Wiki ya wanawake Tanzania au wanawake wa ccm

Wiki ya wanawake Tanzania au wanawake wa ccm

Yona F. Maro

R I P
Joined
Nov 2, 2006
Posts
4,201
Reaction score
255
Ndugu zangu

Saa hizi katika viwanja vya mnazi mmoja jijini dare s salaam kuna kuna ufunguzi wa wiki ya wanawake unaendelea , nimejaribu kupita hapo kidogo kujionea mambo yalivyo na hali ilivyo , kwanza ukiwa nje utaona matangazo ( WIKI YA WANAWAKE TANZANIA ) lingine likisema ( WANAWAKE WAJASIRIAMALI TANZANIA ) lakini ndani ya uwanja wenyewe kwa sasa ni ngojera tu meza kuu imejawa na rangi za kijani , wanafunzi wanaoimba nyimbo za kusifu nao wako kwenye mavazi ya kijani yanasifu upande mmoja .

Nafikiri waandaaji wa tamasha hili hawatendi haki , kama wanasema wiki ya wanawake basi waondoe alama yoyote ile ya kichama au kimakundi na waalike wanawake wote wa Tanzania bila kujali nani anatoka chama gani kama ilivyosasa hivi

Enzi hizi ambapo wanawake wanatakiwa washikamane wawe kitu kimoja bado kuna watu wanawatengenezea makundi kama haya , wao wenyewe wanajitenga ndani yao kama hivi ilivyo kwa kweli sio dalili nziri hata kidogo .
 
Back
Top Bottom