WIKILEAKS: Insight Kuhusu Idara ya Uhamiaji na vyombo vya usalama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

WIKILEAKS: Insight Kuhusu Idara ya Uhamiaji na vyombo vya usalama

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mtazamaji, Sep 9, 2011.

 1. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #1
  Sep 9, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Katika Wikileaks cabale 06DARESSALAAM1944 tunaona namna mfumo wa taifa letu wa uhamiaji unavyofanya kazi, mapungufu yake na uwezo wake na mpinang yake. Siju tumefikia wapi

  • Tunano msisistizo na Mkazo mkubwa wa usalama uko kwenye POE za anga na Namanga pekee.
  • Tunaona ofisa wa uhamiaji uhamiaji akisema hakuna ushirikiano wa kupeana taarifa na vyombo vingine. Kosa ambalo wamrekani wanajutia mpaka leo
  Baadhi ya Nukuu

  Soma cable kamili Zimefichuka » Blog Archive » GLOBAL PURSUIT OF TERRORIST INFORMATION
  Au kaisome from original source Cable Viewer

  Note:
  taarifa hiyo imekuwa created 19.12.2006 . Where are we now?
   
 2. VUVUZELA

  VUVUZELA JF-Expert Member

  #2
  Sep 9, 2011
  Joined: Jun 19, 2010
  Messages: 3,106
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Idara ya uhamiaji wanajua wakibanwa sana basi ule ulaji wa kutoa work permits bwerere utaisha
   
 3. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #3
  Sep 10, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Sasa kama ni kweli mtuhumiwa wa kutorosha wanyama raia pakisatan ameweza kuondoka nchini tena kupitia uwanja wa nege DIA Basi ni kweli cable hiyo inavyosema . vyombo vya usalam havipeani habaari vinavyotakiwa kupeana. mambo yapo kama yalikyokuwa mwaka 2006.

  Hilo ni Moja ya kosa walilfanya wamarekani na hivyo kujikuta kwenye matatizo ya September 11.

  Tujiulize huyo raia wa pakistan kama kaweza kuondokea uwanja wa DIA( JKN) ni wahalifu wangapi wanaingia na kutoka kirahisi kupitia mipaka ya kagera, Kigoma, Tarime n kwingineko
   
 4. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #4
  Sep 10, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Kuna aliwai kuingia na AK47 uwanja wa Mwalimu Nyerere Airport nikashangaa sana! Pale wapo kibisha zaidi na hasa kusumbua ngozi nyeusi tu.
   
 5. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #5
  Sep 10, 2011
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mkuu mipaka yetu na forodha zetu ziko very porous. Ukisikia watanzania wanaokamatwa na dawa za kulevya nje wanaotoka DIA huwa wanapitia sehemu ya VIP, na wengine wakitaka kuingiza vitu visivyotakiwa kuingia wanapiga simu tu. Serikali ikiamua ku-deal na tatizo hilo inaweza, tatizo ni kuwa haitaki na haina haja.
   
 6. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #6
  Sep 10, 2011
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,660
  Likes Received: 415
  Trophy Points: 180
  You may be right. nadhani binafsi nilishawahi kushuhuda kitu kama hii mara ya mwisho nilipowasilia JKN. Mdada mmoja Mswahili tumekuja na ndege moja alikuwa na masanduku makubwa kama matatu, na hakupita hata customs, wakamwambia asubiri hadi "mwenyeji" wake atokee.

  Lakini binafsi customs walinisimamisha na kuniamuru nifungue masanduku yangu yote pamoja na kutaja gharama ya mali nilizokuja nazo ambazo nyingi zilikuwa ni vizawadi kwa mtoto, familia, ndugu na jamaa.

  Hapohapo afisa wa customs ananiambia pembeni kwa Kiswahili nimpe kiasi fulani cha pesa aniruhusu nitoke, lakini baada ya kukataa ombi la rushwa, hapo ndipo ikazuka tafrani kubwa mbele ya Customs, Polisi na abiria wengine ambayo ilidumu kwa saa kama mbili ambapo baadaye niling'amua kuwa sitashinda game na ikabidi nilipe tu kodi waliyodai yote kulingana na kuropoka kwangu tu thamani ya mali niliyokuwa nayo, baada ya wao kuniuliza trick question yao eti una mali ya thamani gani kwenye mzigo wako? Yote hayo yanafanyika huku yule mdada mwenye masanduku manne makubwa tuliyekuja ndege moja ametulia tuli pembeni akisubiri mpambe wake aje kumwokoa mbele ya Customs, TRA na Polisi. Nimeondoka airport, yule mdada nimemwacha na masanduku yake amabayo customs hawakudiriki kuyachunguza kama walivyonifanyia,sembuse Wazungu kibao na watu wengine wenye ngozi nyeupe ambao wote waliruhusiwa kupita bila mizengwe.
   
 7. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #7
  Jan 25, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,534
  Likes Received: 5,685
  Trophy Points: 280
  Uhamiaji ifumuliwe! Imeoza kabisa kwa rushwa! Hawana mbinu kugundua wadanganyifu na watumishi wengine wanajua ukweli lakini ndio system ya ulaji!
   
 8. JamboJema

  JamboJema JF-Expert Member

  #8
  Jan 25, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,148
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Nijuavyo mimi work permits hazitolewi na Uhamiaji bali Idara ya Kazi ya Wizara ya Kazi....
   
 9. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #9
  Jan 25, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Kwa mda mrefu nimeendelea kuckia tatzo la uhamiaji,wahucka hawajui?
   
Loading...