwa ujumla wake Lowasa ni fisadi na mtumiaji vibaya wa madaraka
View attachment 275620View attachment 275621View attachment 275622View attachment 275623View attachment 275624View attachment 275625We're

https://sw.wikipedia.org/wiki/Edward_Ngoyai_Lowassa

wewe in mgeni wa page hizi? Jaribu kuposti upuuzi wowote na utachapishwa! Na ni nini kinakuaminisha Kamba wazungu wakiandika basi ni kweli tutu? Una hakika gain ni wazungu? Jaribu uposti I like uupate uzungu! Upuuzi mtupu!
 
Lowassa hafai kuwa rais wa watanzania kwakuwa hawezi kuongoza hata muhula mmoja kwasababu ya afya yake...mgogoro kweli...

We daktari kama kweli tujuze afya yake ina matatizo gani? ili sisi wapiga kura tuwe na taarifa sahihi? kuhusu mgombea huyu.
 
Vyanzo vya habari ambavyo vimetumika kama source ya habari katika wikipedia ni Uzi wa jamii forum na source zake hazifunguki kabisa kwa vile ni za uongo
 
Kama unaamini mambo ya wikipedia utakuwa mburula kwa maisha yako yote, huko ni suala la mitazamo, uwongo na uzandiki mkubwa. Never trust wikipedia always

Kila mtu anaandika atikovyake kule hata mini kipindi flani nimekua mwandishi wa baadhi ya atiko za wikipedia na nilishawahi kujiandika kama mtu maarufu Tanzania wakati hata majirani zangu tu hawanijui.
 
Sio wazungu walivoandika.wikipedia ni kila mtu anaweza akaandika atakacho.ipo open kwa kila mtu.na ndio maana wikipedia sio source nzuri ya kurely on essential information.hata mimi naweza nikaandika historia ya Hot Lady sahizi wikipedia

Mleta mada ndipo uwezo wa uelewa wake ulipoishia. Hajui hata wikipedia inavyofanya kazi. Hajui kwamba unaweza kuweka hata ile habari iliyofanya ze utamuz kufungiwa na ikakaa vile vile. Aache umburula!
 
Back
Top Bottom