Wiki ya msaada wa Kisheria: Maswali na Majibu

Amicus Curiae

JF-Expert Member
Sep 12, 2012
4,809
6,342
"Usimamizi Bora wa Mirathi kwa Maendeleo ya Familia".

Hiyo hapo juu ni kauli mbiu ya mwaka huu tunapoianza wiki ya msaada wa kisheria inayoanza leo tarehe 12-18 Novemba.

Nakaribisha maswali mbalimbali kwenye eneo la MIRATHI, naahidi kuyajibu maswali hayo kwa weledi mkubwa na lugha nyepesi sana inayoeleweka kwa urahisi.

Karibuni...

Screenshot_20201111-212212.jpg
 
"Usimamizi Bora wa Mirathi kwa Maendeleo ya Familia".

Hiyo hapo juu ni kauli mbiu ya mwaka huu tunapoianza wiki ya msaada wa kisheria inayoanza leo tarehe 12-18 Novemba.

Nakaribisha maswali mbalimbali kwenye eneo la MIRATHI, naahidi kuyajibu maswali hayo kwa weledi mkubwa na lugha nyepesi sana inayoeleweka kwa urahisi.

Karibuni...

View attachment 1625029
Naomba tuwekee journals za TLS mkuu
 
Naomba tuwekee journals za TLS mkuu
Mama X alifariki mwaka 2012 na kuacha watoto watatu A, B wakiwa wa baba mmoja na C aliyekuwa under 18 wa baba tofauti. Mama X aliacha vyombo vya ndani, kiwanja kimoja alipokuwa amejenga boma hadi usawa wa madirisha. Mirathi ilifunguliwa mahakamani na A alichaguliwa kusimamia mirathi ya mama x. Stahiki za mama x kazini ilikuwa 15million. Ambayo ilitumika katika kugharamia kodi za ya nyumba walipoachwa A,B, na C kwa miaka kadhaaa, na kiwango kikubwa kumsomesha C katika sekondari hadi form 4 na baadae chuo hadi C alipogomesha kuendelea na masomo kwa sababu zake mwaka 2018 baada ya kutimiza 18. B alipata kazi sehemu na huko akakopa mara kadhaaa na kuendeleza boma la mamma yao yeye peke yake na wakaamia hapo 2016 ikiwa nyumba iliyokamilika kwa 99%. A alifariki 2019. Kuanzia 2019 C alianza tafrani nyumbani, na sasa amempeleka B mahakamani akidai A ambaye ni marehemu kwa sasa atenguliwe usimamizi wa 'mirathi" kwa kuwa alidhurumu mali za marehemu na pili nyumba wanayohishi iuzwe wagawane fedha na B. Mahakama imewarudisha nyumbani wazungumze na warejeshe majibu baada ya mwezi mmoja. Mwezi umekaribia kuisha na wameshindwa kuelewana. Naomba ufafanuzi wa which is which katika hali hiyo na nini kinaweza kufanyika?
 
Back
Top Bottom